Nauona Upinzani Ukiichukua Nchi 2030

Nauona Upinzani Ukiichukua Nchi 2030

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
745
Reaction score
1,470
Habari wanajamvi,

Kwanza kabisa naomba nianze kwa kudeclare my interest. Katika maisha yangu yote sijawahi hata siku moja kujihusisha na siasa kwa namna yoyote ile. Sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, wala sikuwahi kufungamana na itikadi za kisiasa za upande wowote. Mimi si miongoni mwa wale wanaoamini “Oktoba tunatiki” wala wale wanaopigania kauli ya “No Reform, No Election”. Kwa kifupi, I am not interested in politics at all.

Hata hivyo, kwa upande mwingine wa maisha yangu ingawa si mwanasiasa, nimekuwa mfuatiliaji na mdau mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora. Hivyo basi, naandika uzi huu nikiwa kama raia wa kawaida kabisa, asiye na interest na upande wowote wa kiitikadi na chama chochote cha siasa, bali kama mtu anayesimama katika nafasi ya kuamini kwa dhati misingi ya haki, uwajibikaji na uongozi bora.

Sasa turudi katika hoja ya msingi kama ilivyojitokeza kwenye kichwa cha usi huu. Mimi binafsi naamini kwamba kuna uwezekano mkubwa sana wa upinzani kuichukua nchi ifikapo mwaka 2030. Na iwapo hawatafanikiwa kufanya hivyo katika kipindi hicho, basi naamini itawagharimu zaidi ya muongo mmoja tena ili kujiandaa upya na kujiweka katika nafasi ya kushinda.

Kwa mtazamo wangu, zipo sababu mbili kubwa zitakazowapa wapinzani nafasi hiyo ya kipekee: kwanza, sababu za muda mrefu (long-term causes) ambazo msingi wake umejengwa ndani ya kipindi cha miaka kumi iliyopita (2015–2025), na pili, sababu za muda mfupi (short-term causes) ambazo ninatarajia zitaanza kujitokeza mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 hadi kufikia mwaka 2030. Ili kueleweka, nitaanza kwa kuzichambua sababu za muda mrefu kabla ya kuingia katika zile za muda mfupi.​

Long-term Causes (2015–2025)
1. Tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu (7 Septemba 2017)

Tukio la tarehe 7 Septemba 2017, ambapo aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha upinzani CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu, alipigwa risasi zaidi ya mara kumi mchana kweupe na watu wasiojulikana, lilitikisa taifa kwa kiwango cha kipekee. Tukio hili siyo tu kwamba liliwaacha wananchi wengi katika maswali na huzuni, bali pia lilihusishwa moja kwa moja na mazingira ya kisiasa yaliyokuwa yameanza kuonesha dalili za ukandamizaji wa haki za wapinzani.

Kwa mtazamo wa wengi, shambulio lile lilikuwa kiashiria cha hatari ya kuishi katika taifa linaloendelea kufunga milango ya political tolerance. Hata kama mamlaka zilijitahidi kulionyesha tukio lile kama la kawaida, perception ya wananchi ilikuwa tofauti kabisa. Wengi waliamini kwamba kilichotokea kwa Lissu hakikuwa ajali ya kawaida, bali matokeo ya mfumo wa kisiasa ulioanza kukosa uvumilivu kwa sauti za upinzani.

Kwa mantiki hiyo, tukio hili limeendelea kuwa collective memory kwa Watanzania wengi, kumbukumbu ya namna chama kilichopo madarakani kilivyoshindwa kulinda haki za kisiasa za kila raia. Hii imekuwa chachu ya kimfumo (systemic catalyst) inayoweza kupelekea wananchi wengi kuona upinzani kama sehemu pekee ya ukombozi wa kisiasa ifikapo mwaka 2030.

2. Matukio ya kupotea, utekaji na ukamataji kinyume cha sheria

Mbali na tukio la Lissu, katika kipindi cha 2015 hadi 2024 kumekuwa na mlolongo wa matukio ya kupotea kwa watu, vitendo vya utekaji, na ukamataji usiofuata taratibu za kisheria. Matukio haya ni mengi mno na baadhi yamewahi kuripotiwa rasmi, ikiwemo katika taarifa ya wazi ya Tanganyika Law Society (TLS) iliyotolewa tarehe 9 Agosti 2024.

Ripoti hiyo iliweka bayana kuwa kuna idadi kubwa ya raia waliopotea au kushikiliwa kinyume cha sheria bila taratibu za kisheria kufuatwa. Jambo kubwa hapa siyo tu idadi ya waliopotea, bali ni hali ya ukimya wa serikali na vyombo vya usalama katika kuwawajibisha wahusika. Impunity creates resentment, wananchi wanaposhuhudia viongozi wa upinzani, wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu wakipotea bila ufafanuzi, au raia wenzao wakikamatwa kiholela bila mtu yeyote kuwajibishwa, huwa wanahusisha moja kwa moja vitendo hivyo na chama kilichopo madarakani.

SOMA: Orodha ya watu waliopotea na kutekwa na tamko juu ya ongezeko la vitendo vya utekaji na upoteaji wa watu nchini Tanzania

Hali hii imejenga perception kwamba serikali ya chama kilichopo madarakani siyo tu kwamba haioni thamani ya maisha ya raia wake, bali pia ipo tayari kulinda mfumo kandamizi kwa gharama yoyote. Matokeo yake ni kuongezeka kwa hamasa ya wananchi kutafuta mabadiliko ya kisiasa kupitia upinzani.

3. Msimamo wa CHADEMA (“No Reform, No Election”) na kesi ya Tundu Lissu

Msimamo wa CHADEMA wa “No Reform, No Election” ni moja ya hatua muhimu katika historia ya siasa za upinzani nchini. Kauli hiyo ilituma ujumbe thabiti kwamba chama hicho hakina nia ya kushiriki katika mchezo wa kisiasa usio wa haki. Licha ya msimamo huu kuibua mijadala mikubwa, ukweli ni kwamba umeacha alama ya kudumu kwa wananchi: kwamba kuna watu waliothubutu kusimama na kudai mabadiliko ya kimsingi kabla ya kushiriki uchaguzi.

Hali imekuwa ngumu zaidi pale ambapo Tundu Lissu, ambaye ndiye sura kuu ya msimamo huo, alipokamatwa na kukabiliwa na kesi ya uhaini. Kwa macho ya wananchi wengi, hili ni jaribio la wazi la kuua sauti za upinzani. Hivyo, kwa kadiri serikali inavyoendelea kutumia nguvu kubwa kumdhibiti Lissu na CHADEMA, ndivyo inavyozidi kuwajengea upinzani moral high ground mbele ya wananchi. Ni hali kama hii inayoweza kuchochea wananchi wengi zaidi kuchagua upinzani ifikapo mwaka 2030.

4. Ucheleweshwaji wa Katiba Mpya

Mjadala wa Katiba Mpya ni moja ya mijadala iliyodumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya kisiasa ya Tanzania ya karibuni. Tangu mchakato wake ulipoanzishwa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2011, matarajio ya wananchi wengi yamekuwa ni kuona taifa linapata Katiba inayozingatia mazingira ya sasa na kuimarisha demokrasia ya kweli.

Hata hivyo, zaidi ya muongo mmoja umepita bila kupatikana suluhisho la kudumu. Serikali za awamu zilizofuata zimesita kulimaliza suala hili kwa haraka, jambo ambalo limeendelea kuwavunja moyo wananchi wengi na kuongeza hisia kwamba chama tawala hakina dhamira ya dhati ya kufanya mageuzi ya kikatiba.

Ucheleweshwaji huu umechangia mambo mawili muhimu:​
  1. Kuzorotesha imani kwa serikali na chama tawala – kila kadri mchakato unavyocheleweshwa, ndivyo wananchi wengi wanavyohisi kuwa ni “watumwa wa mfumo” ambao haupo tayari kujibadilika kwa manufaa yao.​
  2. Kuimarisha hoja za upinzani – kwa upande mwingine, ucheleweshwaji huu umekuwa karata ya kisiasa kwa wapinzani, ambao mara zote wamekuwa wakitumia kisingizio cha “Katiba Mpya” kama nembo ya kudai mabadiliko. Kila mwaka unaopita bila hatua thabiti, ndivyo madai ya wananchi kwa Katiba Mpya yanavyoongezeka na kuwa silaha ya upinzani kuelekea uchaguzi wa 2030.​
Kwa hiyo, mjadala wa Katiba Mpya una uwezekano mkubwa wa kuchangia hasira kwa wananchi na kuibua matarajio yatayoibeba upinzani ifikapo 2030.

5. Mabadiliko ya Katiba ya CCM

Mabadiliko ya Katiba ya CCM yaliyopitishwa Julai 2025, hususan kipengele kinachowapa mamlaka Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa kuteua wagombea wa ubunge na Baraza la Wawakilishi hata pale ambapo wamepoteza kura za maoni, yameondoa kwa kiasi kikubwa roho ya demokrasia ndani ya chama. Hatua hii imefanya wanachama wengi kuhisi kwamba hawana tena ushawishi halisi katika mchakato wa maamuzi na kujiona kama wao ni watazamaji wa maamuzi yanayofanywa na viongozi wachache badala ya kuwa washiriki hai.

Kwa mtazamo wa kisiasa, ukosefu huu wa intra-party democracy ni silaha kwa upinzani. Mara nyingi, chama tawala kinaposhindwa kudumisha demokrasia ya ndani, wanachama na hata wananchi wa kawaida hupoteza imani, na hatimaye kuanza kutafuta mbadala wa kisiasa. Kwa maneno mengine, CCM inapokosa kuonesha demokrasia ndani yake, inawarahisishia wapinzani hoja kwamba hakitoweza pia kuendesha demokrasia ya kitaifa kwa uhalisia.

6. Kifo cha Hayati JPM na kuingia madarakani kwa Mama

Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Awamu ya Tano, alikuwa kiongozi wa kipekee aliyepata mapenzi makubwa kwa wananchi wa hali ya chini (ambalo ndilo kundi kubwa la watanzania). Kwa wengi, alikuwa rais aliyeonekana kusimama upande wa wananchi dhidi ya mifumo ya kibepari na ukoloni mamboleo. Kifo chake kilileta pengo kubwa la kiuongozi, na pengo hilo halijawahi kuzibwa.

Mama yeye aliingia madarakani kwa mujibu wa Katiba, lakini si kwa kura ya wananchi. Kwa hiyo, kwa mtazamo wa wananchi wengi, kulikuwa na legitimacy gap tangu awali. Aidha, kwa kuzingatia kwamba serikali ya sasa imeonekana kushindwa kulinda maslahi ya wananchi na rasilimali za taifa kwa kiwango alichofanya mtangulizi wake, imani kwa CCM imeporomoka kwa kasi kubwa.

Kwa ufupi, wananchi wamepoteza radha ya chama tawala kama chama kinachoweza kuwaletea maendeleo halisi. Hili limefungua zaidi mlango wa wananchi kuanza kuutazama upinzani kama mbadala wa kweli.

7. Harambee ya tarehe 12 Agosti 2025 (Mlimani City)

Harambee iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City tarehe 12 Agosti 2025 imekuwa moja ya matukio yaliyoacha alama mbaya kwa chama tawala mbele ya macho ya wananchi. Kupatikana kwa zaidi ya shilingi bilioni 80 ndani ya siku mbili, badala ya kuleta pongezi, kumeibua maswali mengi ya msingi: “Kama chama tawala kinaweza kukusanya mabilioni kwa muda mfupi namna hiyo, inashindwa nini kufanikisha miradi ya wananchi bila mikopo na kodi kandamizi?”

Kwa tafsiri ya wananchi wengi, harambee ile ilikuwa kielelezo cha namna chama kinavyoweka kipaumbele katika kubaki madarakani badala ya kuzingatia changamoto halisi zinazowakabili wananchi. Hili limeongeza zaidi mtazamo hasi kwa CCM, na kwa upande mwingine, limekuwa political gift kwa upinzani.

8. Uchaguzi Mkuu wa 2025

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unatarajiwa kuwa moja ya matukio makubwa yatakayoweka msingi wa siasa za Tanzania kwa kipindi kijacho. Hata kama chama tawala (CCM) kitaendelea kushinda kwa kutumia mfumo uliozoeleka wa nguvu kubwa ya dola, mazingira ya uchaguzi huo yataacha alama kubwa kwa wananchi. Kuna mambo mawili makuu hapa:​
  1. Perception ya haki ya uchaguzi: Iwapo wananchi wataona wazi kwamba uchaguzi haukuwa wa huru na wa haki, basi hali ya kutoridhika (dissatisfaction) itakuwa kubwa zaidi. Kila mara wananchi wanapohisi sauti yao inapuuzwa kupitia sanduku la kura, ndivyo hasira ya kisiasa (political resentment) inavyokua.​
  2. Legitimacy deficit: Iwapo CCM itaibuka mshindi bila ushindani wa kweli, pengo la uhalali wa kisiasa (legitimacy gap) litaongezeka. Hii itakuwa ni mwendelezo wa hali iliyoanza baada ya kifo cha JPM, ambapo wananchi wengi walihisi kuwa Mama hakuingia madarakani kwa kura zao moja kwa moja.​
Kwa ujumla, uchaguzi wa 2025 ukiwa na dosari, basi pengo la uhalali wa kisiasa na demokrasia ya kweli litaimarika zaidi na​
kuwa kiashirio kikubwa cha mustakabali wa siasa za Tanzania kwa kipindi chote cha miaka mitano hadi kumi ijayo na

kuwa msingi wa wananchi wengi kuelekeza matumaini yao kwa upinzani kuelekea 2030.

9. Kuibuka kwa wapinzani ndani ya CCM

Mwisho, lakini si kwa umuhimu, ni suala la kuibuka kwa wakosoaji wa wazi kutoka ndani ya CCM yenyewe. Wapo watu waliowahi kushika nafasi kubwa ndani ya chama, kama vile Humphrey Polepole, na hata viongozi wa dini waliokuwa washirika wa chama hicho, kama Askofu Gwajima, ambao sasa wamekuwa wakikosoa chama tawala hadharani.

Hili ni jambo kubwa zaidi ya inavyoweza kuonekana juu juu. Kwa sababu linavunja taswira ya CCM kama chama chenye mshikimano na msimamo mmoja. Wananchi wanapoona kwamba hata watu wa ndani ya CCM wanaona kuna tatizo kubwa, basi huamini kuwa hoja za wapinzani zina msingi wa ukweli.

Kwa maneno mengine, sauti hizi za ndani ni legitimizing voices kwa hoja za upinzani. Na zikitazamwa kwa mtazamo mpana, zinachangia kwa kiasi kikubwa mazingira ya wananchi kuamua kuipa upinzani nafasi ya kuongoza nchi.​

Short-Term Causes (2025–2030)
Baada ya kuangalia kwa undani sababu za muda mrefu ambazo misingi yake imejengwa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita (2015–2025), sasa hebu tuangalie sababu za muda mfupi ambazo naamini zitakuwa na mchango mkubwa katika kuamua hatma ya siasa za Tanzania kuelekea mwaka 2030.

Sababu hizi za muda mfupi zinajengwa juu ya matokeo ya mazingira tuliyoyajadili awali, lakini tofauti yake ni kwamba zitajitokeza kwa nguvu kubwa katika kipindi cha miaka mitano baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Ndiyo kusema, wakati long-term causes zinajenga msingi wa kihistoria, short-term causes ndizo zitakazokuwa “game changers” zitakazoweza kuibadilisha taswira ya kisiasa ndani ya muda mfupi zaidi.

Katika mtazamo wangu, zipo sababu kadhaa ambazo zitaunda upepo wa kisiasa wa miaka ya 2025–2030 na kumweka upinzani katika nafasi nzuri ya kuwania dola mwaka 2030.

1. Kugawanyika kwa CCM baada ya 2025

Ushindi au hata matokeo yanayopingana ya uchaguzi wa 2025 yanaweza kupelekea mgawanyiko wa kisiasa ndani ya CCM. Wengi wanachama wanaweza kukosa kuridhika na mchakato wa uongozi na uteuzi wa wagombea hususani wa ubunge, hali ambayo inaweza kuzalisha migawanyiko ndani ya chama na kupunguza mshikamano wa kisiasa. Mgawanyiko huu unatoa nafasi kwa upinzani kushika nafasi za maamuzi na kuongeza mvuto wake kwa wananchi.

2. Matarajio makubwa kwa Rais Atayeingia madarakani October 2025

Baada ya kuchukua madaraka bila uchaguzi wa haki na demokrasia, wananchi wengi watamshikiria Mama kwa matarajio makubwa ya kuleta mabadiliko chanya kama rais wa kuchaguliwa kwa mara ya kwanza. Ikiwa matarajio haya hayatatimika, au wananchi watashuhudia kupungua kwa uwajibikaji wa kisiasa, hali hii inaweza kuongeza kutoridhika (political dissatisfaction), jambo litakalowezesha upinzani kuchukua nafasi kama chaguo mbadala.

3. Kuendelezwa kwa nguvu ya vijana kwenye siasa

Vijana, ambao ni sehemu kubwa ya idadi ya watu nchini, wanaendelea kuwa na sauti kubwa kupitia elimu, mitandao ya kijamii, na mashirika ya kiraia. Ushiriki wao wa kisiasa unaweza kugeuza msukumo wa kisiasa, na upinzani unaweza kutumia demographic hii kueneza kampeni za kisiasa na kujenga mtandao wa kisiasa wenye nguvu.

4. Ushawishi wa social media na civic awareness

Uwepo wa mitandao ya kijamii, blogs, na vikao vya mtandaoni unaongeza uwazi na uwajibikaji wa viongozi. Hii huwezesha upinzani kufikia wananchi wengi, kueneza ujumbe wa mabadiliko, na kushawishi mitazamo ya wananchi, hususan wale wanaoshiriki siasa kwa njia ya kidijitali.

5. Maandamano na kesi za kisiasa

Baada ya uchaguzi wa 2025, kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa maandamano ya kisiasa, migogoro, na kesi za kisiasa zinazohusiana na matokeo ya uchaguzi. Hali hii itakuwa ni short-term cause kubwa, kwani inaweza kupelekea CCM kupoteza imani ya wananchi na kutoa nafasi kwa upinzani kushika nguvu kisiasa.

6. Hali duni za kiuchumi za wananchi

Hali ya maisha, ongezeko la gharama za maisha, ukosefu wa ajira, na kushindwa kwa baadhi ya miradi ya serikali, vitakuwa ni vichocheo vya kisiasa. Wananchi wengi watatafuta alternative inayoahidi suluhisho za kiuchumi, jambo litakaloimarisha mvuto wa upinzani.

7. Mikopo na ufadhili wa serikali

Hali ya kutokuwa na uwiano kati ya mapato ya serikali, mikopo, na bajeti zinazoenda kwa miradi ya wananchi inaweza kuibua hasira. Kwa mfano, ongezeko la kodi kandamizi kama “mawinga kulipia kodi” kunaweza kuongeza perception ya wananchi kwamba chama kinajali zaidi rasilimali za chama kuliko mahitaji ya wananchi.

8. Uzorotaji wa miundombinu na miradi ya serikali

Uzorotaji wa miundombinu muhimu na miradi ya maendeleo unaonekana wazi katika baadhi ya maeneo (mfano barabara za mwendokasi). Wananchi wanaposhuhudia matatizo haya bila uwajibikaji wa viongozi, hujenga perception ya udhaifu wa chama tawala, jambo linalopelekea wananchi kutafuta upinzani kama mbadala wa kisiasa.

9. Mafisadi, rushwa na matumizi mabaya ya ofisi

Hili linaweza kuwa moja ya matokeo ya Harambee ya Mlimani City, na kuenea kwa ufisadi, rushwa, na matumizi mabaya ya ofisi za umma huongeza chuki ya wananchi dhidi ya CCM. Hii ni short-term cause muhimu, kwani kila tukio la ufisadi linaloashiria ukosefu wa nidhamu na uwajibikaji linaweza kuimarisha hoja za upinzani.

10. Kutokuwepo kwa nidhamu na uwajibikaji katika ofisi za umma

Kukithiri kwa ukosefu wa nidhamu, uwajibikaji mdogo, na mashughuli yasiyo ya uwazi katika ofisi za serikali huongeza perception ya wananchi kwamba chama tawala hakitoweza kudumisha utawala bora. Hii inatoa nafasi kwa upinzani kushika nafasi ya uongozi kama chaguo la kweli la mabadiliko.

Kwa kuhitimisha, ningependa kusisitiza jambo moja la msingi, hoja zote tulizozichambua kuanzia zile za muda mrefu (2015–2025) hadi zile za muda mfupi (2025–2030) zinabaki kuwa dalili tosha kwamba siasa za Tanzania zinaelekea katika kipindi kipya cha mabadiliko. Mabadiliko haya si lazima yawe ya ghafla, bali yanaweza kuwa ya taratibu, yakichochewa na hasira za wananchi, matarajio yaliyovunjika, nguvu za vijana, na maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano.

Hata hivyo, kama nilivyosema mwanzoni, mimi binafsi si mwanasiasa, wala sina dhamira ya kuwapigia debe vyama vya siasa. Nimeandika kwa jicho la mfuatiliaji wa haki, uwajibikaji na utawala bora. Lengo langu ni kuonesha kwamba kuna trajectory inayoonekana wazi, kwamba kadri chama tawala kinavyoshindwa kujirekebisha na kukabiliana na changamoto za ndani na za wananchi, ndivyo nafasi ya upinzani inavyozidi kuwa kubwa kuelekea mwaka 2030.

Lakini, ukweli mwingine usiopingika ni kwamba fursa hii ya upinzani siyo “cheque wazi” yenye mafanikio ya uhakika. Ni lazima wapinzani wenyewe waoneshe umakini, mshikamano, na uthubutu wa kujipanga ipasavyo. Wakiibuka na migawanyiko, kutoweka na ajenda zinazogusa maisha ya wananchi, au kushindwa kutumia vizuri sauti ya vijana na nguvu ya mitandao ya kijamii, basi ndoto ya 2030 inaweza kusalia kuwa hadithi ya kufikirika tu.

Kwa hiyo, uzi huu siyo bashiri ya kisiasa, bali ni uchambuzi wa mwenendo. Kila kinachotajwa hapa ni kielelezo cha ishara tunazoziona leo: tukio la Tundu Lissu, kupotea kwa watu, ucheleweshwaji wa Katiba Mpya, kifo cha JPM, Harambee ya Mlimani City, uchaguzi wa 2025, na hatimaye nguvu ya vijana na social media. Vyote vinaunda taswira kwamba Tanzania ipo katika njia panda.

Swali kubwa linalobaki ni moja: je, Watanzania tuko tayari kutumia uzoefu huu kama daraja la kuingia kwenye enzi mpya ya kisiasa, au tutaendelea kurudia historia ile ile?Kwa nionavyo mimi, majibu hayapo mikononi mwa chama tawala wala upinzani peke yake, bali yapo mikononi mwa wananchi.​

Mi naishia hapa kwa leo✍️
 
umesogeza mwaka au unatengeneza kutetea imani yako kuwa mwenye iani yako ni ndugu yako
 
CCM ina mbinu kama 50 kidogo za kuendelea kula keki ya taifa wenyewe...
 
Inawezekana, lakini haitodumu milele🙃.
Mkuu upinzani hauwezi kuingia ikulu kwakuwa wapinzani hawana mipango ya short term and long-term

Mfano Chadema wangekuwa wanapigania katika mpya tangu 1992 unafikiri mpaka Leo wangekuwa hawajipata .

Labda kiundwe chama kipya chenye watu wenye weledi.
 
Kwa hiyo upinzani usikate tamaa.akitoka raisi mwanamke upinzani utachukua nchi.mkeka WA sheh yahaya bado haujachanika.wasiwe na para.
 
Ccm 2030 inaanguka .
Jana nilikuwepo kawe kwa nilichokishuhudia upinzani kuchukua nchi bado sana na jana ndio niliamini maneno ya Bashiru ukiwa na dola halafu ushindwe uchaguzi utakuwa ni ufwala
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Sasa kwa nini chama ambacho kina wanachama wengi kinaogopa reforms
Jana nilikuwepo kawe kwa nilichokishuhudia upinzani kuchukua nchi bado sana na jana ndio niliamini maneno ya Bashiru ukiwa na dola halafu ushindwe uchaguzi utakuwa ni ufwal
 
Jana nilikuwepo kawe kwa nilichokishuhudia upinzani kuchukua nchi bado sana na jana ndio niliamini maneno ya Bashiru ukiwa na dola halafu ushindwe uchaguzi utakuwa ni ufwala
Kuwa na idadi kubwa ya watu aimaanishi wote wanakubaliana na chama.
 
Hakuna Nafasi ya SS kuendelea na tukabaki wamoja kama taifa,

HATOGOMBEA
 
Mkuu upinzani hauwezi kuingia ikulu kwakuwa wapinzani hawana mipango ya short term and long-term

Mfano Chadema wangekuwa wanapigania katika mpya tangu 1992 unafikiri mpaka Leo wangekuwa hawajipata .

Labda kiundwe chama kipya chenye watu wenye weledi.
Ni pale vyombo vya dola vitakapojitenga na chama Tawala ndiyo tutashuhudia mageuzi ya muda mfupi. Hakuna kingine.
 
Back
Top Bottom