Merry Christmas kwa UKAWA wote na vyama rafiki tu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,641
218,091
FB_IMG_1545652147908.jpg

Wakuu , kwanza kabisa natanguliza salamu zilizojaa bashasha za mafanikio , baada ya salamu hizi nisiwachoshe na maneno mengi naomba niingie moja kwa moja kwenye hoja yangu .

Nachukua nafasi hii kuwatakia wana UKAWA na vyama rafiki pekee heri ya sikukuu ya christmas na Mwaka mpya , nyinyi ndio tegemeo na dira ya nchi hii , mliyoyafanya kwa kipindi cha mwaka huu , tena katika mazingira magumu kuliko ya kuzimu ni mambo ya kutukuka ! uvumilivu na ujasiri wenu hauwezi kufananishwa na kitu chochote , mmefanya siasa katika kipindi ambacho ukijiita mpinzani ni sawa na kukaribisha kifo , mmebambikwa kila aina ya kesi kwa maelekezo kutoka juu , ama kwa hakika nyinyi ni washindi , taarifa mpya zinaonyesha kwamba bunduki mlizoonyooshewa usoni zinazidi idadi ya bunduki walizonyooshewa majambazi wote wa eneo la maziwa makuu

sijui niseme nini ili ionekane nimetambua ujasiri wenu ambao wale wenzenu waoga na wachumia tumbo , wale waliojaa ubinafsi , wale mliowabeba mithili ya watoto njiti kwenye uchaguzi hadi wakatwaa majimbo na kata , wakashindwa mapambano na kuamua kujiuza mithili ya makahaba wa makaburi ya kinondoni , Hakika najivunia kuwa pamoja nanyi hadi mwisho wa mwaka huu.

Si rahisi kumaliza maneno juu ya ujasiri mnaoendelea kuuonyesha katika mapambano yenu ya kupigania haki , usawa , demokrasia , utu na heshima ya Mtanzania

Mwisho nimtakie heri ya Christmas Mh Freeman Mbowe , namwambia hivi huko Segerea hajaenda kifala , amekwenda kwa vile amekataa kumkiri na kumpigia goti Shetani , amekwenda kwa sababu ya uchungu wake kwa Utu wa Mtanzania , na hakika ushujaa wake umetukuka .

Merry Christmas kwa mara nyingine .
 
Asante.
 
Mungu awabariki wote wote hawa watu.Lakini Mungu wa mbinguni awanyooshe mkono hata wale wa upande wa pili,wauaji, wapiga risasi wenzao,wakandamizaji wa haki za wenzao,miungu watu wenye kejeli na majivuno.Nawaambia mwenye enzi huwa hashindwi.Mungu simama nyoosha mkono wako Kwa Lissu,Ben Saanane,Alphonce Mawazo,Azory,Akwilina n.k.
Upo Mungu,Upo Mungu
 
Mungu awabariki wote wote hawa watu.Lakini Mungu wa mbinguni awanyooshe mkono hata wake wa upande wa pili,wauaji, wapiga risasi wenzao,wakandamizaji wa haki za wenzao,miungu watu wenye kejeli na najivuno.Nawaambia mwenye enzi huwa hashindwi.Mungu simama nyoosha mkono wako Kwa Lissu,Ben Saanane,Alphonce Mawazo,Azory,Akwilina n.k.
Upo Mungu,Upo Mungu
nimeguswa sana na andiko lako
 
Back
Top Bottom