Kama Mtanzania namshauri Spika Ndugai kuwa huu si muda wa vijembe na utani kwa kina Mbowe. Tujibu hoja chafu za awamu iliyopita

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Nimemsikia Spika wetu akibeza baadhi ya viongozi wa Upinzani na wengineo kuwa hawakufanya lolote wakiwa wabunge akiwemo Mh. Mbowe na wengine. Ati Hai sasa ndo imepata Mbunge wa kuisemea!

Nimejiuliza mengi kama Mtanzania kuwa tunataka kujenga nchi ya aina gani? Tutaendelea kuudanganya Ulimwengu hadi lini?

Nafikiri kuna umuhimu wa kupima afya za baadhi ya viongozi wetu.

Siyo siri kuwa Awamu hii ya 6 ya Mama yetu Mh. Samia imeanza vizuri kwa kutaka maridhiano,kutaka mabaya yaliyopita yasijitokeze tena na Watanzania tuwe kitu kimoja. Wote ni mashahidi wa namna Mh. Pombe Magufuli alivyoingiza Madiwani, Wabunge,Wenyeviti wa Vijiji nk kwa sehemu kubwa bila ridhaa ya wananchi. Na Wananchi walijionea wenyeww madudu hayo.

Nahisi,watu aina ya Mh. Ndugai aidha hawafurahishwi na mwelekeo wa Raisi wetu wa sasa,na wanaendelea kutafuta magomvi waliyoyazoea! Watanzania tusikubali, tumuunge mkono Mama yetu ili Nchi yetu ipate maendeleo ya kweli.

Mh. Mbowe juzi ameeleza kwa majonzi makubwa kabisa yaliyomsibu kipindi cha Hayati Pombe Magufuli. Wote tumesikia,na hakuna aliyejibu au kukanusha. Licha ya Mbowe, hata Mh. Spika mwenyewe amekiri hadharani kuwa Mzee alishauriwa na kutenda vibaya japo alipokuwa hai,hakusema hivyo.

Kumlaumu au kumkejeli Mbowe au viongozi wa upinzani huku ukijua wazi hali ngumu ya wanasiasa,wafanyabiashara,watumishi nk waliyopitia kipindi cha awamu ya tano ni unafiki mkubwa.

Mh. Rais na Mama yetu, Mungu akuongoze,upate busara njema za namna ya kutuongoza na Mkono wa Mungu ukuepushe na viongozi wa aina hii,wanaotaka tuendeleze fitina,ubabe, na utengano ili tujenge nchi mpya. Isiyobagua Mpinzani au muunga juhudi, wa ukanda huu au ule, wa dini hii au ile nk.


Nchi ilifika pabaya sana japo wanafiki hawa wanaotaka kujisafisha leo walikuwepo na hawakusema lolote.
 
Ndugai ana vimelea kichwani nilishampuuza! Tuna hasara kuwa na li Supika la hovyo hovyo kama hili! Eti nalo liko kwenye orodha ya viongozi wakuu wa nchi wanaweza kuchukua uongozi lolote likitokea! Mungu apishie mbali!!
 
Mbowe kayasema sasa. Kama TRA wanesingiziwa wajitokeze wakanushe tutawaelewa. Pia Rais SSH alisema kwenye hotuba yake kuwa kuna mwekezaji alifunga biashara zake Tanzania kwa sababu ya kukadiriwa Kodi kubwa na TRA. Hilo mbona hujalikanusha kwa kuuliza kwa nini hakujitokeza wakati huo na kuwaambia Watanzania.
 
Wasalam ndugu zangu, spika wetu ni mbinafsi, mamluki, jeuri, majungu, fitna, kiburi, katili, chuki binafsi, kigeugeu na asiyejua asimamie nini wakatika gani. Tujipe pole miaka5 ya bunge hili ni mingi sana mungu atusaidie.
 
Spika ni mtu anaetakiwa kuwa na weledi, hekima na busara.

Kiongozi kama spika akikosa haya basi chombo anachokiongoza (bunge) huwa dhaifu na legelege.

matokeo yake ni lugha za kejeli, uswahili, na kukosa maadili kwa mhimili mzima.
 
Naona Nyumbu mmeanza kula za uso huku Zitto kawageuka pia Ndugai ni suala la Muda tu mtapoteana hamuwezi kumtukana Hayati mkabaki salama.
 
Back
Top Bottom