Naundiwa zengwe nipewe mke kwa nguvu.

Nimekuwa nikisikia mijadala pembeni kwa watu, mtaani wanahoji mbona sioi wakati mimi ni afsa serikalini na umri umeenda? wengine wanaenda mbali zaidi na kunichunguza napendelea mwanamke wa aina gani, leo kwa masikio yangu nikiwa nimejibanza kwenye kona nimemsikia jirani yangu wa kike akiongea na mwenzake, eti wanaambiana kwa nini tusimtafutie mbinu tumpe mke ukizingatia mtu mwenyewe ana bodaboda 2 na amejenga nyumba ya chumba na sebure? kwa kweli kwa uwezo huo mtaani kwetu wewe ni mtu wa kuheshimika, wanasema ikibidi hata kwa waganga waende tu, mmoja anakoleza kwa kusema tumechoka, sasa wamechoka vipi wakati hayawahusu. Sijui cha kufanya, napanga niwavae kuwaambia nimewasikia na waendelee na mpango wao ili kuwatisha.
Nahisi kama ni aina ya tangazo hivi ili mabinti wachangamkie fursa
 
Aisee una boda boda mbili na umejenga nyumba ya chumba na sebule then uoe siku ukiwa na ghorofa na ka vitz si watataka uwaoe wote sasa
 
Wamechoka kukaa kitaa bila kutongozwa na mabwana hawapo wakati bwana la ukweli upo!! Hehee Upo hapo!!
 
Apataye mke apata kitu chema....

Kumbuka, inasema "apatae".
Jamaa bado anatafuta sasa hajapata.
Kwa hiyo kitu Chema bado hakijapatikana. Naona jamaa wana njama za kumbambikia kitu chao chema kwa mujibu wao.
 
teh teh.... mbAvU zAnGu mie.... mChAkaTo wa KaTiba mPya na uOe.... hAdi waDaDa waKuunDiE tUme nDo uelEwE uNAtAkIwA kuPAta mwenzi...!!! eTi nAomBeni UsHauRi..!! kHaaaaaa....!!!!
 
Je huko 'kijijini' unakoishi kuna sera ya kuoa/kuolewa??? Je wewe ni 'mgumu' sana???? Nahisi wanakutakia mema, wamekosa njia mbadala ya kukuambia.
Ili kukwepa adha, tangaza uchumba kwa kuweka matangazo kila kona ya mtaa.
 
Sasa waite wote anza kugegeda mmoja! Mmoja! Kabla hawajakuletea kitu cha uongo!. Anza anae jifanya anachonga sana leo leo!
 
ushasema umri umeenda, unachoogopa mtu mzima wewe nikitu gn?acha woga wa maisha, km umeshindwa kutafuta mwenyewe ngoja wakutafutie sasa.
 
Mkuu JEKI, wewe ni rafiki yangu mkubwa, naomba nikushauri kitu.

Kama kweli unataka ufanikiwe kuliepuka hilo janga (ofcourse kuoa si lazima),

naomba ujiundie tume binafsi ya mpango mkakati (strategic planning!)

watumie majirani zako hao hao wanaokusema, wape info kwamba unataka kuoa lakini baada ya miaka mitatu hivi (long distance hiyo ujue), wape moyo na maneno yenye asali, wanunulie vibia viwili vitatu hivi siki moja!

Nakwambia urafiki utashika mpaka ushangae mwenyewe!

Usnitch utaishia hapo! Ukijifanya mgumu, utarogwa kweli JEKI. Ohoo!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom