Ni hatari sana kununua line ya MPESA, TIGOPESA ama hata AIRTELMONEY kwa mtu,kuna rafiki yangu alikuwa hapahapa Dar alinunua line ya TOGPESA kwa mtu then huyo mtu akaondoka zake Mwanza,jamaa kaweka kwenye TOGOPESA hiyo shilingi milioni 3 kwa ajili ya biashara.Kwa taarifa yako jamaa alizikomba zote na jamaa alieuziwa line alivoenda TIGO aliambiwa kuwa hawawezi kushughulikia suala lake maana line haikuwa ya kwake kwa hiyo amtafute huyo mhusika mwenye line wayamalize.Ni mwezi umepita huyo jamaa aliezuza line hapatikani na huku nyuma ameacha majonzi.So in short bora ufaiti kivyako upate line yako mwenyewe ambayo utaisajili kwa jina lako mwenyewe