National Database Center iundwe Tanzania

National Database Center iundwe Tanzania

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2017
Posts
1,339
Reaction score
1,493
Habari Tanzania !

Mnataka mawazo ya vijana, ishi nayo hii wewe mwenye nguvu na mamlaka Tanzania.

Naomba kupendekeza kuwa; Watanzania wote wasajiriwe nchi nzima. Tuwe na data za taarifa zao kuanzia Watu waliopo, wanaozaliwa, kufa, umri, Jinsia, Elimu, Kazi, nk ili tunapoweka mipango ya maendeleo tuwe na uhakika halisi na tusiwe watu wa maoteo yasio na maana yoyote.

Ule mchezo wa kupoteza fedha wa Sensa umepitwa na wakati. Sababu sensa hufanyika kila baada ya miaka kumi. Njoo kwenye maendeleo ya nchi hupangwa kila mwaka. Ukitazama Dira ya Taifa inachukua miaka 25 huu si utoto na ujinga wa kupoteza fedha nyingi kila baada ya miaka 10.

Tunataka Database Center hii iwe huru zaidi na isihusishwe na wale jamaa NBS kabisa. Ila wanaweza ingiliana na sio wafanye kazi sehemu moja.

Hii taasisi iweke sera na utaratibu mkali kuwa hakuna taasisi yoyote inayofanyakazi Tanzania kiholela hasa hizi taasisi za Serikali, Bunge na Mahakama.

Nitarudi.

Karibu.
 
Back
Top Bottom