Inategemea, hapo mtaani kwako maziwa yana quality gani na huyo anaefanya delivery yana quality ipi.
Nakupa mfano: hapa nilipo kuna jaama anauza lita fresh 2000 ila maziwa yana maji sana. Hivyo nimebadili location, nachukua maziwa yanakuja na daladala litre 5 natulia, maziwa yako vizuri.
Mwanzo nilikuwa nachukua mgando hapa hapa jilani, ila baadaye nikaonja maziwa mgando kutoka kiwanda za magereza, kingolwila morogoro. Oya mtindi umenyooka ule. Nina mwanangu anakuja dar mara kwa mara, huwa namwambia apitie pale.
Kwahiyo kusubiri delivery ni kawaida kwa kitu unachopenda