Mchungaji Lusekelo awe mkweli, asiikemee CCM yenye kibanzi na kuiacha Chadema yenye boriti

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Kiongozi wa kanisa langu la maombezi Mchungaji Anthony Lusekelo amenukuliwa na gazeti moja litolewalo kila siku akisema ’CCM iwaombe radhi Lowassa na Kingunge’.

Mchungaji huyo amefikia kushauri ama kupendekeza kwamba CCM iwapigie magoti aliyekuwa waziri mkuu wa tisa Edward Lowassa na Mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru ambao walikihama chama hicho mwaka 2015 kutokana na vuguvgu la uchaguzi mkuu.

Kwenye mahojiano yaliyofanyika nyumbani kwake Kawe, jijini Dar es Salaam, Mchungaji Lusekelo alitumia muda mwingi kuelezea jinsi Lowassa na Kingunge walivyomuhimu kwa CCM.

Lusekelo amenukuliwa akisema “unawezaje kumuacha Mzee Kingunge na Lowassa wakaenda vyama vingine? Wale ni asset (mali) ingekuwa mimi ningerudi na kuwapigia magoti. Mzee Kingunge ningemwambia chama kinakuhitaji rudi tukijenge lakini unawaacha tu watu hao”.

Mchunguja Lusekelo aliendelea kudai kuwa CCM imetumia muda mrefu kuwafinyanga viongozi hao kwa hiyo ni hasara kwa kwa chama kuwaacha.

Hapa ndipo Namuona mchungaji Lusekelo kama aina ya mtu asiyeielewa CCM wala siasa, sidhani kama Lusekelo akipewa mtihani wa kueleza chama ni nini kama atafaulu.

Nahisi atafeli kwa sababu haelewi tafsiri halisi ya chama cha siasa. Naona ni vivuri nimsaidie ili siku nyingine asipotoshe wanaomsikilioza kwa kuwa yeye ni mtu maarufu anayesikilizwa na wengi.

Nianze na hoja yake anapoitaka CCM iwaombe radhi Lowassa na mzee Kingunge. Kwanza nimuulize yeye Lusekelo tangu aanze kuwaongoza watu pale kanisa kwake ni waaumini wangapi walioliacha kanisa hilo? Je kuna wakati wowote amabapo Lusekelo alifanya bidii ya kwenda kuwataka radhi na muumini aliyeamua kwa hiari yake kutoendana na kanisa lake?

Lowassa na Kingunge hawakufukuzwa CCM walijiondoa wenyewe kwa hiari yao na kueleza na kueleza sababu zilizowasukuma kujitoa. Je Lusekelo anapoitaka CCM iwaombe radhi anakusudia kuchora picha gani? Anataka ionekane CCM ndiyo iliyomkosea Lowassa na Kingunge au wao ndio walioikosea CCM?

Kwa vyovyote suala la kuomba radhi au kuombwa radhi halipo kwa ababu mtu anajiunga na chama cha siasa kwa hiari yake anao uhuru wa kutoendelea kuwa mwanachama. Kwa ajili hiyo mtu yeyote anapokihama chama ama kujiondoa ndani ya CCM hakosei wala hakusewi kwa kuwa anatumia uhuru wake na haki yake ya kujiunga na chama anachokitaka.

Narudia kusisitiza Kingunge na Lowassa hawakufukuzwa CCM, hakuna mwenye akili timamu anayeweza kwenda kuwapigia magoti na kusema tafadhali rudini CCM inawahitaji, kwa sababu hakuna aliyewafukuza mwenye majuto nao ndani ya CCM anyejiona aliwakosea na kusababisha wahame chama.

Tuje kwenye hoja yake ya kuwapigia magoti na kusema mzee Kingunge rudi chama kinakuhitaji. Nani alimwambia Lusekelo kwamba CCM inayumba baada ya kuondokewa na wanachama hao wawili Kingunge na Lowassa? Kama CCM haijayumba wala haijatetereka ama kudhoofika, Lusekelo anapata wapi mawazo ya hayo ya kutarajia watu na heshima zao kuwapigia magoti mwanachama aliyejiondoa kwenye kwenye chama kwa hiari yake?

Tuje kwenye suala la wawili hao kuwa asset (mali) ndani ya chama, kwanza Lusekelo aelewe kwamba hadi sasa chama kufikia kuitwa hatua ya kuitwa chama maana yake ni mkusanyiko wa wengi wanaoamini katika itikadi na sera za uendeshaji wa chama husika.

Kwa maana hiyo, mwanachama mmoja hawezi kuwa mali ya chama bali chama ndio mali ya wanachama ni viungo ndani ya kitu ikizima kiitwacho chama.

Nimkumbushe kauli ya mzee Kingunge wakati kada maarufu wa CCM enzi hizo aliyetwa Agustine Lyatonga Mrema alipojiondoa CCM na hata pale wabunge 55 waliopigania uanzishwaji serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano, Kingunge alisema mtu mmoja hawezi kuwa maarufu kuliko chama na wala kada hawezi kuwa muhimu chama bali chama ni muhimu kuliko mtu.

Lusekelo anaposema unawezaje kuwaacha mzee Kingunge na Lowassa waende vyama vingine? Nami namuuliza Lusekelo kwani vyama vcingine anavionaje? Ama Lusekelo asione umuhimu wa Kingunge kuwa ndani ya CCM, Je huko aliko chadema haistahili kujengwa kwa kuwa nacho ni chama cha watanzania? Inakuwaje Lusekelo asiuone umuhimu wa Kingunge na Lowassa kuwa ndani ya chadema bali auone umuhimu wao ndani CCM?

Kwa vyovyote Lusekelo bado anasumbuliwa na kasumba ya mfumo wa chama kimoja, nampa elimu ya bure ingawa mimi ni miongoni mwa wafuasi wake kanisani kwake, mfumo wa vyama vingi umehalalishwa kikatiba na utendaji kazi wake unampa mtu uhuru wa sawa na huo uhuru wa wanaohubiri kwenye injili unaomfanya mtu kuacha kanisa au dhehebu au dhehebu lake la zamani alikobatizwa tangu akiwa motto dhehebu linguine.

Lusekelo anaongoza wakristo wengi tu walioacha madhehebu tofauti tofauti na kujiunga naye lakini mbona hatoi mwito kwa yeyote kwenda kuwapigia magoti na kuwasihi warudi kwenye madhebu yao waliyoyaacha.

Lusekelo anaendelea kutoa kauli za ajabu anaposema “mimi ninachojua Lowassa ni Kiongozi mzuri na ana ubinadamu, katika watu ambao mungu alitujaalia viongozi Lowassa yumo, hata uniambie Lowassa mwizi mimi sikubali”.

Lusekelo anongeza madai ya ajabu kwamba huenda CCM wana chuki zao ambazo ndizo zilizochangia Lowassa asiwe Rais. Namfahamisha mchungaji wangu Lusekelo kwamba hata kama CCM wote wangemtaka Lowassa, bado wangetakiwa kuongozwa nan a kanuni kati ya wagombea 38 waliotangaza nia zao na kujaza fomu za kuomba kuteuliwa mgombea urais ilikuwa lazima apatikane mmoja na wengine kuchujwa na kubaki mmoja.

Je kuwachuja wagombea 37 na akabaki mmoja hiyo ni chuki au utaratibu? Ikiwa huo ndio utaratibu mchungaji wangu Lusekelo anatakiwa akubali kwamba hata wangependwa wote wakawa na sifa sawa bado kanuni ingewalazimisha kuwachuja wengine na kubaki na mmoja.

Mchungaji wangu Lusekelo kamati ya maadili ina umuhimu wake sawa na jicho lilivyo na umuhimu wake katika mwili yaani linafanya kazi ya kuona. Akitokea mtu kutaka jicho lisione hataeleweka, ndivyo ilivyotokea kwa watia nia 38 na kamati ya maadili ilichuja majina 33 ikabaki ikabakiza matano, kwanini Lusekelo awaone wagombea wote 32 waliochujwa kihalali ila Lowassa alichujwa kutokana na chuki? Na kwamba hizo chuki ndizo zilizomfanya asiwe Rais, Je watia nia wengine hawakustahili kuwa Rais isipokuwa Lowassa tu?

Lusekelo inampasa akubali kwamba kamati ya maadili ilikuwa na haki ya kumpunguza yeyote na iliongozwa na vigezo vyake halali, moja ya vigezo hivyo ni kamati kutoruhusu nafasi ya urais ipatikane kwa nguvu ya fedha.

Mgombea yeyote aliyebainika ama kuhisiwa kutumia fedha nyingi kufanikisha nia yake ya kuwa Rais alitakiwa kuwekwa kando na hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa CCM kumwngua mtia nia ambaye wengi kati ya wajumbe wa NEC walijianda kumpa kura.

Kwani mwaka 1995 alienguliwa, John Malecela, baadaye kwenye mchujo wa mwisho alichujwa Jakaya Kikwete ingawa aliongoza kwa kura, mara pili ndipo Benjamini Mkapa alipoibuka mshindi.

Kwahiyo suala la chuki halipo bali kilichotokea ni suala la utaratibu kwamba panapokuwa na wagombea wengi lazima wachujwe abakie mmoja, katika kuchujana ndipo kina Lusekelo wameingiza dhana ya CCM kuna chuki wakati CCM hakuna inayempenda wala kumchukia kwa kuwa CCM ni taasisi inayoongozwa kwa kanuni na katiba yake.

La mwisho kwa mchungaji wangu Lusekelo, analaumu kwamba taratibu zilikiukwa lakini anashindwa kubaini kwamba hata huko walikoenda akina Lowassa na Kingunge taratibu na katiba za vyama zilikiukwa ndio maana watu muhimu wakatoka ambao ni Dr. Wilboard Slaa na Prof Lipumba.

Mbona Mchungaji wangu Lusekelo hatoi mwito kwa Chadema kumpigia magoti Dr. Slaa na Cuf Kwa Lipumba warudi? Maana ni asset (mali) na kukosekana kawao upinzani unayumba mno.

Katiba za vyama hivyo zilikiukwa katika kumpokea Lowassa na kumteua kuwa mgombea wao wa urais. Uchaguzi haukufanyika isipokuwa Lowassa aliteuliwa na vinara wachache wa Chadema. Mchungaji wangu Lusekelo awe mkweli asiikemee CCM yenye kibanzi wakati Chadema anayoifagilia ina boriti.
 
Hahahaa,

Lami kapelekewa mzee wa konyagi,sijui kilitumika kigezo gani,ccm bhana,mlidhani lami ingemnyamazisha

Hata kule inakojengwa misikiti na ofisi nasikia ni hatihati, baadhi wanaisusa
 
Mzee wa transfoma, greda duuu.hahaha mambo haya hayawez bora apige injili tu. Asibabie kazi za watu
 
Hahahah Pamoja na Kupewa Rami Bado Anaongea Uchochezi?

Duh.! Naona Mchungaji Nafsi Inamsuta Au Na yeye Kapata Maono Kama Lema?
 
Kiongozi wa dini kuongelea siasa ni kama aliyechukua PHD ya ukemia kujifanya anaujua uchumi na kulazimisha mawazo yake yachukuliwe, lazima atakufelisha ukimfuatisha na usiombe huyo kiongozi awe ana uhusiano na pombe either kwa kuitumia au kwa kuwa na hilo jina ndiyo kabisa atakupoteza.
 
Back
Top Bottom