Natangaza rasmi kujiunga CCM

Natangaza rasmi kujiunga CCM

Changamoto ni watanzania hatujui kuchambua mambo na kuyahusisha na maisha yetu.

mifumo yetu ya elimu haituwezeshi kuoanisha practical life na theorical knowledge.

anayekabiliwa na changamoto sio chama cha mapinduzi bali ni watanzania.

chama cha mapinduzi hakina mwenyewe bali ni mali ya watanzania.

ni sawa na watanzania tulivyounda mashirika kama tanesco kushughulikia mambo ya umeme. sasa kama tumeunda shirika la tanesco tukakusanya kodi tukaweka na wakatokea baadhi ya watanzania wakagundua kuwa watanzania tumelala wakatumia kodi zetu tunazoingiza tanesco kwa matumizi yao na sisi tukabaki tukisema tatizo la tanesco ni kutokuboresha umeme hivyo bora yaje makampuni ya kigeni yatupatie umeme unadhani nani mjinga hapo je ni wale wachache waliotuibia? au ni sisi wenyewe tulioibiwa tuna matatizo?

mfumo wetu wa siasa tumeweka uongozi wa nchi lazima upitie kwenye vyama vya siasa. asilimia kubwa ya watanzania tumelala lakini wakawepo wahuni wachache wakatutambua tulivyolala wanaingia wanasimama kwenye majukwaa wanatulaghai kwa maneno kwa staili ya matapeli tunawakabidhi madaraka kumbe wengi si viongozi.


tukitambua hili hatutakaa kuangalia jina la chama na kudhani jina ndio tatizo, kama unavyoona mkisema kampuni haitalipa kodi miaka mitano na wajanja wakaanza kubadili majina na kujifanya ni kampuni mpya na kuendelea kutokulipa kodi ndivyo wajanja hawa watakavyobadili majina ya vyama lakini matendo ni yaleyale na watu ni walewale.

tunahitaji kutambua matatizo yetu ni yapi na tutatue hayo na sio kukalili majina ya makundi kumbe wajanja wanahama huku na kule.

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaelekea imekanyaga mdudu mchafuzi. Mdudu huyo Zanzibar anaitwa sheshere, Wabena humwita hilufi, Wasangu wanamwita shilufya. MWENENDO wa uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) unasikitisha mno. Masikitiko yenyewe ni yale yanayotokana na utamaduni mbaya wa kuujua ukweli, halafu kwa makusudi, viongozi wakaamua kuudharau.
Mtu akikanyaga sheshere, hawezi kufika anakokwenda; atazunguka sana, atapitiliza hata eneo analokwenda hadi ashikwe au asimamishwe na mtu anayemfahamu.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa Serikali ya CCM. Imekanyaga sheshere. Inasema ovyo, inayumba njia nzima tangu ilipoanza safari mwaka 2005. Haieleweki. Mara inasema maisha bora yanawezekana, mara wabunge wake wanalia Ilani ya CCM haitekelezeki.Mara JPM ana ahidi yale yale waliyo ahidi 2005 lakini hayajatekelezeka.
Wapo makada wa chama hiki kikongwe ambao tambo zao ni kwamba kitadumu madarakani kwa karne nyingi zijazo, lakini wamekosa ujasiri wa kuona kuwa kila hatua inayopigwa katika kujipanga upya inakuwa afadhali ya ilivyokuwa hapo kabla, mwendo ni kukimbilia kwenye kuangamia, hawasikii na wala hawaoni.
Kwa sababu hiyo,wapo Makada waliopata kuonya iwapo chama hicho hakitarudi kwenye asili yake hiyo, itakapofika Oktoba 25,2015, siku ya uchaguzi mkuu mwingine, "kinaweza kupata majuto yasiyo na kifani." Tatizo la serikali ya CCM ni kuvimbiwa madaraka kiasi cha kushindwa kujua hata maana ya kaulimbiu ya Peoples Power. Hata watoto wadogo wanajua kwamba kaulimbiu hiyo haina maana ya fujo, tafsiri ya fujo inatolewa na dola na CCM kwa kusisitiza amani na wakati huo huo wakionekana waziwazi wakijiandaa kukandamiza haki.
CCM inaongoza wanachama wa CCM na wahuni,wapumbavu,mbumbumbu na malofa " kwamba kama hauko CCM basi wewe ni mhuni,mpumbavu,lofa na mbumbumbu.
CCM inakandamiiza haki za msingi za raia kwa vitisho ama kwa kutumia kodi za wavuja jasho kama kujiunga na chama chochote cha Siasa,kukusanyika,kutoa maoni n.k.
Kutokana na ukweli huu, CCM haiwezi kuwaletea watu maendeleo bali inanufaika na Umaskini wao.Haiwezi kuwaletea maendeleo kwa sababu maendeleo yatafanya wananchi wasikitegemee chama hicho tawala kwa fulana, kofia na skafu za kuvaa wakati wa sikukuu, kusali makanisani na misikitini na hata sokoni.
Kwa hiyo, si kila anayehudhuria mikutano ya CCM na anayevaa kofia na fulana ya CCM ni mpenzi, shabiki au mwanachama wa chama tawala bali wengine na ambao kwa kweli ndio wengi hufanya hivyo kwa kukosa mavazi mazuri ya kutokea pamoja na kushuhudia burudani za muziki za wasanii Chege,Temba,Diamond na wengineo.
Ushahidi mwingine wa jinsi CCM inavyonufaika na umaskini wa Watanzania ni biashara ya shahada nyakati za uchaguzi. Biashara ya shahada ambapo mabalozi na wenyeviti wa CCM wa mitaa na kata huranda huku na kule kununua shahada hushamiri sana katika maeneo maskini.
Ndiyo maana CCM ambacho ni mtuhumiwa mkuu wa ununuzi wa shahada za kupigia kura mara zote hushinda uchaguzi katika maeneo ambayo wakazi wake ni maskini wa kutupwa kama vile mitaa ya Dar es Salaam iliyojaa wabwia unga.
Pia kuna madai kwamba chama tawala ni maarufu kwa kugawa fedha shilingi elfu mbili mbili, tatu tatu au elfu nne nne ili kipigiwe kura iwe kwenye uchaguzi mkuu au uchaguzi mdogo. Madai haya yanapata nguvu kutokana na ukweli kwamba wapo wana-ccm wamekamatwa wakiuza au kununua shahada za kura.
Kwa ufupi, CCM inanufaika sana na umaskini wa kutupwa. Bila umaskini wa kutupwa fulana za njano, kofia za kijani na skafu zisingeonekana makanisani na miskitini. Watu wanahudhuria mikutano ya hadhara ya CCM ili kuambulia ‘kiwalo' tu na si mapenzi na chama.
Pia watu wanahudhuria kwa wingi mikutano ya hadhara ya CCM ili waweze kuambulia shilingi elfu tatu za kununulia unga wa muhogo wakasogeza siku mbele na si kwa kukipenda chama hicho kikongwe cha siasa nchini. Umaskini ni kete kubwa kwa CCM.
Huenda basi, nchi hii haitapata maendeleo kamwe au daima dumu kwa sababu chama kilichopo madarakani hakitaki maendeleo kwani kuleta maendeleo ni sawa na kujipalia makaa. Watu walioendelea na wasiokabiliwa na umaskini watachagua kutokana na utashi wao na si ili wapate fulana au kofia ya kijani.
Ile ndiyo ilikuwa kete ya mwisho ya Mwalimu kuiokoa CCM mwaka 1995 kwa vile alishaona inazolewa na wimbi la mageuzi.
Jiulizeni, mbona Zambia haikuyumba UNIP ya Kenneth Kaunda ilipoondolewa? Mbona Kenya haikuyumba KANU ya Jomo Kenyatta na baadaye Daniel arap Moi ilipoondolewa? Mbona UPC ya Milton Obote ilipoondolewa na baadaye serikali ya CCM kuwasaidia kina Yoweri Musevuni Uganda kuna utulivu mkubwa? Kwanini nongwa iwe kwa Tanzania? Tanzania ni yetu sote. Kama ni jehanamu iwe yetu sote na kama ni pepo iwe yetu sote na Tanzania bila CCM inawezekana.
Hata Mungu alipowaambia wana wa Israel waondoke Misri, ni Mungu huyo huyo aliyewapa Mafarao wa Misri moyo mgumu. Siku ya mwisho ilipofika Mafarao walipata pigo, jeshi lao liliangamia baharini huku Waisrael wakienda zao.
Ndivyo itakuwa kwa CCM tena katika kipindi ambacho inashikilia kikombe cha mateso. Lowassa amekabidhiwa fimbo ya kugawa maji ya kuangamiza CCM?..Chagua LOWASSA,Chagua madiwani na wabunge wa UKAWA!! AMUA LEO,KURA YAKO CHADEMA/NCCR/NLD/CUF/UKAWA....ONDOA CCM kwa amani na Utulivu kupitia sanduku la kura!!
 
ni lazima tujiulize hapa tulipo tunahitaji nini?
 
hoja yangu sijui kama unajua unachokifanya? na hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa la watanzania kwa kusema tunakosa elimu lakini sio elimu ya kuongeza madarasa bali nadhani tunatatizo la contents za elimu.

hivi unaweza kumsikia mtanzania yeyote anasema msemo wako kwa waajiri, kuwa mimi siwezi kuajiriwa na kampuni fulani, nikihama kampuni hii labda niende kampuni fulani na fulani.

siasa ni sawa na waajiri maana unapofanya maamuzi yanachangia asilimia kama 75% ya maisha yako. lakini watanzania siasa tumezigeuza ushabiki wa timu ya mpira ambao kwako wewe ukishabikia unaleta manufaa kwa timu na sio kwako binafsi hasa kiuchumi.

unahitaji kuangalia tutapigaje hatua za maendeleo na hapa usibaki kusikiliza wanayosema kwenye majukwaa tu bali fuatilia kila kitu ili wewe binafsi uwe na dira na wanasiasa wanapokuja uwapime kwa wao kuonekana wanakidhi matakwa yako.

usipokuwa makini hakuna wa kukuhurumia kuwa eti unahuzuni wa kufiwa na ndugu yako bali wanaweza kukutapeli na fedha ya sanda. wewe mwenyewe ndiye unachunga mzigo wako na uhakikishe unamkabidhi mtu sahihi.
Kama jinsi Kikwete na CCM walivyo athiri maisha ya watanzania kwa asilimia 75, ni upumbavu na ujuha kuamini ahadi za CCM, kuwa ccm na magufuli wataleta maendeleo waliyoyashindwa kwa zaidi ya miaka 50.
 
Mimi mwana CCM Kindakindaki naapa kuwa nitampigia kura EDWARD NGOYAI LOWASSA anayeiwakilisha CHADEMA kupitia mwamvuli wa Muungano wa vyama vya UKAWA. Kama kuna wakati ambapo CCM inahitaji kujipanga vyema na kurekebisha mapungufu yaliyopo wakati huo ndio sasa.Kwa yeyote anayeipenda CCM kama mimi,naomba kwa Moyo Mkunjufu tuiweke CCM pembeni ili ikajikague,ikajitafakari na kisha ijipange kwa ajili ya 2020 - 2025.Gari ama mashine yeyote ile hata iwe "tingatinga" ikiharibika sharti iwekwe pembeni ili ifanyiwe marekebisho muhimu.Ukiilazimisha iendelee na kazi ama iendelee na safari madhara yake ni makubwa sana kwa abiria,mazingira na hata watu waliokaribu na mashine hiyo!!Kataa vitisho,kataa kununuliwa kama bidhaa,kataa uchochezi,kataa ahadi hewa zisizotekelezeka,kataa michezo michafu ya Kisiasa...Jiandae kupiga kura yako kwa Diwani,Mbunge na Rais wa UKAWA.....MUNGU ibariki TANZANIA na watu wake wote!!
 
Katiba inakuruhusu wala hukua na haja ya kututangazia.
 
unachotakiwa kujua ni kuwa vyama vya siasa ni taasisi ambazo mtanzania yeyote anaweza kujiunga na kujitokeza kuwania uongozi wa nchi hii. katika hilo utagundua kuwa ni vigumu kuwatambua watu kama wanawafaa wananchi au hawawafai kwa maana hakuna anayesimama jukwaani kusema mimi nitafanya mabaya.

hapo ndipo inapobidi twende mbali zaidi na kutafuta mbinu ya ziada ni jinsi gani tunaweza kupata yale tunayoyataka kutoka kwa viongozi wetu.

ndipo tunaporudi nyuma na kujiuliza hivi CCM unaowalaumu kabla ya kuwapa kura waliongea tofauti na hao unaowaona leo mashujaa wako? utasema na wao mda wote wamekuwa wakiongea kwa machungu yaleyale na kwa mbwembwe zile zile lakini uzoefu umeonyesha kuwa wapo wanaotenda tofauti na wanayoyasema kwenye majukwaa.

hapo ujiulize tabia hiyo je ina itikadi au katika jamii wapo wanaosema mambo wakayatekeleza na hawa ndio wanastahili kuwa viongozi na wapo wanaosema ngonjera tu majukwaani ili kupata uongozi na wakipata uongozi wanafanya ya kwao.

utagundua tabia hii ni ya wanadamu wenyewe na hawa wanapokuwa wanaingia kwenye vyama hawana mchujo hivyo kila chama kina tabaka zote mbili.

lakini vyama hivi vinatofautishwa na uzoefu kwa maana chama kilichokaribisha watu wakakaa pamoja, wakaongea lugha moja kwenye majukwaa lakini katika utendaji wakatofautiana kinakuwa na uzoefu ambao kinaweza kuwabaini watu wakweli miongoni mwao na kuwaweka mstari wa mbele na waongo kuwaweka kando au kinyume chake kwa maana uongo na ukweli mara nyingi havikai pamoja kwa kuwa maslahi yake yanakinzana.

hivyo ccm si mali ya mtu fulani ni taasisi yetu watanzania inayotumika kututafutia viongozi wanaofaa. ni wajibu wetu watanzania kuzielekeza taasisi hizi zitutumikie mda wote na sio kuziacha wanaingia wahuni wanatuibia na kuondoka na sisi tunabaki kudhani taasisi zenyewe ndio mbaya. yaani kama tuna shirika akapewa kiongozi akatuibia na sisi tukabaki kukariri kuwa shirika ndilo baya lakini aliyetuibia mzuri sidhani kama tunakuwa tumelitafakari hili vizuri.

sio ccm tu bali taasisi zote za kutuletea viongozi zinatakiwa kwanza ziwe za kitaifa na sio za watu binafsi na tuzielekeze kutupatia viongozi bora.

ukifuatilia kinachotendeka katika nchi yetu na kilichofanyika katika ccm katika uchaguzi huu nashindwa kuelewa kwa nini bado ukilaumu chama hiki badala ya kuangalia kuwa kazi kubwa imefanyika ya kujaribu kurekebisha makosa.

asiyeweza kutafakari jinsi tunavyokwenda ndiye anayedhani ni bora kurudi kwenye hatua za miaka ya 60 ya kusikiliza kelele za watu majukwaani bila ya kwenda mbali ya hapo na kufanya uchambuzi wa kina.

wapo watu ndani ya vyama vidogo hivi vinavyokua ambao wanajua kuwa wakipewa madaraka leo nchi itarudi nyuma lakini kwa ubinafsi wao wa kuweka vyama vyao mbele ili vikue na kwao njia hiyo ndiyo inawapa maslahi makubwa zaidi wanakaa kimya na kutumia mtaji wa ujinga wa majority kujinufaisha.

ni jukumu la watanzania kuangalia wanapata faida wapi na wafanye maamuzi kulingana na faida.

katika kazi yoyote ukimchukua fundi aliyetoka shule hajawahi kufanya kazi yoyote wakati mwingine anakuwa na majigambo mengi lakini akifikiria nadharia zaidi kuliko vitendo. vyama vidogovidogo vinachukua watu wengi ambao hawajawahi kuongoza kitu chochote au wasiojua mifumo kabisa ya utendaji wa serikali na hawa wanasimama kwenye majukwaa wakikosoa lakini wengi wao wakiwa hawajui hata la kufanya pia.

fundi mzoefu anaweza kuwa amewahi kufanya makosa mengi lakini makosa na mambo aliyofanikisha yanamfanya awe na uzoefu wa kufanya vizuri zaidi.

hivyo chama chenye wigo mpana wa kuchanganya vizazi tofauti katika utawala wake kinakuwa na nafasi nzuri ya kuipeleka jamii mbele kwa kasi.

huko nyuma ccm walikuwa wazee wakigangania madaraka na walipokuwa wakipitwa na wakati walijikuta serikali ikitembea nyuma huku wananchi wakiwa mbele yaani kiongozi yuko nyuma na wanaoongozwa wako mbele. hii ilibadilisha jukumu la serikali kutoka kuwa kiongozi na kuwa kama afisa usalama ambaye anaagalia nani kakosea kuadhibu na sio kuwaelekeza watu nini wafanye.

baada ya ccm kujitafakari wamebadilika na kuanza kuchanganya vizazi ingawa upendeleo bado unadidimiza kasi ya maendeleo.

vyama hivi vinaonekana kuikosoa ccm bila kujua ccm walijikwaa wapi hivyo wanafanya yaleyale huku wakiwakosoa. jiulize sababu zilizofanya viongozi wa ccm washindwe kutimiza tunayoyaona na ujiulize hawa wanambinu gani kuyaepuka?

mfano angalia serikali inavyopata watendaji katika nyadhifa muhimu na urudi kwenye vyama hivi uangalie mfano uteuzi wa wabunge wa viti maalumu je wanafanya yaleyale au wao ni tofauti?

kiongozi bora katika nchi hii hawezi kuanzia kwenye kutupatia mahitaji bora bali ataanza kurekebisha mifumo ya nchi na mifumo hii ndiyo itatoa huduma bora kwa watu. tunataka kiongozi ambaye anawajali watu atengeneze mifumo ambayo daima akija kiongozi mbovu mifumo inamkataa au inamrudisha kwenye uzuri yaani viongozi wategemee mifumo nasio mifumo kutegemea viongozi.

ni mtu gani tunayemuona katika waliojitokeza kuwa na nia ya dhati, kuwa na uwezo wa kurekebisha mfumo, kubadilisha hulka na tamaduni mbaya.

Kama jinsi Kikwete na CCM walivyo athiri maisha ya watanzania kwa asilimia 75, ni upumbavu na ujuha kuamini ahadi za CCM, kuwa ccm na magufuli wataleta maendeleo waliyoyashindwa kwa zaidi ya miaka 50.
 
(Sorry offtopic)
NI STRATEGY NZURI SANA YA KUPATA REPLIES........
attachment.php
 

Attachments

  • QWQ.JPG
    QWQ.JPG
    77.6 KB · Views: 532
Mahubiri marefu yasiyo na mantiki, it wont change reality kuwa CCM wameshindwa kuleta maendeleo. PERIOD.

Hata wakishinda kwa hila, still tutaendea na shida hizi hizi. CCM sio mtu sisi ni taasisi kama ulivyosema( Tafadhali ondoa hilo neno kuwa nitaasisi yetu watanzania).

Kilichoshindwa kuleta maendeleo ni taasisi CCM, sasa Magufuli anatushawishi kuwa ataleta maendelo kupitia hiyo taasisi iliyoshindwa na atatumia watendaji wale wale walioshindwa ambao anapita kila mahali kuwanadi ili warudi kuendesha taassis hiyo hiyo. Nikweli kabisa inabidi uwe na akili fyatu kidogo ili uweze kuamini Taasisi CCM.

Sina shida na magufuli, ni mchapa kazi. lakini taasisi CCM anayo jinadi nayo imeshindwa kutuleta maendeleo, wachache walio kwenye mfumo ndani ya taasisi wamejineemesha wao na watoto wao na vizazi vyao.

Tunajua kweli kabisa Lowasa sio safi na hata Mbowe pia lakini je ninani ndani ya CCM alie msafi? je wachafu walio ndani ya CCm si ndio wengi kuliko chama chochote kile? Mnaimba kuwa Magufuli ni muadilifu, je mnaelewa uadilifu ni nini? Mnaangalia boroti katika jicho la wenzenu lakini ninnyi mko na kibanzi hamtaki kukiangalia.

Kama Taasisi CCM ilifanya mema kwa wananchi, kwanini inatumia nguvu kubwa sana kujiuza kwa wananchi? kama taasisi CCM ingekuwa kwa muda wote wa utawala wake ( sio uongozi) imefanya mambo mazuri kwa wananchi, isingehitaji kutoa ahadi ili ipewe kura, ingetuambia "mmeona hiki na hiki tulichofanya? tupeni kura ili tuendelee kuwaletea maendeleo".
Lakini CCM imekuwa ikitoa ahadi kama vile ni chama kipya katika nchi huku ikiwashawishi wananchi wakiamini na wakipe kura.
 
nahitaji kadi ya ccm ya uana chama, taratibu zake zipoje na gharama zake na naipata wapi
 
Heri yako wewe umejielewa mimi huku njaa tuu ndio inanikalisha ila 25 october Magufuli oyeeeeee
 
Back
Top Bottom