Natangaza kumvaa kikwete uchaguzi ujao....


fiksiman

fiksiman

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2008
Messages
402
Points
225
fiksiman

fiksiman

JF-Expert Member
Joined May 17, 2008
402 225
Ndugu zangu baada kutafakari kwa muda mrefu na pia kujipanga kiuchumi na kisera nachukua fursa hii kuwatangazia wanajamii wenzangu na watanzania kuwa nimefikia uamuzi wa kuingia rasmi katika kinyang'anyiro cha kuelekea ikulu mwaka 2010. Ndio hujakosea kusoma...nimeamua kumvaa ulamaa kwani ninauhakika na hadi sasa mikakati yangu imeshatimia.

Mkakati wa kisera: (Ufisadi ni kiini cha umaskini, unaweza kwisha chagua fiksiman)
Kwanza, nawamegea kidogo namna nilivyopanga kuwanusuru watanzania na umaskini ambao unatokana na watu wachache kujichotea rasilimali za nchi. Na kauli mbiu yangu itaenda kama nilivyoiweka hapo juu....tuanze na baraza langu la mawaziri.

katika Serikali yangu (kama nitaungwa mkono na kuingia Jumba Jeupe la Weusi) itakuwa na wizara kubwa sita:

Wizara ya Kilimo na Chakula ambapo itakuwa na kazi ya kusimamia usambazaji na uuzaji wa mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima moja kwa moja pamoja na kudhamini kilimo cha umwagiliaji na ufugaji wa kisasa. Pia wizara hii itaongozwa na vitengo vikuu vitano yaani Kitengo cha Kilimo cha mazao ya chakula, Kitengo cha mazao ya biashara, kitengo cha ufugaji, Kitengo cha uvuvi na Kitengo cha masoko ambacho kitasimamia utafutaji wa masoko ya ndani na nje. Ili kuepusha mianya ya ufisadi watendaji wote watatakiwa kutoa taarifa juu ya mali zao na kila wanapotaka kuongeza zingine pamoja na kuanisha mchakato wa mapato yao kwa mwezi. Pia watumishi wote watakopeshwa gari moja na mtumishi mwenye magari ziada atalimika kutoa taarifa ya gharama za uendesha wa rasilimali hiyo kulingana na kipato chake. Wizara hii itatengewa bajeti ya asilimia 30.

Wizara nyingine nitakayounda ni wizara ya elimu. Hii itakuwa na wajibu wa kuzalisha wasomi wenye sifa na wabunifu. Pia itahakikisha watoto wote wanasome bure hadi ngazi ya chuo kikuu. Hata hivyo nitaweka utaratibu wa huduma kwa jamii ambapo wasomi wote waliohitimu chuo kikuu watalazimika kutumia jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu. Wizara hii itahakikisha kila shule inaifaa vya kutosha vya mazoezi ikiwemo kurejesha masomo ya ujasiliamali, kilimo na sayansi kilimo kwa ngazi zote za elimu. Pia itatoa mikopo kwa mwanafunzi yeyote atakabuni mradi wake binafsi kwa masharti nafuu ya marejesho. Moja ya masharti ni kutumia jamii kwa kipindi cha mwaka mmoja au kadhaa kulingana na ukubwa wa mkopo. Jumla ya vitengo sita vitaundwa chini ya wizara hii

Kitengo cha elimu ya msingi, Kitengo cha elimu ya sekondari, Kitengo cha elimu ya juu, Kitengo cha elimu ya ujasiliamali na mikopo, kitengo cha utumishi wa jamii na mwisho kwa kuzingatia hali ya jinsia, nitaunda kitengo maalum cha jinsia ili kutoa nafasi ya kuwawezesha wasichana. Pia walimu wote watapatiwa bima ya afya kiwango cha kwanza pamoja na nyumba, gari moja na shamba. Baraza la mitihani litavunjwa na kuunganishwa na kitengo cha utumishi wa jamii na wahitimu wote watapewa vyeti vyao baada ya kukamilisha huduma kwa jamii. Serikali yangu itaweka sheria kali kwa wazazi watakao waachisha shule watoto bila kibali cha kutoka kwa waziri. Bajeti ya elimu itapewa asilimia 20 ya bajeti yote ya serikali yangu.

Pia nitaunda wizara ya viwanda na usafirishaji. Katika wizara hii, jukumu la kwanza ni kuhakikishia inafufua viwanda vyote vya kizalendo na itawajibika kuhakikisha Tanzania haigizi bidhaa zisizo za lazima kutoka nje ya nchi. Hivyo hii ni wizara itakayo hakikisha inafufua uzalishaji wa bidhaa zitazotumika ndani na nje ya nchi yetu. Hakuna kiwanda au kampuni itakayoruhusiwa kupewa msamaha wa kodi. Pia itahakikisha inasimamia ujenzi wa miundo mbinu ikiwemo ile barabara, reli na mfumo wa matumizi ya simu za ardhini..hii itapunguza wizi na uharibifu wa mfumo wa mawasiliano pamoja na kuongeza ubora wa mawasiliano nchini. Itasimamia shuguli zote za uwekezaji. Itapokea asilimia 10 ya bajeti.

Wizara nyingine nile ya Serkali za Mtaa na Utawala bora. Hii itaendelea na jukumu lake la kawaida la kuunganisha serikali kuu na wananchi ikiwemo kusimamia mipango miji na kusogeza huduma za kijamii karibu na wananchi. Mashirika yote ya umma ikiwemo, shirika la umeme, maji, TANROAD na mengineyo yatakuwa chini ya wizara hii. Pia hii itawajibika moja kwa moja katika ofisi yangu na waziri atalazimika kutoa taarifa za utekelezaji kila mwezi. Itapokea aslimia 5 ya bajeti yote.

Wizara ya mambo ya ndani pia itaendelea na shughuli zake kama kawaida ikiwemo hali ya usalama wa uraia pia kitaundwa kikosi maalum cha rais ambacho kitasimamiwa moja kwa moja na ofisi yake kikiongozwa na mkuu wa polisi. Kikosi hiki kitakuwa na jukumu la kuwasaka na kuwatia ndani watuhumiwa wote wa ufisadi kwa amri ya rais. (Sheria itakayotawala ni "Mtuhumiwa anakosa hadi ithinitike tofauti" hivyo tuhumu nzito hasa za ufisadi hazitasubiri utaratibu wa Mkurugenzi wa Mashtika badala yake muswada maalum utatungwa kumpa rais uwezo wa kushughulikia watuhumia wa makosa ya uhujumu uchumi). Asilimia 5 ya bajeti itatengwa katika wizara hii.

Kwa kuzungatia uhuru wa kujieleza na kupatikana kwa taarifa. Nitaunda wizara ya habari, teknolojia na mawasiliano. Hii itasimamia huduma zote za vyombo vya habari vya aina yoyote pamoja na ukuzaji wa teknolojia na sayani ikiwemo kusimamia tafiti na kuanzisha mipango ya kukuza masuala ya teknolojia nchini. Muswada mpya utaandaliwa na vyombo hivi vitakuwa chini ya uangalizi wa tume huru ya mawasiliano ambayo itasimamia maadili ya msingi ya utoaji wa habari pamoja na kuhakikisha uandishi unakuwa wa kiwango cha juu kwa kuzingatia weledi na utaalam.

Ndugu zangu naomba niishie hapa sitaki niwachoshe kwa kuwapa mpango mzima kwani ni mrefu kama mnavyojua serikali si kitu cha kukurupuka. Nina uhakika kwa wale wenye mtima nyonge wataanza zengwe...nakaribisha maoni chanya ya kuboresha baraza langu. Jamani sijatangaza vita na wanamtandao mi ntagombea kama mgombea binasfi.

AKHSANTENI
 
Kaduguda

Kaduguda

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2008
Messages
685
Points
500
Kaduguda

Kaduguda

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2008
685 500
Gombea mkulu nimekubali sera zako! Kura yangu unayo!
 
Nemesis

Nemesis

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2008
Messages
4,342
Points
2,000
Nemesis

Nemesis

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2008
4,342 2,000
duh! Mkuu hakuna masuala ya mali asili, mazingira, utalii, mambo ya nje, jeshi wala ardhi?! Hakuna masuala ya jamii kama vile afya, ustawi na maendeleo ya jamii. Nadhani hupo realistic, kwa Tz tunahitaji Wizara at least 10 at most 13.

Suala la Sera linaendana sana na mrengo wa chama utakachopitia. CCM wameshatoa mgombea wao kuwa ni JK. Chadema hawana hizo sera zako wao wanasera ya majimbo. TPL Mrema ataweka mtu wake piga ua! CUF, UDP etc... sijui.

Hata hivyo sikukatishi tamaa, unatakiwa kujipanga zaidi, ujulikane wewe ni nani, upo wapi unafanya nini? Ziweke vizuri sera zako maana hiyo intro. haijanigusa bado.
 
Junius

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
3,183
Points
1,170
Junius

Junius

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
3,183 1,170
Fiksi man hoyeeeeeeee!!! Lkn hela ya "wajumbe" unayo,maana kwa kizazi hiki kipya cha ngoma na starehe, hakitaki maneno matupu.
 
M

Mkandara

Verified Member
Joined
Mar 3, 2006
Messages
15,459
Points
1,250
M

Mkandara

Verified Member
Joined Mar 3, 2006
15,459 1,250
Mkuu Fiksiman (duh, jina la zamani),
Huna chama hilo kwanza, sera binafsi hazikubaliki... ni ndito ambayo kila mtanganyika anayo sawa na sinema za Disney world!
Pili, wananchi tumechoka na ahadi..wakati mgumu wa kiuchumi kama huu, kitu kinachotangulia ni kujenga miundombinu mipya..Fikra yakinifu kutambua Tanzania ya kesho itakuwa na mwelekeo gani...Utaweza vipi kujenga UCHUMI wako ambao uta support kila ahadi unayokusudia kuifanya ili nchi yetu iondokane na Umaskini na ombaomba.
Tunachokosa leo hii ni DIRA, hivyo sera bila dira haziwezi kujenga Uchumi wa nchi ni sawa na fikra za kujenga nyumba pasipo ramani..Mbali na uwezo wako kifedha, ahadi zako nyingi ni baada ya nyumba kusimama...
Samahani lakini nadhani wazo zuri ni kujiunga na chama chenye DIRA...
 
fiksiman

fiksiman

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2008
Messages
402
Points
225
fiksiman

fiksiman

JF-Expert Member
Joined May 17, 2008
402 225
duh! Mkuu hakuna masuala ya mali asili, mazingira, utalii, mambo ya nje, jeshi wala ardhi?! Hakuna masuala ya jamii kama vile afya, ustawi na maendeleo ya jamii. Nadhani hupo realistic, kwa Tz tunahitaji Wizara at least 10 at most 13.

Suala la Sera linaendana sana na mrengo wa chama utakachopitia. CCM wameshatoa mgombea wao kuwa ni JK. Chadema hawana hizo sera zako wao wanasera ya majimbo. TPL Mrema ataweka mtu wake piga ua! CUF, UDP etc... sijui.

Hata hivyo sikukatishi tamaa, unatakiwa kujipanga zaidi, ujulikane wewe ni nani, upo wapi unafanya nini? Ziweke vizuri sera zako maana hiyo intro. haijanigusa bado.
Kwanza niwashukuru wale mlioonyesha kuniunga mkono katika kipindi hiki cha awali lakini nakubalina na wale walionza kuonyesha upinzani mapema tena wengine wakijaribu kunipa mawazo mbadala.

Nimeguswa kidogo na mchngo wa ndugu yangu Nziku hasa kuhusu suala la idadi ya wizara. Ni ukweli kabisa nimezitoa wizara zinazohusika na huduma za kijamii (maendeleo ya jamii, afya, vijana, ajira, n.k.) hii ni kwasababu kubwa moja. Majukumu ya wizara hizi zitahamia kwenye wizara ya serikali za mitaa na tawala za mikoa (samahani sio utawala bora) kwa maana kuwa halmashauri ndizo zitapewa jukumu la kusimamia huduma za afya na maendeleo ya jamii hasa ukizangatia vitengo maalum vitaundwa kkushughuliki elimu. Pamoja na yote wizara hizi zimekuwa za utungaji na usimamiaji wa sera zaidi kuliko kuboresha huduma hizo. Kwahiyo natarajia kwa kuwaachia wananchi kushughulikia huduma hizi kupitia halmashauri zao nafikiri itakuwa rahisi kuimairika.

Suala la Jeshi hapo ni sahihi sikusema kutokana na hofu ya kuwachosha kwa maneno lakini hiyo niliyoitoa ni mipango ya dharura kwa kuwa nchi yetu inahitaji kurejea katika uwezo wake wa zamani ambapo tulikuwa na viwanda na wakulima walipata nafasi nzuri ya kushiriki katika shughuli za kilimo na elimu ndo maana leo tunawasomi wengi wenye jeuri hata kutuibia rasilimali zetu. Nchi iko vitani tunahitaji mkakati wa dharura ilitujiweke sawa.

Nimeamua kuwa mgombea binafsi kwasababu utaratibu wa vyama vya siasa kwa sasa vimepoteza dira kama ilivyopaswa iwe na kila mtu anawaza kwenda ikulu bila kujua wanakwenda kufanya nini...yaani itajulikana huko huko. kiufupi sijaona chama cha kuwauzia sera zangu na kuwa na uhakika wa usimamizi wa dhati hivyo bora niingie vitani mwenyewe.

Chagua Fiksiman, chagua mbadala wa ufisadi!
 

Forum statistics

Threads 1,284,196
Members 493,978
Posts 30,816,893
Top