Nawaamini CHADEMA individuals kuliko kama taasisi

Nawaamini CHADEMA individuals kuliko kama taasisi

kiroka

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2018
Posts
371
Reaction score
1,900
Nikiwaangalia na kuwasikiliza wanachadema mmoja mmoja kama Peter Msigwa, God bless Lema, Sugu Lissu, na vijana wengi wa chama hiki hakika ni wazuri katika kujenga hoja ukitafuta wanaccm waje kushindana na chadema kwenye mdahalo CCM watapoteza asubuhi saana

Lakini kwenye ubora wa taasisi CCM wanawazidi CHADEMA mbali saana hapa ndo napata shida kwa mfano

Tangu kuanzishwa kwa chadema haina jengo lao wenyewe kama ofisi wana wanachama wengi nchi nzima kwann taasisi kubwa kama hii taifa wameshindwa kua kiwanja wameshindwa kujenga kwa miaka mingi je Hawa walioshindwa kujenga ofisi zao kwa kutumia wanachama walio nao je tukiwapa nchi wataweza kujenga madarasa na vituo vya afya kweli?

Matumizi ya pesa, ccm wizi wao upo kwenye rasilimali walizo nazo yaan mwanaccm kujimilikisha uwanja au jengo la chama ni Jambo la kawaida, CHADEMA nao walikua wanapata ruzuku, michango ya wanachama, Misaada mbali na kuuza brand za chama lakini matumizi yake hayako wazi ndo maana kuna kipindi wabunge wa chadema walikua wakilalamika makato kwenye mishahara yao na hawajui pesa inaenda wapi, Mimi kama mwananchi nikiyasikia hayo nashindwa kuiamini taasisi hii kua je siku tukiwapa nchi wataweza kweli kua wasafi kuliko CCM, hapa ni sawa nakua na mke mzinifu (CCM) alafu unataka kumwacha uoe mwingine (CHADEMA) lakini huyu mwingine mpya nae anakashfa ya uzinifu ndo unaona Bora ukumbatie huyu unaemjua zaidi.

Kubadilisha uongozi, tangu 1998 mwenyekiti ni mbowe tu habadiliki kwann, taasisi ina watu wengi kwann tusiwape wanachama wengine nafasi kuonesha uwezo wao CCM kubadilisha uongozi inawasaidia saana maana kila anaekuja anakuja na mtazamo mwingine unaweza ukamchukia mwenyekiti aliepita ukampenda aliepo madarakani, hii ndio huipa CCM uhai na muonekano mpya mbele ya wapiga kura, CHADEMA kama taasisi wanataka katiba ya nchi na moja ya hoja kubwa ni mamlaka ya Rais, tume huru ya uchaguzi na mgawanyo wa madaraka lakini chadema waseme mwisho wa mamlaka ya mwenyekiti wao ni upi je ndani ya chadema kuna uhuru wa kutosha katika suala la democracy, kama nashindwa kuyaona hayo ndani ya chadema nawezaje kuwaamini nikawapa kura yangu waweze kuniongoza tofauti na CCM.

Nidhamu ndani ya chama hivi chama kinawaleaje wanachama wake kama kuna malezi sahihi akina mdee wanapata wapi ujasiri wa kwenda kuapishwa bila ridhaa ya chama chao achana na ester bulaya ana damu ya CCM vipi Halima mdee kuna mwanadada nchi hii mpambanaji kwenye CHADEMA zaidi ya Halima kama Halima ameamua kufanya haya vpi kwa waliobakia CHADEMA bado wanalia Halima kua mbunge haramu lkn bdo Halima hawajatoka bungeni wamelelewaje achana na kukumbatiwa na mfumo wao wenyewe kwanini hawaoni shida kufanya uhaini huu kwenye chama chao.
 
Unakariri maneno unakuja kutapika huku.

Lile jengo la makao makuu ya chama na ofisi ya BAVICHA ni jengo la babaako?
 
Hoja zinajibiwa kwa hoja

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app

Ukisikiliza hizi hadithi za CCM taasisi, utakuta utaasisi wake uko ndani ya madaraka ya urais aliyo nayo mwenyekiti wao, tena ni kwenye kuviamrisha vyombo vya dola. Siku CCM itapoteza nguvu ya dola, itajifia kama vilivyokufa viwanda, maduka ya ushirika, taasisi nyingine za ushirika.
 
Nikiwaangalia na kuwasikiliza wanachadema mmoja mmoja kama Peter Msigwa, God bless Lema, Sugu Lissu, na vijana wengi wa chama hiki hakika ni wazuri katika kujenga hoja ukitafuta wanaccm waje kushindana na chadema kwenye mdahalo ccm watapoteza asubuhi sa.
CCM bana, CCM iko madaraka I miaka 60 mbona haitaki kutoka kupisha wengine
 
Ukisikiliza hizi hadithi za CCM taasisi, utakuta utaasisi wake uko ndani ya madaraka ya urais aliyo nayo mwenyekiti wao, tena ni kwenye kuviamrisha vyombo vya dola. Siku CCM itapoteza nguvu ya dola, itajifia kama vilivyokufa viwanda, maduka ya ushirika, taasisi nyingine za ushirika.
Alafu hiyo ccm taasisi,inanayoongoza nchi, vijana wengi ni jobless kama huyu aliyeandika upuuzi, umeme hakuna maji ni shida, huo utaasisi wa ccm unatusaidia nini
 
Kusema kweli kama Chadema ilivyo vizuri kwa wanachama na ingekuwa vizuri na kitaasisi hakika CCM ingeshaondoka zamani. Yaani Chadema wangekuwa watu wa kujifunza sijui, sasa jamaa kasema jambo la maana kuhusu mapungufu wanambeza ingekuwa CCM wanajitathimini. Lakini siku Chadema ikiwa taasisi lazima itachukuwa nchi.
 
Nikiwaangalia na kuwasikiliza wanachadema mmoja mmoja kama Peter Msigwa, God bless Lema, Sugu Lissu, na vijana wengi wa chama hiki hakika ni wazuri katika kujenga hoja ukitafuta wanaccm waje kushindana na chadema kwenye mdahalo CCM watapoteza asubuhi saana

Lakini kwenye ubora wa taasisi CCM wanawazidi CHADEMA mbali saana hapa ndo napata shida kwa mfano

Tangu kuanzishwa kwa chadema haina jengo lao wenyewe kama ofisi wana wanachama wengi nchi nzima kwann taasisi kubwa kama hii taifa wameshindwa kua kiwanja wameshindwa kujenga kwa miaka mingi je Hawa walioshindwa kujenga ofisi zao kwa kutumia wanachama walio nao je tukiwapa nchi wataweza kujenga madarasa na vituo vya afya kweli?

Matumizi ya pesa, ccm wizi wao upo kwenye rasilimali walizo nazo yaan mwanaccm kujimilikisha uwanja au jengo la chama ni Jambo la kawaida, CHADEMA nao walikua wanapata ruzuku, michango ya wanachama, Misaada mbali na kuuza brand za chama lakini matumizi yake hayako wazi ndo maana kuna kipindi wabunge wa chadema walikua wakilalamika makato kwenye mishahara yao na hawajui pesa inaenda wapi, Mimi kama mwananchi nikiyasikia hayo nashindwa kuiamini taasisi hii kua je siku tukiwapa nchi wataweza kweli kua wasafi kuliko CCM, hapa ni sawa nakua na mke mzinifu (CCM) alafu unataka kumwacha uoe mwingine (CHADEMA) lakini huyu mwingine mpya nae anakashfa ya uzinifu ndo unaona Bora ukumbatie huyu unaemjua zaidi,

Kubadilisha uongozi, tangu 1998 mwenyekiti ni mbowe tu habadiliki kwann, taasisi ina watu wengi kwann tusiwape wanachama wengine nafasi kuonesha uwezo wao CCM kubadilisha uongozi inawasaidia saana maana kila anaekuja anakuja na mtazamo mwingine unaweza ukamchukia mwenyekiti aliepita ukampenda aliepo madarakani, hii ndio huipa CCM uhai na muonekano mpya mbele ya wapiga kura, CHADEMA kama taasisi wanataka katiba ya nchi na moja ya hoja kubwa ni mamlaka ya Rais, tume huru ya uchaguzi na mgawanyo wa madaraka lakini chadema waseme mwisho wa mamlaka ya mwenyekiti wao ni upi je ndani ya chadema kuna uhuru wa kutosha katika suala la democracy, kama nashindwa kuyaona hayo ndani ya chadema nawezaje kuwaamini nikawapa kura yangu waweze kuniongoza tofauti na CCM.

Nidhamu ndani ya chama hivi chama kinawaleaje wanachama wake kama kuna malezi sahihi akina mdee wanapata wapi ujasiri wa kwenda kuapishwa bila ridhaa ya chama chao achana na ester bulaya ana damu ya CCM vipi Halima mdee kuna mwanadada nchi hii mpambanaji kwenye CHAADEMA zaidi ya Halima kama Halima ameamua kufanya haya vpi kwa waliobakia CHADEMA bado wanalia Halima kua mbunge haramu lkn bdo Halima hawajatoka bungeni wamelelewaje achana na kukumbatiwa na mfumo wao wenyewe kwanini hawaoni shida kufanya uhaini huu kwenye chama chao
Ccm wameimarika ni sababu wao wanashika dola so hawawezi kuwa sawa na chadema ccm wameiba mali nyingi za umma na kuzifanya zao mfano viwanja vya mpira vya mikoa vingi wanasema ni mali yao wakati vilijengwa kwa nguvu ya wananchi mfano mzuri ni Nelson Mandela kilichopo mkoani Rukwa kilijengwa na wananchi chini ya usimamizi wa Kiwelo akiwa mkuu wa mkoa
 
Back
Top Bottom