Sababu ya Wanawake wengi Tanzania kupata U.T.I na suluhisho lake

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,107
34,066
Habarini Wadau,

Kwa Miaka ya hivi karibuni kuna magonjwa ambayo yamekithiri sana miongoni mwa Watanzania na watu wengine Duniani, kama Kisukari, S.T.I's za aina zote, Cancer n.k

Nitazungumzia Urinary Tract Infection (U.T.I) kwa nchini kwetu Tanzania pamoja na kisababishi ambacho wengi hawakijui

MASWALI: Umewahi kujiuliza ni kwanini miaka ya zamani wakati watu hata walio wengi kama wanafunzi walikuwa wakitumia vyoo vya shimo vyenye tundu chache lakini hawakuwa wakipata Bakteria wanaosababisha UTI?

AU, Mwanamke umewahi kujiuliza ni kwanini unatumia choo kisafi kabisa na kujisafisha kwa maji lakini unapata UTI isiyokoma?

AU, Umewahi kuwaza ni kwanini wanawake wa Kenya (Hasa Nairobi) na Wanawake wa Kizungu hawapatwi sana na UTI isiyokoma kama ilivyo kwa wanawake wa Mombasa, Lamu, Pate, na Tanzania?

SABABU KUU YA UTI KWASASA TANZANIA
- U.T.I Inaweza kuambukizwa kutokana na ngono isiyo salama kutoka kwa Mtu mwenye UTI na kupeleka kwa asiyekuwa nayo, LAKINI PIA,

1) U.T.I inaweza kusababishwa na Bakteria ambao kwa kawaida hukaa katika maji yaliyotulia kwenye vyoo hivi vya kisasa ambavyo muda mwingi hubaki na maji. Mwanamke anaweza kutumia vyoo hivi na kuondoka na bakteria wasababishao UTI

2) U.T.I inaweza kusababishwa na utawazaji mbaya, kwa kawaida Mwanamke kulingana na maumbile ya Uke wake ulivyo anapaswa kujitawaza kwa kujimwagia maji kutoka sehemu ya mbele kuelekea nyuma na anapaswa kujikausha kabisa kwa kutumia Tissue/Toilet paper au kitambaa kikavu.

Endapo Mwanamke atajitawaza/atachamba na maji pekee bila kujikausha na kuondoka na ubichi ubichi kuna uwezekano mkubwa sana wa bakteria kujizalisha sehemu za siri

KWANINI WENZETU WAKENYA NA WATU WATU WA NJE HAWANA HII KADHIA SANA?

JIBU: Ni kwasababu wao wanatumia zaidi Tissue / Toilet paper kuliko maji.

Ni ngumu sana katika pochi ya Mzungu au Mkenya kukosa Toilet Paper. Sisemi kuwa dada zetu wasitumie maji...kwani maji ndiyo yanayotakatisha zaidi, LAKINI ni vyema wakahakikisha wanajikausha kila baada ya kutumia maji.

Utumiaji wa Wipes nao ni mzuri lakini haukaushi maji vizuri

Wakati tunakuwa tulikuwa tukitumia karatasi au majani ya miti na hakukuwa na maambukizi ya UTI kama hivi sasa.

Aidha, Unaweza kuzuia au kutibu UTI kwa kutumia mchanganyiko wa majani mabichi ya Mpera, Mtipisi, na Mkomamanga mbichi Hasa kwa Wanaume.


Wabillah Tawfiq,
 
Back
Top Bottom