Navumilia mateso ya moyo kwaajili ya mtoto wangu

One moment

Senior Member
Oct 22, 2016
108
113
Baada ya pilika zangu za kutafuta mkate wa kila siku nakutana na rafiki yangu wa kike baada ya kunipigia tuonane.

Nakutana nae na moja kati ya ombi lake ni NDOA anahitaji nimuoe maana amechoka mateso na kusimangwa kutoka kwa mama yake.

Baada ya kama wiki mbili nikaridhia ombi lake baada ya kujifikilia sana, niliwaza mengi sana hasa hasa ilikuwa ni umri wangu kusogea na sina hata mtoto mmoja wa kusingiziwa hivyo nikamtuma mshenga kupeleka posa na taratibu za nyingine.

26/12/2014 nikafunga ndoa na binti, maisha yakaendelea na inshort yalikuwa mazuri namshukuru Mungu, baada ya mwaka mmoja tukabahatika kupata mtoto mmoja wa kike.

Baada ya miezi mitatu tangu huyu binti ajifungue nikapata kesi moja mbaya sana na kunusurika kwenda jela lakini nilipoteza vitu vingi katika hiyo kesi ikiwemo connection zangu zote za kuingiza mtonyo.

Binti akadai talaka baada ya mazingira kubadilika na mtonyo kupiga chenga katika meza, silaha yangu kujitetea ilikuwa ni mtoto kwamba siwezi kukumpa talaka wakati mtoto wetu ni mdogo sana asubili mtoto akue then ataenda. Binti kaja juu kajaza watu mtaani hawezi kuishi na mimi tena anataka talaka yake aende aanze maisha yake.. Pamoja na watu kumsihi ikashindikana ikabidi nitoe talaka akaenda zake yeye na mtoto "Tena usijaribu kunipigia simu, mtoto wangu ntalea mwenyewe "

Kauli yake ya mwisho kabla hajaondoka kwangu, pamoja na kumsihi asiongee maneno mengi sana abakishe akiba ya baadae maana mtoto anahitaji malezi yangu pia kama baba.

Baada ya wiki nikapokea barua ya wito nahitajika serikali ya mtaa, binti anataka Asset tulizochuma hasa hasa vitu vya ndani (Furniture). Shauri likaisha Baada ya mimi kukubali kumpa kila kitu na mjadala ukafungwa.

Nikajichanganya na maisha ya kuishi gesti baada ya mwezi nikapanga chumba na maisha yakaendelea.

Baada ya miezi tisa binti karudi na mtoto akiwa katika hali mbaya sana, hakuwa amejipanga na maisha wazazi wake hawakumpa support Ananiheshimu sana kwa sasa na sikuona jinsi ya kumwambia aende na ikiwa mtoto bado hajaacha kunyonya.

Naishi nae nikiwa na chuki sana katika moyo but najitahidi nisimuoneshe wakati mwingine nashindwa kujicontrol. Nahitaji mtoto wangu akue vyema na apate malezi yangu.

NI VIPI NITAWEZA KUTOA CHUKI NILIYONAYO DHIDI YA HUYU BINTI ILI LENGO LA KULEA MTOTO WANGU LITIMIE?
 
Huyo hakukupenda ila alipenda maisha uliyokuwa nayo na sasa hivi amerudi kwakua jua limempiga vibaya mno mtaani, kwanza mkapime afya zenu kabla hamjaendelea na ndoa.
Yaah alirudi akiwa na hali mbaya sana.. So sikuweza kumwambia aende
 
Back
Top Bottom