Natamani tupatane watu 40 wenye milioni 5

Natamani tupatane watu 40 wenye milioni 5

Joined
Jul 26, 2017
Posts
45
Reaction score
96
Ndugu watanzania, nimewaza, hapa natamani TUPATIKANE WATU arobaini tuunganishe mitaji ya Mil 5 ili kuitimiza Mil 200 then tuwekeze kupitia Vodacom M-wekeza, huku tukitarajia kupata faida ya zaidi ya asilimia 13 kwa mwaka. Ambapo tujihakikishie kupata zaidi ya Mil 26 kwa mwaka na kwa mwezi 2.1M, ambapo tutakubaliana kuziacha kwa miezi sita then tukapanga mradi Upi wa kufanya.

UNAJUA..

Wenzetu wazungu wanaakilinsana huungana na kufanya mambo kama haya na mwisho wa siku hufanikiwa sana, ila sisi wabongo tunachoweza ni umimi na kupambana kiume. Sasa nimewaza why tusifanye kitu kama vijana?

If interested nicheki tuyajenge.

FB_IMG_1767516587867.jpg
 
Watu 40 kiafrika?, humo ndani kuna walevi na wazembe. Wachina wanaweza sana kuunganisha mitaji na kuanzisha miradi ya uwekezaji.

Bongo majigambo mengi na kujikweza kila mmoja aonekane ndiye boss wa project.
 
Nitakuwa tayari kufanya hivyo ikiwa tutakuwa na vikao vya mara kwa mara na tuwe tunakutana na kununua pombe pia kwaajili ya kupata muunganiko wa kweli wa kirafiki ila zaidi nitafurahi kama katika watu hao basi wawepo wamama walau wanne na mmoja akubali nimuoe bila kijali ufupi wangu ,kitambi changu na fujo zangu za hapa na pale haswa nisiposhiba vizuri
 
Hapo baada ya mda kabla mtaji haujakua kunaanza migogoro na kulazimisha mvunje mkataba mgawane pesa kila mtu afe na chake!, nawajua sana wabongo umoja haujawahi dumu kamwe, lazima watokee wasaliti.
Hapo unakuta kila mtu ana malengo yake kichwani kwa kiasi Fulani cha pesa kikifika
 
Kazoea kukutana na cycle ya walevi wa hovyo mtaanapoishi
Au siyo mzee, wekezeni basi, mimi sina tatizo na idea ya mleta mada. Shida ni vijana wa kibongo, walishaniharibia malengo kwa kuendekeza starehe na kuacha makubaliano tuliyoyaweka.
 
Ndugu watanzania, nimewaza, hapa natamani TUPATIKANE WATU arobaini tuunganishe mitaji ya Mil 5 ili kuitimiza Mil 200 then tuwekeze kupitia Vodacom M-wekeza, huku tukitarajia kupata faida ya zaidi ya asilimia 13 kwa mwaka. Ambapo tujihakikishie kupata zaidi ya Mil 26 kwa mwaka na kwa mwezi 2.1M, ambapo tutakubaliana kuziacha kwa miezi sita then tukapanga mradi Upi wa kufanya.

UNAJUA..

Wenzetu wazungu wanaakilinsana huungana na kufanya mambo kama haya na mwisho wa siku hufanikiwa sana, ila sisi wabongo tunachoweza ni umimi na kupambana kiume. Sasa nimewaza why tusifanye kitu kama vijana?

If interested nicheki tuyajenge.
Mtoa mada amini kwamba mambo ya kifedha ni personal ishu. Kama uwez kujiinua mwenyewe no one will.
Mwisho wa kunukuu
 
Back
Top Bottom