National Committee For Constitution Reform (NCCR)

Sr. Magdalena,
Ahsante sana kwa swali lako. Naomba kulijibu kama ifuatavyo;
NCCR iliyoundwa mwaka 1991 ndio ilikuwa kamati ya kitaifa ya mabadiliko ya katiba, yaani National Committee for Constitutional Reform.
Viliporuhusiwa vyama vingi mnamo mwaka 1992, NCCR-Mageuzi kilisajiliwa kuwa chama, lakini kikiwa si Kamati tena bali National Convention for Construction and Reform, yaani kama katiba ya chama inavyotafsiri jina hili; ni chama cha Mageuzi na Ujenzi wa Taifa.
Aidha nikutaarifu kuwa Halmashauri Kuu ya Chama ilipokutana mwanzoni mwa mwaka jana (2011), pamoja na mambo mengine iliruhusu mjadala wa kulibadili jina la chama kuwa katika lugha ya kiswahili, hivyo pendekezo lako linaendana kabisa na mchakato uliokwisha kuanza ndani ya chama.
Kumradhi, katika maelezo yako kuna kitu sijaelewa, umesema bunge limepitisha mabadiliko ya sheria ya uchaguzi, ni yapi hayo?

Mkuu Kahangwa heshima mbele sana,

Nilimaanisha sheria ya mchakato wa mabadiliko ya katiba, nimebadilisha kwenye post yangu, na nashukuru kwa kunirekebisha.

Nadhani itakuwa jambo la busara sana kufanya mchakato wa kupata jina jipya, tena la kiswahili ili mtanzania wa kawaida aelewe chama kinasimamia nini na kina amini nini, na mabadiliko haya yangefanyika haraka ili muweze ku rebrand jina hilo na watu kulizoea kabla ya 2015, naamini chama chenu kikiwa strong kama CDM itakuwa ni jambo jema sana kwa mstakabali wa taifa letu, na je unaweza kutueleza japo kwa kidogo makubaliano mliyo tiliana sahihi na CDM ni yapi na nyinyi kama chama mnadhani yatawasaidia vipi? Kwa kuwa kubwa linalozungumzwa ni ufutaji wa kesi ya mwenyekiti wenu na mbunge wa CDM kawe.
 
Ahsante sana kwa ushauri Sr. Magdalena. Bahati mbaya kwangu sikuwepo nchini wakati makubaliano kati ya NCCR-Mageuzi na CHADEMA yanasainiwa. Ikitokea nikapata undani wake zaidi, sitasita kukufahamisha.
Miongoni mwa mambo ambayo chama kinasimamia, ni kutaka kuwepo mageuzi ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika taifa letu (kama jina la sasa linavyoashiria). Chama kinaongozwa na falsafa ya UTU na kinaona ndio falsafa inayoifaa jamii yetu. Ujenzi wa demokrasia kamili, uwepo wa haki na sheria zinazosimamia haki ni miongoni mwa mambo ambayo chama kinayaamini. Kutokana na hayo, kwako wewe waweza kupendekeza jina gani?
Ukitaka ufafanuzi wa hayo machache niliyoyataja, nifahamishe tafadhali.
Aidha, naomba uzingatie kuwa, kufanyika kwa marekebisho ya sheria ya mchakato wa kupata katiba mpya hakuna maana tayari katiba mpya imekwishapatikana. Hivyo watetezi wa hoja ya Taifa kuwa na katiba mpya hawapaswi kuweka silaha chini wakidhani 'vita' imekwisha.
 
asante sana kwa maelezo yako matamu ila tngependa mara baada ya kufahau makubaliano hayo utuhabarishe ili nasi tujue nini kinachoendelea ktk taifa hili NCCR NI CHAMA MAKINI NA IMARA
 
Hapa hakuna chama. Sijawahi kuona viongozi wakuu wa chama wanashushwa kwenye jukwaa wasihutubie ngome zao. Wote tuliona kupitia tbc namna katibu mkuu wa nccr na mbunge yule mwanamke wa kasulu walivoshushwa jukwaani kwa kumsema kafulila vibaya. Sasa hapa kuna chama kweli?afadhari juzi wamefuta kesi ya mdee kawe mana hata kama ni uamuzi uliochelewa lakini bora umefanyika mtuachie mbunge wetu jembe. Saiv mnapata ruzuku hakuna sababu ya kuendelea kutumiwa na sisiemu kama zamani. Imarisheni chama chenu kisomeke. Muwe na uwezo wa kufanya mikutano watu waje.badilisheni uongozi muweke vijana wenye upeo, hawa akina mbatia na ruhuza wamepauka mno. Wameshatumika na sisiemu mpaka wamechuja. Tengenezeni agenda. Mtuuzie wananchi tununue. Kama cdm walivotuuzia agenda ya buzwagi na list of shame. Sasa agenda bado ni nying ktk gvt mbovu kama hii.hayo ndo mamuzi magumu mnapaswa kufanya.
 
Back
Top Bottom