Navumilia kuwa Mtanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Navumilia kuwa Mtanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BIN BOR, Jan 7, 2011.

 1. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zamani nilijivunia kuwa Mtanzania, lakini sasa navumilia kuwa Mtanzania. Kila kukicha, aheri ya jana. Mkombozi wa taifa hili atatoka wapi? Yuko wapi mkombozi.....aliye tayari kusulubiwa kwa ajili ya ukombozi wa watu wake? Wadhalimu wanatamalaki kuanzia ikulu hadi Nangulukulu. Hadi lini tutashindwa kupumua kutokana na kubanwa na viongozi waovu wa taifa hili? Kitabu kitukufu cha nchi hii (katiba) badala ya kuwa safi sasa ni fifi. Ile nyumba takatifu (ikulu) imegeuzwa danguro. Watu matajiri huenda huko kujiburudisha. Mitume (mawaziri) pamoja na bwana wao (mkuu) wamedhamiria kuwa wezi na wanyang'anyi. Nchi imegeuka kama pori la wanyama. Tunaokula nyasi tunaliwa na walao nyama. Hadi lini? Nitashika silaha na kuukabiri uovu huu. Udogo wangu si hoja. Daudi alimuua Goliath kwa kombeo tu. Kila mtu basi na ashike kombeo lake, tupambane na udhalimu huu. Hadi tutakapofanikiwa, nitaendelea kuvumilia kuwa Mtanzania.
   
Loading...