Jongwe
JF-Expert Member
- Apr 25, 2008
- 1,040
- 666
Waswahili wenzangu nimekuwa nikitatizwa sana na matumizi ya maneno yafuatayo, labda mimi kiswahili kimenipiga chemga, ama watumiaji wanatumia maneno hayo ndivyo sivyo.
1. Kwa niaba yangu mwenyewe - Mtu anatoa shukrani halafu anatanguliza neno "kwa niaba yangu mwenyewe natoa shukrani..." hivi hii ni sahihi kweli? Kwani isiwe kwa niaba ya ndugu zangu (akiwa na maana anawakilisha kundi fulani la watu..)
2. Mimi kama mimi - nijuavyo mimi unapotumia neno "kama" ina maana unafananisha na kitu fulani. Sasa inakuwa mtu anaongea anasema "mimi kama mimi nisinge chukua hiyo pesa" kwani isiwe "ningekuwa mimi nisingechukuwa hiyo pesa". Utakuta mwanaume/mwanamke anakuambia mimi kama mwanaume siwezi kufanya... kwani isiwe mimi mwanaume siwezi kufanya...