Ila siku akitaka mchezo huwa anakutafuta mwenyewe si ndiyo?
Nampenda sana Steve Harvey, pamoja na kuchekesha huwa kuna hyakati anatoa ushauri mzuri sana hasa kwa wadada.
Mojawapo ni: wewe ndiye utakayeamua mwanaume akutreat vipi. You set the standard.
1. Mfano mdogo kwake na mke wake...kwenye ndoa yake ya kwanza na ujanani alikuwa mhuni ila alipokuja kukutana na mkewe wa sasa, Marjorie, she purposed to make him who she wanted him to be. Alianza na kubadilisha wardrobe yake na kumfanya amtreat as a lady. Kwenye gari lazima Steve amfungulie mlango anapoingia na anapotoka. Akijifanya kusahau basi haingii wala hatoki. If a man really loves you, he will change for you as long as unachotaka afanye sio kosa la jinai au nje ya uwezo wake.
2. Kuna mbinu ya tit for tat. Usilalamike..huwa hatupendi mtu akilalamika. Ila mweleze tu, ninapenda unifanyie 1, 2, 3. Kisha mwache hapo. Asipotekeleza na wewe mnyime kile akipendacho kutoka kwako. Mfano mwingine kutoka kwa Steve Harvey na mkewe ni, Steve alikuwa careless. Akija anachukua chakula kwa fridge akimaliza anaacha kilichobaki mezani harudishii kwenye fridge wala hapeleki vyombo jikoni, tena wala hakutakiwa kuviosha. So mkewe akamweleza na siku iliyofuata walipofika chumbani, Steve anajiandaa kupata mzigo mkewe akajifunga taulo akawa anatoka. Steve akahamaki unaenda wapi. Akamjibu anaenda kutoa vyombo ambavyo yeye aliviacha. So muda ambao ungepata unachokitaka ndio muda ambao inabidi nikafanye yale uliyopaswa kuyafanya.
3. Sex. Ngono tumeifanya ni kitu kidogo sana lakini ngono ni muunganiko mkubwa. Muda mwingi wapenzi tunatumia kufanya ngono bila ya kujuana. Kama nanyi mko kundi hili, njia nyepesi sana ya kujua kama bado yupo na wewe ama la ni kumnyima ngono. Mweleze mpaka atakapoonesha upendo unaoutaka (again set the standard). Kama anakupenda kweli anabadilika na atasubiri. Kama la, usiumie akiondoka.
Mwisho mkumbushe kina Elon Musk, Phil Knight, Bill Gates na matajiri wengi walioandika biography zao wanajutia muda waliotumia kutafuta pesa wakasahau familia zao. Jiulize, hapo ni boyfriend hata si mchumba ila yuko bize kwako unadhani hata kama unampenda akija kukuoa (NAKUHAKIKISHIA HANA MPANGO WA NDOA NA WEWE..ila tuendelee kuassume) unadhani atakaa nyumbani kulea familia? Mimi binafsi nimesoma biography za Elon Musk na Phil Knight (owner wa NIKE) na wote wawili wanajutia kutotumia kuda wa kutosha na familia zao. Dalili uaziona mapema, again, set the standard unayoitaka. If he loves you he will conform.
Mdediketie Buy Me a Rose - Luther Vandross.
Wahenga walisema we are never busy...its priorities!
Kila la kheri...kimbia kabla hujawa single mother (ndiyoo unaweza kuwa single mother tena ukiwa kwenye ndoa)!
Sent using
Jamii Forums mobile app