Nawashauri CHADEMA wajiunge na CCM

Endelea kusubiri hizo taasisi za kimataifa tu mkuu, lkn mwisho wa siku utaishia kulia lia tu...Mbowe anawaharibia
 
Changia basi na hapa tukuone
 
Na lowassa akirudi na kundi lake, hawana ubavu tena wa kumuita fisadi maana wameshamsafisha wao wenyewe.
Binafsi ningependa lowassa abaki huko huko mpaka awamalize kabisa.
 
Nonsense. Hivi nyie mnadhani huyo Mungu ni wa kwenu tu? Ukitaka kumjua Mungu jinsi alivyo kwamba ni wa wote nenda kamuulize Farao siku ni kutaka huko mbinguni. Pharaoh has a very interesting tale to tell you
Tulianza na Mungu na tunamaliza na Mungu.
 
Hata 2015 mlisema hivi hivi,
Hao wabunge wako 7 unaowasemea wanapatikana kutokea mkoa mmoja tu
 
Changia basi na hapa tukuone

Mkuu mbona tunachangia sana labda wewe ndio mgeni humu jukwaani. Nilipoona anasema kuhusu Lowassa nikajua hana jipya na marudio tu. Tunataka sababu mpya zenye mashiko lakini hizo za Lowassa tumeshakubali muda mrefu kwamba wapinzani tulichemka. Sasa ukisema sababu ya kushindwa wapinzani ni kwa sababu ya Lowassa ni kama mnatuona labda sisi ni wajinga fulani. Toka Lowassa yuko ccm wapinzani wanashindwa, malalamiko yao ni kuwa uwanja wa ushindani hauko sawa na ccm hawako tayari kurekibisha hilo. Hilo la Lowassa ni tatizo dogo na wala sio sababu ya ccm kushinda jana.

Sababu ya ccm kushinda jana ni kuhakikisha rais anafurahi. Wengine toka tulipoona madiwani waliohama kwa rushwa wanapokelewa kwenye hafla ya jeshi moja kwa moja tukajua sasa hatushindani na chama cha siasa bali cha kijeshi. Hao waliotuhumiwa kwa rushwa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na aliyetuhumiwa mbali ya kukiri kabla ya kubadili kauli kapandishwa cheo! Sasa hapo unategemea ushindi kwa upinzani? So kutuambia Lowassa ndio sababu ni kama kutuona watoto sana. Hapa tulipo tunawasanifu tu japo mnaona mmeshinda. Simply tumewapuuza maana tunajua awamu hii haiwezi siasa za hoja wala ushindani wa kisiasa. Niendelee ama niache?
 
Wewe ni kiazi kabisa. Kwani na chenge yuko huko unakosema yaani Mungu atusamehe kwa akili hizi za kitanzania tutangoja sana hayo maendeleo na watu watakuwa wanafanya vitu bila sisis wananchi kuhoji. Hivi kuna mtu mwenye milki na Tanzania au ni sisi wananchi wanavyokuja kuomba kura wapole sasa wamegeuka kuwa vichaa kabisa.
 
Katika history tunaambiwa kuwa the colonialists created the seeds of their own destruction..leo tunasema chadema created the seeds of its own destruction..wacha kiendelee kubongonyoka
 
Endelea kusubiri hizo taasisi za kimataifa tu mkuu, lkn mwisho wa siku utaishia kulia lia tu...Mbowe anawaharibia
Mbowe hawezi kuwaharibia kumbuka huyu tunayesema anawaharibia ndiye mwenyekiti pekee anayeonekana ana mikakati ya kisiasa ukitaka kulijua hilo kama unafuatilia Siasa za hapa Tanzania. Hivi ktk vyama vyote vya Siasa ulishawahi kumwona mwana chadema hata asiye na chama lakini anasimamia Itikadi yenye kutoa elimu ya uraia yaani tuseme Mbowe amefanya Tanzania wengi kujua somo la uraia kila mtu ni mbobezi wa mambo. Kwani ni hoja ngapi ngumu nakutana nazo mtaani una kuta mwenye hoja ni mtu asiye na chama kabisa lakini ana hoja ambazo kulijibu ngumu. Hiyo yote ni chadema kimewapa Watanzani udhubutu na kwa njia hiyo uwezi kumwambia Mwanachadema na au siyemwanachama lakini anaishi misimamo yao alafu umwambie Mbowe hafai wakati majibu ya kukujibu ya kukupa juu ya yy kuwepo anao .Mwisho tunaonekana hatuna hoja ni pale anakujibu hivi Mbowe akiwa dhaifu ni faida ya chama gani ni jepesi na kama jibu ndio hilo mwisho tunaonekana hoja zetu ni hoja mfu
 
Kama kuna mtu mwenye akili timamu sasa huko CHADEMA kwa hali ilivyo sasa,basi ajiunge na CCM maana kuendelea kuwepo huko,ni kuifanya ccm iendelee na uovu wake dhidi ya wale wanaohofiwa kuwa wapinzani.Hata hali ya uchumi inavyozidi kuwa ngumu,kuna watanzania wengi wanaamini ni kwa sababu ya upinzani!Waachieni ccm ili hali halisi ijulikane
 
Kama mm ni kiazi wewe utakuwa ni muhogo wenzio wanakupasua katkati
 
Mbowe hajawahi kuijenga CHADEMA.............CHADEMA imejengwa na dr. slaa alipokuwa mbunge na katibu mkuu wa CHADEMA..........
 
Mbowe hajawahi kuijenga CHADEMA.............CHADEMA imejengwa na dr. slaa alipokuwa mbunge na katibu mkuu wa CHADEMA..........
Aliyemwingiza Dr Chadema ni nani zaidi ya Mbowe mku ktk siasa ww ni mpya kwa hiyo hujui ndo maana unakuja na jibu kama hili .Hivi unajua kisa cha Dr kujiunga na upinzani
 
Aliyemwingiza Dr Chadema ni nani zaidi ya Mbowe mku ktk siasa ww ni mpya kwa hiyo hujui ndo maana unakuja na jibu kama hili .Hivi unajua kisa cha Dr kujiunga na upinzani
aliemuingiza dr chadema sio ishu tunaangalia impact yake kwenye chama....Mbowe huyo huyo ndio aliemuingiza Lowasa ......tunajua dr alijiunga chadema baada ya kudhulumiwa kugombea ubunge karatu
 
hahahhahhahhahahhhhh
 
Wape ushauri mwengine simuoni kiongoi wa CDM anaewza kua mwanachama wa JPM, labda wafanye biashara waachane na siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…