Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,560
- 1,821
Habari za leo wapendwa?
Mwenzenu niko njia panda hata future yangu siioni! Kwa ujumla naelekea kukata tamaa kabisa. Mimi ni mgonjwa, nahitaji ufumbuzi wa tatizo langu lakini pamoja na juhudi zote mpaka sasa sijapata mwanga nalimalizaje mie! Ni mwaka sasa tangu nimeanza kuteseka na tatizo hili. Mimi ni mwanaume, umri wangu miaka 50. Nina tatizo katika njia ya mkojo ambalo daktari wangu amelitambua kuwa ni COMPLICATED U.T.I.
DALILI ZAKE:
1. Mkojo kuuma sana wakati wa kukojoa mpaka muda mfupi baada ya kukojoa.
2. Muwasho na maumivu eneo zima la kinena, mapajani kwa ndani na njia ya haja kubwa.
3. Ninapokaa nahisi kama nimekalia kitu katikati ya makalio (eneo kati ya uume na njia ya haja kubwa).
4. Maumivu makali wakati wa ejaculation (kutoa mbegu za uzazi).
N.B: Pamoja na mkojo kuuma, mkojo unatoka kawaida na unaisha kwenye kibofu.
JUHUDI ZA KUSAKA TIBA:
Nilianza kupata huduma katika hospitali ya wilaya huku kwetu mkoani ikionekana nasumbuliwa na U.T.I. lakini sikuwahi kupata nafuu yoyote. Hatimaye nilipewa rufaa kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako nilipata vipimo mbalimbali (ikiwa ni pamoja na ULTRASOUND SCAN, VIPIMO VYA DAMU NA MKOJO).
Baada ya vipimo, Daktari Bingwa wa njia ya mkojo (Urologist) aliniambia kuwa tatizo langu linaitwa COMPLICATED U.T.I. Ni U.T.I. ambayo imesababisha maambukizi kwenye Tezi Dume. Tezi dume haijangezeka (not enlarged) lakini imevimba (inflamed) ndio sababu ya hisia ya kukalia kitu katikati ya makalio. Alinambia kuwa tiba yake haihitaji upasuaji kwa kuwa tezi haijaongezeka. Nitapewa dawa za kuondoa maambukizi (infection) na hali yangu itaimarika.
Nilipewa dozi ya LEVOFLOXACIN 500mg mara moja kwa siku kwa muda wa siku 30 lakini hata baada ya kutumia dawa hiyo kwa ukamilifu sikupata nafuu yoyote. Kwa sasa nipo nyumbani huku mkoani. Changamoto niliyonayo ni kukosa fedha ya kurudi Muhimbili kufuatilia tiba zaidi ukizingatia sina bima ya afya.
SABABU YA KULILETA HAPA JAMVINI:
Natambua kuwa JamiiForums imejaa wabobezi wa fani na taaluma mbalimbali. Nimelileta hapa nikiomba msaada wa ushauri kwa madaktari mliomo humu juu ya tiba zaidi ninayoweza kutumia bila kulazimika kurudi Muhimbili baada ya LEVOFLOXACIN kufeli ukizingatia tatizo tayari linafahamika.
Mniwie radhi kwa post ndefu. Nimejaribu kuandika hivi ili maelezo yatosheleze bila kuacha maswali mengi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa msaada kutoka kwenu.
Natanguliza shukrani nikisubiri msaada wenu!