Nauli halali Dar - Moshi kwa sasa?

Nauli halali Dar - Moshi kwa sasa?

kyalankota

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2014
Posts
2,594
Reaction score
1,463
Habari za majukumu wadau wa JF! Natumaini mko poa na mnaendelea kupambana na hali zenu.

Lengo langu ni kutaka kujua nauli ya Dar to Moshi kwa basi ni sh ngapi kwa sasa?
Pia nataka kujua kama kuna gesti ama lodge ambazo zipo karibu na hospitali ya KCMC ama ni lazima nitokee town kwenda huko? Ntakuwepo kwa siku kadhaa.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
Kwenda moshi ni lazima ulipishwe nauli ya arusha pia inategemea na basi husika ila nauli ipo kwa viwango

Kuna Ordinary nauli ni 23000/= = haya ndo yale mabasi gonga nyundo na seat ni 3 by 2 unaeza kukuta lina tv moja au 2 au zisifanye kazi hakuna cha bure kama pipi soda wala keki hapo safari tuu na hayanaga muda muhafaka au zikafanya hili ndo daraja la kawaida

Semi luxury 33000 = Hili ndo daraja la kati hapa ndio kampuni nyingi zinatumia unakuta bus lina tv mbili na kuendelea seats ni 2 by 2 wanagawa vinywaji pia na pipi na biscut au cake kwa baadhi pia Ac zipo zenye nazo na zisizo nazo kwani kwao sio lazima.

Luxury / VIP 36000 - 46000/= luxury hapa gari zake huwa hazina tofauti sana na semi ila kuna vitu huwa vinaongzwa kama tv ni 5 na kuendelea na lazima liwe na choo

VIP bus linaweza lisiwe na choo ila ni mlolongo wa seat huwa ni 2 by 1.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom