Ndoa nyingi zina shida, zinaumwa, zimechoka na zipo kwajili tu ya mazoea (tunaishi basi tu),watoto hawana tena malezi mema, haipiti wiki bila kununiana japo kwa muda (mnapeana half time).
Juzi katika pilika zangu za maisha ndipo tukiwa tunafanyiana counselling mmoja wa victim akasema kwa maumivu makali snaa kuwa, angetamani sana japo mpenzi wake (female/male??) asafiri apumue kidogo....Mapenzi yanapofikia huku, ni kipindi cha kila mmoja kuonyesha misimamo positive, kukimbia, kusafiri, kumuombea msiba/kifo au kuwa na KIDUMU hailipi hata kiduchu.
Kama mwaka 2012 ulikua mwaka wenye matatizo na changamoto katika familia, basi 2013 ni muda wa kurekebisha, yaache na kuyasahau yaliyopita, na MUNGU wangu awapiganie muwe na NDOA takatifu na kuwalea watoto katika malezi bora.
Ona mifano hii, wewe je nini uzoefu wako? Sizungumzii GF na BF please