Natoa wito Jeshi na Walalahoi tumuunge Mkono Kapten Tesha. Tumlinde ni moja ya Tunu za Taifa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
13,625
Reaction score
29,891
Napenda kutoa Rai kwa heshima na Taadhima kwa Watanzania. Tumuunge mkono Kapten Tesha. Natamani haraka sana nije Tanzania. Natamani sana. Nimemsikiliza machozi yamenitoka.

Huyu Kapten anajua vizuri hatari ambayo inamkabili baada ya hili. Anajua vizuri changamoto ambazo atakumbana nazo. Ameamua kumfunga paka kengele. Huyu ni mmoja ya Wazalendo wakubwa wa hii nchi. Tafadhali nawaomba Watanzania bila kujali vyama, dini na rangi au njaa na matumbo yetu. Tumuunge mkono.

SAA YA UKOMBOZI NI SASA. Miaka mingi sisi tumeshiriki kuifisadi hii nchi na kujineemesha wenyewe na familia zetu. Huu ni wakati wetu kutubu na kuona aibu kwa mateso ambayo tumewapa mama, dada, shangazi na wake zetu.

Mateso ambayo wamepata wazee na watoto wetu. Kwa namna yoyote. Mimi nakiri kuwa nimeshiriki kuifisadi nchi kwa kula kwa urefu wa kamba yangu. Bila kufikiria wale ambao wamefungiwa kwenye milingoti hata kamba hazipo. Nimekula kwangu na nikaenda kula kwao. Naombeni msamaha watanzania.

Hotuba ya Kapten Tesha imenifikirisha sana. Nimetokwa na machozi. Amemtaja Shetani kwa jina kabisa bila woga wowote. Tumuunge mkono. Lissu nisamehe pale ambapo nlikusema vibaya. Sasa nakuelewa zaidi. Umeutoa uhai wako sababu yetu. Ungeweza kukaa ughaibuni ukala maisha. Hukufanya hivyo. Ulirudi nchi ile ile iliyokupiga risasi ukapambane na mafisadi. Wewe si mtu wa kawaida. Katika hili Lissu hukuwahi kufikiria Dini. Ulifikiria haki zaidi.

NATOA WITO TUMUUNGE MKONO KAPTENI TESHA.
 
Nilisema, kadri tarehe 29 oct inavyosogea, kuna matukio mengi na yasiotarajiwa yanaenda tokea, kuna moja nalisubiri, wana CCM wale maarufu kumgeuka mama siku chache kabla ya 29 OCT, sema yeye anauwezo mdogo wa kufikiri hawezi ona hili.
 
Ila bado nina shaka, Tesha msoja kweli?

Au amekuja kupima upepo? Ile kofia na nembo ya begani vimenitia mashaka tusubiri kidogo
 
Nilisema, kadri tarehe 29 oct inavyosogea, kuna matukio mengi na yasiotarajiwa yanaenda tokea, kuna moja nalisubiri, wana CCM wale maarufu kumgeuka mama siku chache kabla ya 29 OCT, sema yeye anauwezo mdogo wa kufikiri hawezi ona hili.
Hii ni kete ya muhimu ambayo possible washauri wa Mama hawajajua au labda anashauriwa lkn hashauriki. Refer Sikio la kufa...
 
Ila bado nina shaka, Tesha msoja kweli? Au amekuja kupima upepo? Ile kofia na nembo ya begani vimenitia mashaka,tusubiri kidogo
Mbona Ile "Taarifa kwa Umma" ya Jana kama una walau D mbili tu unaelewa kuwa ndiye au siye...
Au uko kitambaa cheupe unajipoza 😂
 
Mimi na ukoo wangu na Kijiji changu tuko tayari kumuunga mkono kapteni Tesha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…