Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,516
Nayasema haya bila kupepesa macho wala kutikisa masikio. Nasema na kuamini kuwa kama CHADEMA ikimpokea Edward Lowassa kuwa mwanachama wao,CHADEMA itakuwa inajifuta kwenye ramani za siasa za nchi hii. Sababu nitaieleza hapa chini.

Nguzo imara ya CHADEMA ni mapambano dhidi ya ufisadi. Chama hiki kikuu cha upinzani nchini kimejijenga katika kujitenga na ufisadi. Matendo na maneno mengi ya CHADEMA yamekuwa yakionyesha mapambano dhidi ya ufisadi. Mapambano hayo yamewafanya CHADEMA kujizolea sifa,wanachama na washabiki. Itashangaza kuibomoa nguzo hii iliyojengwa kwa miaka kadhaa.

Kumkaribisha Lowassa utakuwa unafiki na usaliti. Naamini tetesi za Lowassa kutaka kujiunga na CHADEMA zitaendelea kuwa tetesi milele. Ikiwa kweli, CHADEMA watakuwa wanafiki na wasaliti. Watakimbiwa na hawataaminika. Na huo ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA. Wawe makini katika hili. Jamaa ni kielelezo cha wanachopambana nacho.


Ni ukweli uliowazi kuwa wana mageuzi wengi ni wafuasi wa CHADEMA na ni ukweli uliokuwa wazi kwamba ni chadema hii iliyotoa orodha ya mafisadi 11 Tanzania na mh Lowasa akiwa mmojawapo.

Swali ambalo wana mageuzi wanajiuliza ni kwamba kama Ccm imemkataa Lowasa kutokana na uchafu wake iweje awe msafi ndani ya chadema?

Na je Ile tuhuma ya ufisadi imeishia wapi? Na amesafishwaje? Hakika huu utakuwa mwisho wa chadema kwani wana mageuzi wengi sasa watahamia vyama vingine vya upinzani ikiwa ni pamoja na kurudi chama tawala kwani upinzani utakuwa hauna jipya kama ilivyotegemewa!
Kama tunavopata tetesi, Leo Lowassa atatua CDM, Ukirejea misimamo ya CDM dhidi ya ufisadi na watuhumiwa wa ufisadi, utaona jinsi binadamu tulivyo wanafiki.

Binafsi nimekuwa CDM/nimekiunga mkono tangu kuanzishwa kwake, Tumekuwa tukitoa shule kuhusu jinsi nchi inavyomilikiwa na viongozi wachache wa CCM wanaofanya rasilimali zetu kuwa chambo kwa wawekezaji ambao huwapa viongozi hao rushwa.

Kwa bahati nzuri sana moja wa watuhumiwa wa muda mrefu ni huyuhuyu Lowassa. Leo kwa mbwembwe Lowassa atatua CDM!! Aibu kubwa sana - hata kule kukaa kimya tu bila kukanusha kuwa anakuja CDM ni aibu, sembuse kumpokea!!

Kama alivyotumiwa fedha kuteka mfumo wote wa uchaguzi ndani ya CCM, nguvu za fedha zake na marafiki zake sasa zitahamia CDM, - kununua wapiga kura na mfumo wote wa uongozi, ni bahati mbaya sana kwa upinzani ambao kwa sasa upo ktk peak kukubali kurubuniwa kwa ajili ya kupata tu simple popularity.

Ninachosema ni kuwa sasa Upinzani umetekwa kwa fedha lukuki za Lowassa na kwa tamaa ya viongozi wetu tumeingia mkenge.

Upinzani tungeshinda mwaka huu bila Lowassa, lakini kwa kuwa mmeamua kutuletea aibu hii, sikupenda kupiga kampeni lakini kwa hili nawaambia tutaigeuka CDM na kupigia kampeni CCM kwa kuwa kumbe CDM pamoja UKAWA NI WANAFIKI NA MNANUNULIKA!! Heri wazee wa CCM waliokataa fedha na kuweka uzalendo na nchi yetu mbele dhidi ya maslahi ya wachache.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
Nampa pole nyingi mweshimiwa Dr. Slaa kwa kukubali kuuza heshima yako kwa siasa za miezi mitatu na kuvunja heshima uliojijengea Kwa zaidi ya miaka kumi.

Nimejaribu kuwasikiliza chadema Kwa kumkaribisha Lowassa na kubadili maneno kuwa sio fisadi bali ni mfumo wa ccm. Jamani sisi ni watu wazima na tunaelewa mnachotuambia, ulisema mambo mengi sana kuhusu lowassa na tukakuamini na baadhi ya ufisadi wake una ushahidi wa barua leo hii umeamua kuchana ushahidi ukalamba matapishi yako na kukubali kumkaribisha lowassa.

Haya yote hayana maana zaidi ya rushwa, tamaa ya madaraka na undumila kuwili wa viongozi wa kisiasa. Nani asiyefahamu kuwa lowassa alitumia pesa nyingi katika mchakato ccm ili kuwashawishi wajumbe wampigie kura?

Leo hii hakuna mnachoweza kutushawishi wananchi kuhusu lowassa ambaye hata watoto wadogo wanajua ni mtoa rushwa. Hakuna zaidi nachoweza kusema zaidi ya kupokea rushwa ili mmeze matapishi yenu. Ninavyokujua Slaa huwezi kukubali kumpokea lowassa zaidi ya kupewa rushwa ili ukubali.

Kinachoendelea ukawa ni ujinga uliotukuka wa viongozi kupokea rushwa na kuja mbele ya TV kutudanganya wananchi.
Yaani Dr umeshindwa kujua kuwa malengo ya lowassa ni ya muda mfupi je baada ya hapa mtakuwa katika nafasi gani ya kisiasa na kama njama zenu zikifeli?

Kumbuka lowassa amekatwa ccm kwa matendo yake na watu wanayajua wakiamua kuyasema sijui mtaficha wapi nyuso zenu.
Mwisho naomba mungu aendelee kutuonyesha ukweli wa viongozi wetu yuwajue vizuri. Mungu ibariki Tanzania.
Dr.Slaa pengine ndiye mwanasiasa wa upinzani anaeheshimika na kusikilizwa zaidi Tanzania.

Yote hii ni sababu ya misimamo yake kupinga ufisadi, kusimamia na kutetea maslai ya Taifa bila kuogopa.

Amewahi kutaja hadharani listi ya mafisadi 11 Lowasa akiwa namba tisa na Kikwete akiwa namba kumi na moja.

Alienda kule Arumeru alimtuhumu Lowasa waziwazi kwa ufisadi na kukwepesha miradi ya Arumeru na kuipeleka Monduli.

Lakini leo tunaambiwa kuwa Lowasa anakaribishwa ndani ya Chadema na kuungama dhambi na atasamehewa.

Sina tatizo na ujio wa Lowassa ndani ya chama tatizo langu ni heshima na taswira ya Dr. Slaa aliyojijengea kwa muda mrefu kwa kuukemea ufisadi.

Je leo yupo tayari kutangaza hadharani kuwa Lowasa amekuwa msafi sio fisadi tena, yupo tayari kupunguza ile list of shame ya Mwembeyanga kutoka kumi na moja na kubaki kumi.?

Japo siasa hazina adui wa kudumu wala urafiki wa kudumu, kwa hili naona heshima ya Dr.Slaa na Chadema kwa ujumla ikiporomoka.

Maana heshima ya Dr Slaa na Chadema imejengwa kwa kuukemea ufisadi, lakini tunakoelea Hali itabadilika na kuwa Chadema ni chama cha kuwasafisha Mafisadi.

Nb.Ni mtazamo tu wadau msijenge chuki.
Sidhani kama Bw.Lowasa yuko sawa sawa kabisa! Inawezekana hayuko mzima kama tunavyodhania. Ninaposema mzima nazungumzia uzima wa psyche inawezekana kabisa hayuko hapa Duniani na amepoteza kabisa uwezo wa kutambua uhalisia!

Hili siyo jambo geni sema hapa kwetu nyumbani halieleweki sana kwa sababu bado hatujafikia huwo uwezo wa kuwa na wataalamu wa haya mambo kwetu sisi tunatambua ugonjwa pale tu mtu anapoumwa tumbo, kichwa, homa, kukohowa n.k lkn kuna magonjwa mengine yanayohusisha psyche ambayo yanasababishwa na mambo mengi kama Umri, ambapo mgonjwa huwa anapoteza hali ya kutambua uhalisia na anakuwa kwenye Dunia yake tu, hivyo anafanya mambo ambayo anayaona yeye kwenye Dunia yake, rejea ushambuilizi wa kisu kwenye daladala yule mtu alikuwa na mgonjwa na alipoteza uhalisia ktk Dunia yake alikuwa anaona kuna mtu anamshambulia na hivyo akaamua kumshambulia kama kujitetea...

Niliposikia ya kwamba Mke wa Bw.Lowasa kamsihi sana Mume wake asitoke CCM na kuhamia CHADEMA na yeye kukaidi nikatambua ya kwamba kuna kitu kinamsumbua Bw.Lowasa, ni kwamba yuko Dunia nyingine na sasa akina Slaa, Mbowe &Co. siajabu wameshajua hilo na wanachofanya ni kumtumia tu kwani kama kweli yuko sawa psyche ni ngumu sana kufanya maamuzi aliyofanya huku akijua fika yatakayo mkuta!

attachment.php


Mheshimiwa Mbowe nasikia Mh Lowassa amepokelewa UKAWA na kupewa hadhi ya kugombea urais, mimi kama mwanachama wa kawaida wa CHADEMA sikubaliani kabisa na uamuzi mliofanya nyie viongozi bila kutushirikisha wanachama wote wa kupokea makapi toka CCM halafu na kupewa wadhifa mkubwa wa kugombea urasi, inamaana UKAWA kwa ujumla kulikuwa hakuna mtu anayefaa kugombea urais? Mpaka tungoje mtu aliyeshindwa toka CCM ndiyo aje agombee urais UKAWA?

Kuna watu wana miaka 30 wako CHADEMA na wanafaa kugombea urais iweje leo Lowassa wa siku 2 tu teyari mumeshakuwa na imani nae kwa kiasi kikubwa namna hii, je akiwasaliti kama Shibuda mtakuja kutuambia nini sisi wanachama wa kawaida ambao hatuna nguvu zozote?

Mengi Ashery Ngoso
 
Mhhhhhh siasa aipo ivyo wewe watu wanacheza na akili za wengi au umesahau kuna watu waliapa kutembea na wazazi wao kama watarudi chama Fulani baada ya kuondoka na wakarudi bila kujali viapo vyao siasa ni mchezo mchafu tuuh
 
Naunga mkono CDM hawakiwi kabisa hatua kujadili kuwa Lowasa akijiunga na CDM je chama kitaterereka?

Mchango wa Lowasa ni mdogo sana na hafai kabisa hata kuwa mwanachama wa kawaida tu wa CDM. Nasikia eti kikwazo ni Dr. Slaa lakini wengine wamekubali. Kama ni kweli uwezo wa Mbowe utakuwa umefika mwisho.

Juhudi zote za kuruka angani zitangushwa na mtego mdogo sana.
 
Mkuu EL hawezi kutoka CCM! Kwanza akitoka hauziki hata aende chama gani! Na sitegemei kama CDM itafanya kosa la namna hii!

Akivua gamba anavaa gwandwa kwahyo me nashauri aje fasta hata kama ni chenge na wezi wote waje wavae gwanda
Kwani hata waswahili tuna sema kufanya kosa si kosa vibaya ni kurudia kosa,na biblia inasema Mwenye dhambi mmoja akitubu ni Fraha mpaka mbinguni hadi maraika wanafrahia,nakishauri chama changu chadema wawapoke wote bila kujali madhambi yao
 
Mchukueni tuu lowasa maana malengo yenu si kupinga rushwa , ajenda yenu ni uroho wa madaraka
 
Mkuu wala usiwe na wasiwasi, Chadema ni chama makini. Hatuko tayari kula saani moja na wezi wa ccm
 
chukueni ili mshinde kwa kishindo atawasidia japo tunajua mlikuwa nae katika mpago wenu wa rais awe wa kasikazini awamu hii,
 
mbona kwa mahasimu Yanga na simba ,inawezekana.Lengo ni kuitoa ccm madarakani au kuendelea kuwa chama cha upinzani milelee?
 
Back
Top Bottom