Mdau
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,789
- 470
Wadau, nawaletea maelezo ya Mtanzania ambaye aliniambia akipata nafasi ya kumuona rais atamueleza yaliyo moyoni mwake...haya ni baadhi ya maelezo...endeleeni
"Mimi ni Mtanzania wa kawaida sana, sijui chochote kuhusu uchumi wala mambo ya kisiasa...maisha yangu ni kama wenzangu wengine wengi, nanunua mahitaji yangu kwa rejareja katika vibanda na magenge ya jirani..
Sasa mheshimiwa rais,naomba basi uniambie au unishawishi ni namna gani naweza kukupigia kura yangu mwaka huu 2010, hasa ukizingatia haya yafuatayo....
*Mfumuko mkubwa wa bei wa bidhaa ambazo ninazihitaji sana kwa matumizi yangu na familia yangu; mfano;
i. Sukari huku kwetu ni Tshs 2200 kwa kilo
ii. Mafuta ya kula kibaba 1 ni Tshs 200 na Lita 1 ni Tshs 1500
iii. Sabuni kipande kimoja kidogo ni Tshs 300
iv. Chumvi pakiti 1 ni Tshs 150-300
v. Unga kilo 1 ni Tshs 800
vi. Mchele ninanunua kwa Tshs 1300 kwa kilo
vii. Maharage ni Tshs 1500 kwa kilo
viii. Mboga za majani fungu moja limefikia Tshs 250
ix. Kiberiti ni Tshs 100
Sasa basi, napata tabu sana kukuelewa au kuwaelewa wenzako wanaponiambia kwamba hali yangu ya maisha imeboreka...kumbuka hapo juu ni mchanganuo wa vitu vichache tu vya msingi, bado mahitaji ya wanangu kwa shule yamepanda bei, kodi ya vyumba vya uani hapa napoishi imepanda pia,huku uchakavu ukiongezeka..wakati mwingine huwa nahisi labda nilizaliwa niteseke, nafikiria hata kujiua kabisa..Sigara ambazo nazitumia kupunguza mawazo nazo bei juu..
Wiki hii mbunge wetu kaja,kuna vijana wake wametugawia elfu kumi kumi,na nilipewa kwa sababu mimi ni maarufu kidogo hapa mtaani..lakini,sidhani kama nitapiga kura, nimepiga mara nyingi sana lakini naona hali inazidi kuwa ngumu..wanangu nawasihi sana wasome, lakini sijui kama watafika huko ambapo mimi nilishindwa, nadhani nitakua nimekufa au nitashindwa kuwalipia..nimechoka sana na hali hii,na mbele naona kiza kinene, kiasi kwamba, naomba niwe mkweli kukwambia kwamba,kitu chochote sasa hivi siogopi kufanya,muhimu niweze hudumia familia yangu..majuzi tuliuza mifuniko miwili ya mtaro wa maji chafu kama vyuma chakavu,ilikua na kutu sana,lakini ilitupatia chochote..mbeleni huwezi jua,ukute tutauza hata watu..."