Nawatakia heri ya sikukuu za Christmass na Mwaka mpya wana UKAWA tu popote mlipo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,660
218,148
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza na bila kuweka fitna au unafiki wowote , ninaomba kuchukua nafasi hii kuwatakia heri ya sikukuu hizi maarufu sana duniani wapenzi , washabiki na wanachama wote wa vyama vinavyounda UKAWA popote walipo duniani .

Sitaki kuchuma dhambi yoyote , na ndio maana sikutaka kuwahusisha wanaccm kwa vile siwapendi kuliko kitu chochote kinachoonekana ama kisichoonekana katika nchi hii , fitna kwangu mwiko .

Pia nachukua nafasi hii kuwapa pole wana UKAWA wenzangu kwa yote mliyopitia na mnayoendelea kupitia kwenye siasa za kishamba zinazofanywa na zinazoendelea kufanyika kwenye nchi yetu .

2018 - NEVER GIVE UP , mapambano ya kudai haki , demokrasia na utu wa Mtanzania yaendelee kwa kasi ya radi.

Mungu ibariki UKAWA .
 
Mimi so mwana UKAWA kwa kuwa sina chama, pia sio m ccm.
Hivyo napokea salam zako na kukutakia heri pia.
Pia niwatakie heri ya krismasi wana ccm wanaochukizwa na vitendo vya kigaidi mf. dhidi ya Tundu Lissu, Benn Saanane, Azory Gwanda etc
Umeandika kikamanda mtupu !
 
Back
Top Bottom