The secretary
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 4,148
- 2,542
Siungi mkono hoja, tutafute namna nyingine ya kuwaadabisha hao viongozi na sio hii ambayo raia wa kawaida ndio wanaumia.
Siungi mkono hoja, tutafute namna nyingine ya kuwaadabisha hao viongozi na sio hii ambayo raia wa kawaida ndio wanaumia.
Siungi mkono hoja, tutafute namna nyingine ya kuwaadabisha hao viongozi na sio hii ambayo raia wa kawaida ndio wanaumia.
hebu suggest an altetnative method which you think is betterSiungi mkono hoja, tutafute namna nyingine ya kuwaadabisha hao viongozi na sio hii ambayo raia wa kawaida ndio wanaumia.
Muhimbili yenyewe iko juu ya mawe, haina kitu - si madawa ya dharura, mashine za kuuwa wadudu kwenye vifaa, oksijen etc, ukipelekwa Muhimbili ukapona ni Mungu wanko na sio hao madaktari makarani wanaoishia kuandika yaliyokusibu ilihali hawana vifaa vya kukuhudumia. Hapo ni hospital ya taifa, je hali ikoje huko mikoani, wilayani ambapo 95% ya ajali za TZ ndiko zinakotokea? Hata nyuzi za kukushonea huo mshipa unaomwaga damu hawana! Tafakari!Unajua ili ufanye maamuzi sahihi inabidi uwe na taarifa sahihi. Naomba kumwuliza mleta mada, asume kesho aubuhi unapata Ajali mbaya (Mungu epushia Mbali) unavuja damu kwa wingi, tumekubeba kwenye machela mbio Muhimbili, tunakuta Madokta wamegoma anakuja Mwandishi anakuhoji, Je utaunga mkono Hoja?
'Usiombe kukutwa na huu Mgomo'. Hauwawajibishi viongozi bali wananchi wa kawaida.
Mungu epushia mbali huu Mgomo. Amina.
Watanzania tumezoea kutowawajibisha viongozi mtu anavulunda anajua miaka mitano ikifika anachapa lapa huu mtindo waliohuanzisha madaktari wa kuwawajibisha utaleta mabadiliko badala tusisubiri hiyo miaka mitano hii ni kwa manufaa yetu
Kuunga mkono mgomo wa madaktari; mtanisamehe kwa tafsiri yangu, ni sawa na Ugaidi, Ukaburu, Ush***zi, Use**ge wa kupindukia!!!! Wanaoathirika na mgomo huu siyo akina Pinda, Mponda, Nkya, Kikwete, Slaa, Mbowe, Lipumba, Seif,Magufuli, Mwakyembe, Rizi-1, wala wengineo wa tabaka hilo... endapo kama ule mgomo uliopita ungewagusa wangekuwa wamesalimu amri...lakini wanajua hata kama ma-dr wakigoma kwa miaka yote-5 mfululizo, hawataathirika hata kidogo...sisi walalahoi tu ndio tunaathirika... Ni bora MAANDAMANO mara elfu moja huwa wanayaogopa, pia hayawaui walalahoi kwa wingi kama mgomo wa ma-dr. SIUNGI MKONO KABISA MGOMO WA MA-DR.
Mazungumzo gani unaona yanaweza fanyika ukapatikana muafaka? bora madaktari wagome tena kazeni buti haswaaa mpaka kieleweke.Aisifuye mvua imemnyeshea. Siungi mkono hoja. Ndugu yetu amepoteza mtt wake kwa ajili ya huo mgomo. Mazungumzo yafanyike sio mgomo.