Naumwa visigino. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naumwa visigino.

Discussion in 'JF Doctor' started by God bell, Oct 25, 2011.

 1. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 573
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana jf nina tatizo la visigino, nikisimama kwa mda mrefu vinaniuma sana. Lakini nikiwa natembea hata km ni safari ndefu haviumi shida ni pale tu ninaposimama mda mrefu. Naombeni ushauri kwani ni mwaka wa 3 sasa naumwa. Asanteni.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,002
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  Dawa ni nyingi kwa kweli lakini Inshallah nitaziandika hizi 4 ambazo ni common tu:

  (1) Pika kuzu-bara kwa lugha ya kiingereza inaitwa (coriander) pamoja na hinna na sikikwa kiingereza inaitwa (Vinegar)pamoja na unga wa shairi ni (unga wa ngano)kisha uweke au upake pale penye maumivu.

  (2) Ukipika sarjal kwa lugha ya kiingereza inaitwa (quince) pamoja na maji ya shairi (ngano) ikisha upake panopo uma hupoza maumivu.

  (3) Asali safi ya nyuki ukinywa pamoja na mafuta ya habbati Sauda kwa kiingereza inaitwa (Nigella Sativa oil) huondosha maumivu ya viungo.

  (4) Ukisaga kuzu-bara Kwa kiingereza inaitwa (Coariander) au maji yake pamoja na maji ya busanji kwa kiingereza inaitwa (violet) na lozi kwa kiingereza inaitwa (Almond ) kisha paka katika viungo vinavyouma. Inshallah maumivu yataondoka.
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,017
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  This is the culprit.
  [​IMG][​IMG][​IMG]
  Treatment
  local steroid injection such as Diprofos [SUP]TM[/SUP]
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,982
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Anza mazoezi ya kusimamia kucha au vidole, unatumia njia mbadala
   
 5. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,015
  Likes Received: 341
  Trophy Points: 180
  duuh Hii nayo!
   
 6. God bell

  God bell JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2011
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 573
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana Mzizi Mkavu kwa ushauri wako mzuri. Naomba kujua hiz dawa nitazipataje? Zinauzwa dukani? Asante mkuu.
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,002
  Likes Received: 3,609
  Trophy Points: 280
  Wewe Nenda katika Maduka ya Kariakoo Mtaa wa pemba kwenye Maduka ya madawa za kiarabu,au kama una jirani yako muarabu muulize atakufahamisha wapi inapatikana mimi sipo bongo miaka mingi tena ningelikuwepo ningeweza kukusaidia wapi inapatikana.
   
Loading...