Nauli za kivuko kigamboni zapanda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nauli za kivuko kigamboni zapanda

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIZAKINENE, Dec 31, 2011.

 1. K

  KIZAKINENE Member

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  watanzania wenzangu hasa wale tuanoishi kigamboni ni wakati mwingine tena wa kupata machungu ya ugumu wa maisha kwa mwaka mpya wa 2012 ambao kunako majaaliwa tutaka nao hapo kesho. Nauli za kivuko zimepanda sisi wengi wetu wenye vigari vya aina ya Sloon tutakamuliwa ka shilling 1,500 abiria wa kawaida shilling 200.00, n.k. sasa mimi nauliza hawa watu wanapandisha gharama za kivuko bila kuboresha miundombinu. Kwanza waboreshe miundombniu ndio wapandishe hizo nauli ili kufidia kufidia gharama hizo, kwa kufaya hivyo hata sisi wadu wadau hatutakuwa ma mallamiko kwani tunalipia tunachokipa-wachumi na wataalamu wa fedha wanaita "thamani ya pesa".

  Vilevile pale ferry kuna matukio ya ajabu sana, kuna hawa wanaojiita eti ni walinzi wa watanzania-Wanajeshi, polisi, magereza, uhamiaji na vibosile wengine. hawa wanajiona wako juu ya sheria. Askari mzima analala mpaka saa moja asubuhi anafika ferry saa mbili au zaidi, hataki kupanga foleni kama wanavyofanya wanachi wengine wastaarabu ambao wanakaa kwenye foleni mpaka masaa mwawili. tunavyo jua askari anatakiwa kwenye wanaita foleni yao kuingia kazini saa kumi nambili au 12.30 ili waanze kazi saa 12.30. na ndio maana askari wote wantoka kazini saa nane na nusu na sisi raia tunatoka kazini saa 9.30 kwa sababu tuanaanza kazi saa 1.30.

  Sasa hawa jamaa kwanza wanaiibia serikali kwa kuchelewa kazini, pili sio askari wenye nidhamu ya kazi na wanakikuka maadili yao kazi , tatau wanaibia serikali kwani pale ferry sidhani kama wanalipa nauli kivuko. Na utakupta wengine wanakuja na magari yao ya binafsi na huku wamevaa kiraia na mbaya zaidi wanasababisha ususmbufu watumiaji wengiine wa kivuko na kuvyuruga utaratibu mzima wa uendeshaji wa kivuko.

  sasa tuanongezewa gharama za kivuko wakati kuna watu hawalipi hizo nauli.

  Wadau, hao wahusika watuambie hivi hakuna taratibu zilizowekwa katika uendeshaji wa kivuko? na askari hizo sheria na taratibu haziwahusu? na wafanye utaafiti ni kiasi gani cha mapato kinapotea kwa siku, wiki, mwezi na mwaka kutokana na hao askari kutolipa nauli ya kivuko kabla ya kuwabebesha mzigi wa gharama watumiaji wengine.
  wadau hii ndi kero yangu
   
Loading...