Baada ya kufuatilia mchakato wa kampeni na kutafakari tulikotoka na kuangalia tunakokwenda nimeamua kutangaza kujiunga na CCM.
Sababu ni nyingi lakini kwa uchache sababu zangu ni hizi
1. Ubora wa vyama
Kimsingi CCM ni chama cha watanzania kwa maana chama hiki hakihodhiwi na familia fulani au waasisi hawana mizizi tena ndani ya chama hiki. lakini vyama hivi vingine nimeviangalia nikaona bado vinamirikiwa na watu fulani.
Vyama hivi vinakaribisha wanachama kwa kuwa ndio tiketi ya kuungwa mkono na wapiga kura lakini katika baadhi ya vyama bado nafasi muhimu zinahodhiwa moja kwa moja au kupitia wawakilishi wao. si kila mtanzania anaweza kuingia katika vyama hivi akazigusa nyadhifa hizo hata kama zimevikwa mwavuli wa nyadhifa hizo kupigiwa kura kidemokrasia.
Kama taifa ni lazima tujihakikishie kuwa chombo hiki ni maliyetu kabla ya kufanya maamuzi ya kukikabidhi chombo hicho madaraka makubwa zaidi ya nchi yetu vinginevyo tunaweza kuchuuza uhuru wetu na mali zetu kwa gharama nafuu nafuu.
Kwa chama cha watanzania tunakuwa na uhakika kuwa hata kama chama kitapata kiongozi akatuongoza vibaya lakini kwa kuwa kiongozi huyu chama si chake basi kiongozi huyu anaweza kutoka na akaingia kiongozi mwingine na akatupeleka tunakotaka.
2. Ubora wa wagombea urais waliosimamishwa na vyama.
Leo hii watanzania wote wanalalamika maendeleo yetu hayalingani na uwezo wetu. kabla ya kufanya maamuzi yoyote ni lazima tutafakari tatizo liko wapi na tuchague njia ya kupita.
Jambo hili linachangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi tuliokuwa tumewapa dhamana lakini hiyo pekee haitoshi bali kuchunguza kwa vipi? tatizo kubwa ambalo limefanya viongozi wetu washindwe kutupatia maendeleo tuliyotegemea ni mfumo wa kupatikana viongozi hawa. tulitengeneza utaratibu wa watu kuunda makundi na kuanza kutafuta uongozi na pale wanapoupata hugawana nyadhifa zote lakini muungano wao kama kundi hudhoofisha madaraka na uwezo wa uongozi.
Mtu anapewa kuongoza wizara au shirika si kwa sababu ameonekana kuwa na uwezo wa kuliongoza vizuri bali kwa sababu ni mwana mtandao au kundi. mtu anafanya kosa anashindwa kuwajibishwa si kwa sababu hakuna sheria bali ni mwenzao.
Mambo haya yalifanya watu waliopewa dhamana wakafanya kazi kwa uaminifu kwa kuwatumikia wananchi kuchukiwa na watu hawa waliounda mitandao wakiwa wengi wao hawana sifa kwa maana utendaji wa hawa ama uliwazibia riziki kwa kuziba nafasi walizokuwa wakizitumia kutuibia watanzania au waliumbuliwa kwa uzembe wao au kuonyeshwa wazi kuwa walikuwa mbumbumbu.
Enzi hizo watendaji bora kama Augustino Mrema walikimbia chama hiki cha watanzania, kwa uelewa wangu ni kuwa chama ni mali ya wanachama hivyo katika kufanya maamuzi wote wabaya kwa wananchi na wazuri wanashiriki katika kufanya maamuzi.
Wazuri watajitahidi kuleta maamuzi ya kuwatetea wananchi na wabaya watajitahidi kufanya maamuzi ya kulinda maslahi yao. hivyo inategemea ni kundi gani limeshika mpini na kundi gani limeshika makali.
Baada ya 1995 tumepita hatua tofauti mpaka hapa tulipo leo.
kwa mtizamo wangu binafsi chama hiki cha watanzania yaani CCM kwa sasa bado kinayo makundi yote ndani lakini kundi linalotaka kuwatetea wananchi limeshika mpini. Kwanza walitambua kuwa chama hiki kimetekwa na watu wanaosimama kwenye majukwaa kuwaambia wananchi mambo mazuri lakini walipopewa nyadhifa wamewageka wananchi na katibu mkuu akazunguka nchi nzima akitangaza nia yao ya kurejesha madaraka kwa wanachama.
Msemo huu wasiouelewa wanaweza kudhani ni maswala ya mashina ya vyama huko ngazi ya chini lakini tafsiri pana ni kurejesha chama katika kutumikia wanachama au wananchi na sio chama kutumika kama njia ya watu kuingia kutafutia dili tena nyingi zikiwa ni za kukinzana na sheria.
Bado nikirejea mwaka 2010 wakati wa msimu wa pili wa raisi wetu anayemaliza mda wake, alikuwa ameamua kuachana na wapambe wa kampeni. hili lina maana gani? kwangu mimi ninaona kabisa kuwa raisi baada ya kukaa miaka mitano aliona jinsi mizigo ya makundi ya kampeni ilivyokuwa ikimkwaza katika kutimiza matakwa ya wananchi. nadhani alitamani asitumie watu kufanya kampeni ambao wangemgarimu k