Nauza ticket ya ndege Mwanza - Dar.

Majanga tu wajamaneni!
Nimelipa 150,000 na sijafanikiwa kusafiri.
Wamekataa ku cancel trip yangu na hela hawataki kunirudishia, wananiambia kama unataka change flight date halafu itakubidi ulipie fee ya mabadiliko tsh. 40000 plus nauli ya tarehe utakayosafiri.
Kwa mfano tarehe 6.04.2014 watanicharge 40,000+26,000+150,000 jumla tsh 216,000/=

hakika fastjet ni walaghai sana.
 

Mkuu hayo unayosema sio ya kweli..., ukibadilisha tarehe baada ya kununua inategemea umebadilisha lini na bei za hio siku, kwahio utalipa accordingly, kwahio kama siku unayobadilisha kuna vacancy kibao au ni ya mbele sana utaongezea hio elfu arobaini tu.

Mkuu hizi airlines unapata punguzo la bei/bei ndogo sababu unabook in advance kwahio wanajua kabisa siku ambazo ndege huwa haijai (na ni bora upeleke ndege ina watu kwa bei rahisi kuliko kupeleka ndege tupu), kwahio kwenye mahesabu yao wameshapanga kabisa kwamba huwa tuna percent fulani ya vacant seats (ndio hizi watu wanazijazia) ila ukienda late unatoa pesa nyingi tu kama wengine, (usishangae wewe ukatoa elfu 90 umekaa na mtu ametoa Laki na Nusu) kwenye ndege moja.

Kama ingekuwa wanaruhusu cancellations bure huoni kwamba ile advantage yao itakwisha ? Kwahio kama unasafiri siku za karibuni / hauna uhakika wa safari Fast Jet ni expensive ila kama unabook muda mrefu in advance (maybe likizo na familia) Fast Jet is way to go

Kama nilivyomshauri huyo jamaa hapo juu cha maana aonane na mawakala wa ticket wadogo wadogo wanaweza kuwa na wateja wao wakachukua au ajaribu kwenda airport aonane na wajanja wa hapo au hata uliza madreva taksi wa hapo karibu wanaweza wakawa wanajua mtu au wakampatia ufumbuzi (Ila legally hana Case yoyote zaidi ya kuongezea hio pesa kubadilisha tarehe)
 

Mkuu sio kweli wao wakisababisha unaweza ukarudishiwa pesa au ukabadilisha siku bila additional charges
Delays and Cancellations - Plan Your Trip - fastjet

 

Waulize ile elfu 26 ni ya nini unless kama ticket za bei rahisi wamemaliza (muda unaosafiri ni wa karibu sana/siku chache) kwahio ticket zilizobaki za tarehe 6/4/2014 ni za 176,000/= kwahio unaongezea hio 26 kwenye ile uliyoshatoa lakini ungebadilisha tarehe ya mbele zaidi ungeongezea hio 40,000/= peke yake

according to their site

 
Ni wahuni tu nawe utakuwa unashirikiana nao, tiketi ya basi inabadilishwa ijekuwa ya ndege?

Kaka dunia mbona hiko wazi siku hizi, google low cost tickets uone masharti yake, pesa hairudi hata kubadilisha muda wa safari lazima ulipie pesa ya kutosha kulinganisha na Airlines za kawaida. Hata basi za low cost nazo zina masharti tena zaidi ya hayo, kwa mfano unakata ticket ya basi unasema utapandia ubungo, uwezi kupandia kituo kingine chochote ni lazima ni ubungo kwa kuwa ticket yako inasema lazima upandie ubungo hata kama basi utakutana nalo kabla ya ubungo au litakuacha ukalikimbiza inabidi kulipa nauri mpya.

Hivi ni vitu vya kawaida ulimwenguni sema kwa Tanzania ndio wameanza Fast Jet ndio maana watu tunashangaa, Hata mabsi yatakuja ya aina hiyo muda si mrefu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…