PreGE2025 Naunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika

PreGE2025 Naunga mkono msimamo wa Katibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
650
Reaction score
1,374
Kwenda kusaini kitu kinachoitwa Maadili ya uchaguzi bila kufanyika kwanza reforms ni sawa kabisa na kusaini hati ya kifo chako wewe mwenyewe.

Mimi niwaombe sana ndugu zangu wapigania uhuru wa Nchi hii, CHADEMA, kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa, ebu tuwaachie watawala waendelee kuchaguana wao wenyewe na kuendelea kutawala kimabavu.

Pia soma > John Mnyika: Katibu Mkuu CHADEMA sitakuwepo kwenye kikao cha tarehe 12 Aprili 2025 cha kushauriana na kusaini maadili ya uchaguzi ya 2025

Tuwaachie uchaguzi wote wafanye wao wenyewe. Siku hasira ya Mungu itakapokaa juu yao watakuja kutupigia magoti na kuomba suluhu ifanyike. Mimi naamini hakuna linaloshindikana chini ya jua.

Udhalimu huwa haudumu sana. Kwa hiyo, naomba tusishawishike kwenda kusaini hiyo kitu.

Angalizo: Hapa wanaweza kutafutwa mamluki wakaenda kusaini na hatimaye wakapatikana mamluki wengine wakagombea kwa jina la chama ili tu kuhalalisha uchaguzi.

Narudia tena, tuwaache waendelee na uchaguzi wao, hawa hawana nia njema na Taifa hili.
 
CHADEMA simamieni kile mnachokiamini. Wananchi walio wengi na wenye akili timamu, wanawaunga mkono kwenye hii safari. Na ushahidi mmeuona kwenye mikutano yenu ya hadhara mliyoitisha kote nchini.
 
Wakisign hicho Hati ninawaona kama wapumbavu sana.
Kwani bila wao kushiriki uchaguzi wapenzi wa CHADEMA wataishi maisha yenye furahaa na amani kuliko kwenda kugombana ili tu uwatumikie wananchi.

Yaani ccm wao wanaona rahaa kutangwa mtu ambaye hakuchaguliwa na wananchi, sasa maana ya uchaguzi ni nini? Kitongoji changu uchaguzi wa serikali za mitaa alitangazwa Mgombea wa Chadema kama mshindi jioni...ila usiku wa manane akatangwa wa ccm ndiye mshindi wa CHADEMA akafutwa.

CHADEMA chondechode msishiriki uchaguzi...Dr. Magufuli alisema kuwa wapinzani wanachelewesha maendeleo, badala ya kusema bunge linachelewesha maendeleo ili pesa ya kulipa watu posho bila kazi aekeleze kwenye maendeleo.
 
Sasa njia nyeupeeee kwenda ikulu,bungeni na Baraza la Madiwani, CCM hureee!!!
 
Back
Top Bottom