Navumilia mateso ya moyo kwaajili ya mtoto wangu

Yaah alirudi akiwa na hali mbaya sana.. So sikuweza kumwambia aende
Mbona jibu lako halina mashiko kabsa?ungempeleka Mtoto hostapil directly,baada ya matibabu warudi walipotoka&kutuma matumizi!
Kweli wanaume sasa hivi hakuna!
 
Huyo mwanamke achana nae tu. Mtoto utakuwa unamtumia pesa ya matumizi. Huyo akinawiri tena atakuoiga chini. Sasa hivi ana shida ndo maana amekukumbuka.
 
Baada ya pilika zangu za kutafuta mkate wa kila siku nakutana na rafiki yangu wa kike baada ya kunipigia tuonane.

Nakutana nae na moja kati ya ombi lake ni NDOA anahitaji nimuoe maana amechoka mateso na kusimangwa kutoka kwa mama yake.

Baada ya kama wiki mbili nikaridhia ombi lake baada ya kujifikilia sana, niliwaza mengi sana hasa hasa ilikuwa ni umri wangu kusogea na sina hata mtoto mmoja wa kusingiziwa hivyo nikamtuma mshenga kupeleka posa na taratibu za nyingine.

26/12/2014 nikafunga ndoa na binti, maisha yakaendelea na inshort yalikuwa mazuri namshukuru mungu, baada ya mwaka mmoja tukabahatika kupata mtoto mmoja wa kike..

Baada ya miezi mitatu tangu huyu binti ajifungue nikapata kesi moja mbaya sana na kunusulika kwenda jela lakini nilipoteza vitu vingi katika hiyo kesi ikiwemo connection zangu zote za kuingiza mtonyo.

Binti akadai talaka baada ya mazingira kubadilika na mtonyo kupiga chenga katika meza, silaha yangu kujitetea ilikuwa ni mtoto kwamba siwezi kukumpa talaka wakati mtoto wetu ni mdogo sana asubili mtoto akue then ataenda. Binti kaja juu kajaza watu mtaani hawezi kuishi na mimi tena anataka talaka yake aende aanze maisha yake.. Pamoja na watu kumsihi ikashindikana ikabidi nitoe talaka akaenda zake yeye na mtoto
"Tena usijaribu kunipigia simu, mtoto wangu ntalea mwenyewe "

Kauli yake ya mwisho kabla hajaondoka kwangu, pamoja na kumsihi hasiongee maneno mengi sana abakishe akiba ya baadae maana mtoto anahitaji malezi yangu pia kama baba..

Baada ya wiki nikapokea barua ya wito nahitajika serikali ya mtaa, binti anataka Asset tulizochuma hasa hasa vitu vya ndani (Furniture).. Shauri likaisha Baada ya mimi kukubali kumpa kila kitu na mjadala ukafungwa..

Nikajichanganya na maisha ya kuishi gesti baada ya mwezi nikapanga chumba na maisha yakaendelea..,

Baada ya miezi tisa binti karudi na mtoto akiwa katika hali mbaya sana, hakuwa amejipanga na maisha wazazi wake hawakumpa support.. Ananiheshimu sana kwa sasa na sikuona jinsi ya kumwambia aende na ikiwa mtoto bado hajaacha kunyonya..

Naishi nae nikiwa na chuki sana katika moyo bt najitahidi nisimuoneshe wakati mwingine nashindwa kujicontrol.. Nahitaji mtoto wangu akue vyema na apate malezi yangu..

NI VIPI NITAWEZA KUTOA CHUKI NILIYONAYO DHIDI YA HUYU BINTI ILI LENGO LA KULEA MTOTO WANGU LITIMIE?
Tatizo ni pale mwanzo,ww na binti hamkuwa tayari kw maisha ya ndoa kumbe kila MTU alikuwa kutatua shida yake,binti aepukane na masimango na kunyanyasika ww umri umeenda update mtoto na wote mmefanikiwa nia zenu.sasa kk kaa na mwenzako mweleze kila kitu usifiche naye najua atafunguka na pengine akaonyesha majuto kamili,kutambua kosa na kutokurudia pia anaweza kukueza ushawishi ulitoka wapi ukabaki unashaangaa na ukakuta umebaki mweupe kama mwanzo pengine ata yy anawaza aanzie wapi,pia sijui maisha yenu ya ss.
 
Mtot kunyonya sio tatizo pia wale wanaojifungua tu na kufarik na kuwaacha watt wao ilihali bado wadog labd kam bado una mapenz nae huyo mwanamke povuuuu
kwann umeridhia dada aonekane marehem wakt yupo?. na mtoto awe yatima wkt mamake yupo?.. samehe 7x70
 
Mbona jibu lako halina mashiko kabsa?ungempeleka Mtoto hostapil directly,baada ya matibabu warudi walipotoka&kutuma matumizi!
Kweli wanaume sasa hivi hakuna!
Ningeeleza kila kitu humu usingesoma, Ni hivi huyu demu maisha yalimshinda kabisa, baada ya kuzinguana na wazazi wake wakamtimua akawa anaishi maisha ya mtaani na mtoto, na mpaka anafikia hatua ya kunitafuta tena mimi ni baada ya mambo kuwa magumu sana kwa upande wake, hakua tena na sehemu ya kukaa, hakua na kitu cha kumpa mtoto, hakua na chochote bob....
 
  • Thanks
Reactions: Pep
"Najiona dhalili sana, please naomba nikae hapa nilee huyu mtoto sina jinsi sina pa kwenda sina tumaini mtoto akiacha kunyonya ntaondoka niende kuishi maisha yangu" Hii kauli ilikuwa nzito sana kwangu pamoja na umwamba wangu na mikazo niliyonayo bt ilinifanya nijue hali anayopitia ya majuto na kukata tamaa.. So nakaa nae huku nikisubiri mtoto aache kunyonya aondoke bt nakuwa nachuki nae muda wote, so ntaweza kucontrol chuki zangu kwake
matter of time mtoto akiacha nyonyo ataondoka sasa una chuki ya nn
 
Maamuzi yangu ninayo ndio, nimeuliza ntaweza vipi kucontrol hali ya kuwa na chuki nae ili anilelee mtoto wangu, kumbuka anaishi kwangu kwaajili ya malezi ya Mtoto, mtoto akikua kidogo anasepa huyu... Nafikili watu wengi hawajanielewa sijui kwa sababu nimeandika kwa jazba
Hapo hakuna kusepa kuna kurudisha penzi kila la kheri katk penz lenu jipy yaan umekosa maamuz kabis kisigizio mtt ananyonya aaaaah kwa heri hayo ni maamuzi yako binafs
 
kwann umeridhia dada aonekane marehem wakt yupo?. na mtoto awe yatima wkt mamake yupo?.. samehe 7x70
Sas si bora huyo mama ijulikane hayupo kwani wa kwanza atakuwa ni yeye sas inahaja gani mleta maada aishi nae huyo mwanamke kwa chuki sabb uangaliz wa mtot watakuja fanyiana kit mbaya fanya kitu ambach roh yako inapend mtt asiwe kisingizio
 
matter of time mtoto akiacha nyonyo ataondoka sasa una chuki ya nn
Sikuja hapa wewe uniulize kwamba kwanini nakuwa na chuki, na wakati kila kitu nimeeleza katika andiko langu, naweza kucontrol chuki dhidi yake ndo kitu nilichohitaji kutoka kwako...
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Sikuja hapa wewe uniulize kwamba kwanini nakuwa na chuki, na wakati kila kitu nimeeleza katika andiko langu, naweza kucontrol chuki dhidi yake ndo kitu nilichohitaji kutoka kwako...
Sas hayo so maisha maisha yenyew yawap yakuwekean vinyongo mkuu chukua mwanao timua huy mwanamke mtot asiwe chanzo rah ya mtot kupat malez mazur ni ikiwa maelewano kat ya baba na mama yap nyumb ina amani na furah kinyume na hapo unayofanya wew ni maigizo huu ni ukwel mchungu kwa her
 
Pole sana Mkuu najua wanaume wengi tutakushauri umtimue ila usifanye visa kusamehe pia ni adhabu tosha kwa mwenye makosa hasa mahusiano jitahid kjjipanga uanzishe maisha upya kuliko kuwaza kuhusu chuki hizo
 
Sas hayo so maisha maisha yenyew yawap yakuwekean vinyongo mkuu chukua mwanao timua huy mwanamke mtot asiwe chanzo rah ya mtot kupat malez mazur ni ikiwa maelewano kat ya baba na mama yap nyumb ina amani na furah kinyume na hapo unayofanya wew ni maigizo huu ni ukwel mchungu kwa her
Nilikuwa nahitaji mawazo na sio maneno ya kejeli..
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kwa mujibu wa maelezo yako ni kwamba sababu iliyomfanya akuache ndio hiyo hiyo iliyomfanya akurudie, hivyo ikitokea tena umepatwa na matatizo atafanya kama alivyokufanyia mwanzo, hivyo maamuzi yako yanategemea busara yako kwa sababu mtoto ndiye kiunganishi kati yenu.
 
Back
Top Bottom