Nauli ya Dar kwenda Ifakara

Nauli ya Dar kwenda Ifakara

Wakaya

Senior Member
Joined
Sep 11, 2014
Posts
198
Reaction score
67
Habari ndugu zangu wana jf,naomba mwenye kufahamu nauli ya kutoka Dar kwenda Ifakara Morogoro
 
nauli halisi toka dsm to ifakara ni 17,000 hapo andaa na matumizi yako ya njiani maana safari ni hatua...
 
Nilipita muda mrefu kidogo wakijenga kwa kiwango cha lami, ujenzi umekamilika kuanzia Kilombero hadi Ifakara?
 
Habari ndugu zangu wana jf,naomba mwenye kufahamu nauli ya kutoka Dar kwenda Ifakara Morogoro

Nauli ya Ifakara Tsh 17,000/- , kama unahitaji gari ya haraka panda Mwembamba Express, ukirudi usisahau Pepeta za zawadi ya family.
 
Nilipita muda mrefu kidogo wakijenga kwa kiwango cha lami, ujenzi umekamilika kuanzia Kilombero hadi Ifakara?

Mkuu wakati Unapita walikuwa wanajenga eneo gani, ila kwa ufupi bado barabara mbovu.
 
Barbara iko poa wameweka moramu sehemu zote tata. Ukipanda mwembamba SAA 7 na nusu upo Ifakara.
 
Nilipita muda mrefu kidogo wakijenga kwa kiwango cha lami, ujenzi umekamilika kuanzia Kilombero hadi Ifakara?

Ulipita ikiwa unaota ndotoni? Lami mwisho kilombero darajani kuanzia mkamba unapiga shimo tu.
 
Ulipita ikiwa unaota ndotoni? Lami mwisho kilombero darajani kuanzia mkamba unapiga shimo tu.

Wakati napita walikuwa wakitandaza lami eneo la magereza jina limenitoka, kumbe kazi ilisimama.
 
Wakati napita walikuwa wakitandaza lami eneo la magereza jina limenitoka, kumbe kazi ilisimama.

panaitwa signali Luna kipande kidogo cha lami lakini hii ndo njia inayo ongoza kwa kua na madaraja mengi zaid
 
Nauli halali 17000, ukilia mpaka 15000, nenda kuna mwana jf mwenzako pale m-pm ifa96.
 
Last edited by a moderator:
Mungu awabariki wote!.Asanteni sana pia.
 
Ukitaka kwa kuunga panda BM au Abood mpaka Moro 7000, pale Moro kuna magari mengi ya Ifakara Tsh 12000, thus jumla 19000 Tsh. Ubarikiwe.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Naweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo?
 
Back
Top Bottom