Kuna msema wa kiswahili usemao, ukitaka kukata kuumaliza mti basi ng'oa mizizi yake maana, ukikata matawi tu, mvua ikinyesha huchipua na mti ukawa mbichi kuliko hapo awali.
kwa akili ya harakaharaka utafikiri huu msemo unahusu miti, lakini kiukweli unatuhusu sisi wanadamu na shughuli zetu na kwasasa unamuhusu mh Raisi aliyejipa jina la mtumbua majipu.
Kwanza nianze kwa kusema binafsi kama mtanzania ambaye kipindi cha kampeni walinipigia hadi Push-Ups ili niwape ridhaa, ninayo haki ya msingi kabisa kuwakosoa wanaponidanganya na pale ninapoona usanii, japo wengi hawapendi sana hili, wanapenda kukosoa lakini kukosolewa hawako tayari. Sasa wote ni viumbe Muamuzi ni Mungu kama unavyopenda kukosoa penda na kukosoloewa pia ili pua ikirudi aridhini inapotazama uweze kupata thawabu.
Baada ya hayo niingie kwenye mada, kwanza nakataa kwamba mh Raisi anatumbua majipu, nakubali kwamba hadi sasa anatumbua chunusi na hilo akilifikiria vizuri atakubaliana na mimi..... hebu tuanzie hapa;,
Juzi tu Mtendaji mmoja wa bandari alitumiwa memo na mmoja wa mawaziri afungue Koki iliyofungwa kwa miaka mitano kisa waziri mkuu anaenda! nauliza swali je yule waziri aliyetuma memo hata tu kuhojiwa amehojiwa? na kama alihojiwa ilikua wapi? maana mambo yote yaendayo vibaya mh Raisi na Waziri mkuun huyatatulia hadharani kwenye runinga (huitwa kutumbua jipu).
Kuna nyimbo zenye tenzi nzuri sana tuliimbiwa kwamba Lowasa ni Richmond na akaitwa fisadi papa na tukaambiwa hata kama akiwaambia elimu,elimu,elimu msimkubali maana ni mwizi wa kutisha! je hili Mh unatuambia nini watanzania kwa sasa?
Kuna jipu Linaitwa Mfumko wa bei, mtanzania wa kipato cha chini ni dhahiri kabisa kwamba hata kama tar 25/10/2015 alikua anakula milo miwili saivi haiwezekani tena, kila unachogusa unakiacha ulipokikuta hakifai kubeba, je hili jipu Mh linatumbuliwa lini?
Majizi, Mafisadi, yalinununa mabehewa feki kwa kodi za mlala hoi wala nchi hauikunufaika! je hili jipu nalo linatumbuliwa lini?
Jipu la ubabe wa kisiasa pale ambapo anayetawala hutumia nguvu nyingi na jeuri hadharani kumminya yule asiyekua na dola je hili nalo Mh lini linatumbuliwa?
Je kuhusu Escrow watanzania tuseme ndo imeisha isha je?
Mimi ni mtanzania wa kawaida sana haya mambo najiuliza na yananiuma, najiuliza kwasababu siko tayari kuwa kati ya wale waliotwa kichwa cha mwendawazimu. kila waonacho na waambiwacho husema ndio mzee hata kama kina wazamisha.
Nina mengi ya moyoni lakini hebu walau nipate ufahamu wa haya machache