Habari za leo,wakuu!
Katika kupitia pitia magazeti leo,kuna gazeti moja limemnukuu N/W Ardhi na Maendeleo ya makazi kuwa majengo yote yaliyojengwa karibu na vyanzo vya maji Arusha vibomolewe.Hili jambo lishapigiwa kelele sana na wadau wa mazingira bila kupatiwa suluhisho.
Je,matamshi au maagizo haya ya mh.N/W kuitaka NEMC kufika Arusha ni nguvu ya soda au kuna nini nyuma ya pazia na je,walikuwa wapi (serikali kuu na mamlaka zake kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi taifa) hadi lile jengo kusimama vile pale Sanawari-Arusha ?
Angalizo: Positive discussion na sio siasa wala majungu,ipotezeee,kama hauna la kuchangia.
Nawasilisha
Itabidi wabomoe na Police, Traffic na Fire.
Tatizo la maji Arusha siyo hayo majengo bali ni ukataji wa miti na kilimo kinachofanywa kando kando ya mlima Meru.
Pia kuna kilimo cha salad kinachofanywa katikati ya mto nacho ni noma.
hii hotel mbona cifahamu, iko Dar au
Habari za leo,wakuu!
Katika kupitia pitia magazeti leo,kuna gazeti moja limemnukuu N/W Ardhi na Maendeleo ya makazi kuwa majengo yote yaliyojengwa karibu na vyanzo vya maji Arusha vibomolewe.Hili jambo lishapigiwa kelele sana na wadau wa mazingira bila kupatiwa suluhisho.
Je,matamshi au maagizo haya ya mh.N/W kuitaka NEMC kufika Arusha ni nguvu ya soda au kuna nini nyuma ya pazia na je,walikuwa wapi (serikali kuu na mamlaka zake kuanzia mtaa,kata,wilaya,mkoa hadi taifa) hadi lile jengo kusimama vile pale Sanawari-Arusha ?
Angalizo: Positive discussion na sio siasa wala majungu,ipotezeee,kama hauna la kuchangia.
Nawasilisha
Mkuu yaani N/W amenukuliwa hivyo kuwa hiyo hotel iko kando kando ya mto na akahoji jeuchafu unaotokana na hoteli hiyo hasa maji machafu yanakwenda wapi na akafika mbali kuwa wakzi wa chini yaani huo mto unakotiririka wanakunywa ama kutumia maji yenye uchafuzi.nadhani nimeeleka,hoja ni je ni hii hotel tu au kuna majengo mengine na kwa nini ame base kwenye hoteli tu.au u mgeni kule arusha?New Arusha iko kando ya mto, Equator iko kando ya mto, Mount Maru iko kando ya mto, Diwani Mathias anajenga kando ya mto, Jengo la Benki kuu liko kando ya mto, ofisi za TRA ziko kando ya mto, Ofisi za polisi na trafic mkoa ziko kando ya mto, ......fafanua unachotaka tikijadili
Mkuu ni typing error lakini imeeleweka hata kama ni kando kando ya mto,lile eneo lina chemchem na walipokuwa wanajenga palikuwa panatitia.so in that sense,eneo lile linachangia uwepo wa maji kwenye mto themi,usitoke nje ya mada tafadhali.tuendelee kupata mawazo mbadala,hasa kutoka kwa wana hydrolojia na wapenda mazingiraMtoa mada anashindwa kutofautisha kati ya ujenzi kando ya mto na ujenzi kwenye chanzo cha maji/mto.
Ukumbuke pale pembeni kuna ofisi ya chama ambayo imejengwa kwa msaada wa huyu jamaa wa Naura, na ujenzi ulienda sambamba.Hii hotel wakati inajengwa ujenzi ulisimama kutokana na kelele za wanamazingira! Lakini ghafla ikaja kuota kama uyoga kwa nguvu ya mafisadi,je tutarajie lolote kweli!!sidhani:nono:
Kama wataamuru libomolewe na vibali walitoa wenyewe itabidi walipe thamani ya jengo, gharama zote za kabla na baada pamoja na faida wataoikosa wamiliki kwa miaka itakayowachukua kujenga jengo lingine. Kuna uwezekano kabisa ni mbinu ya kujirudishia mtaji na faida ya haraka.
Nakumbuka majengo marefu ya Oyster-bay, yalibomolewa kwa mbwembwe, jamaa kashinda kesi na amelipwa kitita kuliko yasingebomolewa!
Kila action ina reaction.