Naumia sana ninaposikia kuna upigaji wa fedha za umma

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,147
7,721
Juzi nikiwa naangalia taarifa ya habari usiku saa mbili, nilimuona Makamu wa Rais akiwa katika ziara mkoani Mwanza, nadhani alikuwa anafungua Hospitali ya Igala kama sijakosea.

Katika ufunguzi huo alibaini ubadhirifu wa fedha za umma katika ujenzi huo na kumtaka Waziri wa Afya kuunda tume na kufanya uchunguzi.

Huwa najiuliza inakuwaje ubadhirifu/ufujaji/wizi wa fedha za umma unatokea kwenye eneo hilo wakati kuna viongozi wa eneo hilo?

Lakini pia huwa najiuliza, hivi hadi leo hii bado tunawatumishi wezi wa fedha za umma? Tatizo nini? Kama ni ukosefu wa maadili fukuzeni, wafilisiwe. Haiwezekani kila mara tunasikia ubadhirifu wa fedha za umma.

Mapendekezo
~ Ofisi ya CAG iwe inafuatilia na kuchunguza thamani ya fedha kwenye kila mradi wa serikali au unaofadhiliwa na wafadhili, na ikibainika kuna ubadhirifu basi wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.

~ Ofisi ya CAG iongezewe watendaji wadilifu na weledi.

~ Itungwe sheria maalumu ya kuwashughulikia wezi/wabadhirifu wa fedha za umma.
 
Tatizo samaki mmoja akishaoza, na wengine huoza pia...

Kila mtu anatafuta mwanya wa kupiga, hata hao unaoona wanakemea wapigaji hata wao huenda wanapiga mahali usipopajua...

Kwanza kitendo cha hao wakubwa kununuliwa migari ya thamani, kulipwa vizuri na kuhudumiwa kama wafalme huo tu ni upigaji kwa taifa ambalo zaidi ya 50% ya wananchi wake wanaishi chini ya 1$ per day...
 
Ukipewa buyu lako la asali lazima utayasahau hayo maumivu

images (8).jpeg
 
Hakuna kesi hapo wala hao wasimamizi hawawezi kuchukuliwa hatua kwasababu pesa wanakula wote hali mtu mmoja wazee wa 10% ndo sehemu zao hizo za kujidai ukikataa kutoa miradi mingine utaisikia tu redioni.
 
Back
Top Bottom