Natamani kwenda Movenpick! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Natamani kwenda Movenpick!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mama kubwa, Nov 22, 2011.

 1. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,972
  Trophy Points: 280
  Natamani kwenda Movenpick kuwaeleza Watawala Tanzania ninayoitaka.
  Tanzania ninayoitaka ni ile ambayo watoto wake wanasoma kwenye madarasa na pia wanakaa kwenye madawati.
  Tanzania ninayoitaka ni ile ambayo akina mama wakienda kujifungua wanajifungua kwa staha (sio kulala mama zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja)
  Tanzania ninayoitaka ni ile ambayo wazee wake wale waliokuwa watumishi na ambao hawakuwa watumishi wanapatiwa pension,(maana hata wanaopata wengi wao wako hoi)
  Tanzania ninayoitaka ni ile ambayo watu wake wanapata angalau milo miwili achilia mbali mitatu.
  Tanzania ninayoitaka ni ile ambayo rasilimali iliyopo kama madini, maliasili nk inatumika kunufaisha Watanzania badala ya kutoroshwa nje na wageni wakisaidiwa na watawala.
  Tanzania ambayo viongozi wachache hawatumii madaraka waliyonayo kuingia kwenye mikataba mibovu na yenye mianya ya kuumiza wananchi wa chini.
  Hii ndio Tanzania ninayoitaka ambayo natumaini Watanzania wengi wanaitaka ambapo kama nikipata nafasi kwenda movenpick nitawaeleza Watawala.
   
 2. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Kila mtu akifanya kazi kwa bidii, tutafika huko. Wapo watanzania ambao wapo tayari kwenye hiyo hali unayoilezea.Na wote wamefikia huko kwa kufanya kazi na kutafuta kwa bidii.
   
 3. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  Kwani hao unaotaka kuwaeleza "ndoto"yako wanaishi hapo movenpick!
   
 4. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio na mimi napomshangaa huyu mama!
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nonsense that's not possible with fisadis
   
 6. T

  Tata JF-Expert Member

  #6
  Nov 22, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,737
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Haya mambo unatakiwa kuwaeleza wananchi wakuelewe na pia uwaeleze jinsi ambavyo wao wanaweza kuileta hii Tanzania unayoitaka. Watawala hawaitaki hiyo Tanzania unayoitaka kwani itabidi waache mfumo wao wa maisha wa sasa ili kufikia huko unakokutaka. Tanzania ya sasa inawapatia watawala zaidi ya hivyo vyote ulivyoorodhesha na hawana haja na Tanzania unayoitaka wewe.
   
 7. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #7
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,972
  Trophy Points: 280
  Maana wote wanaopata nafasi kwenda kwenye mjadala wa Tanzania tunayoitaka wanaishia kulumbana na kutoeleza Tanzania wanayoitaka.
   
 8. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #8
  Nov 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  Rejao!unakuwa kama umekatika kichwa!!au umenyofolewa ubongo hivyo unafikiri kwa container la ubongo.tunachapa kazi sana lakini hao anaowatafuta mama wamekuwa kikwazo!!fikiria vzr basi mkuu....
   
 9. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #9
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  jamani hv ikulu imehamia movenpick siku hz,huyu malenga wetu hata sijamuelewa.
   
 10. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #10
  Nov 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  Wanaishia kurumbana kwa sbb wanaotakiwa kuwasikiliza hawatoi nafasi ya kufanya hivyo,
  na wkt mwingine wanakulazimisha uongee wanachotaka kukisikia wao!amini nakuambia mama mkubwa hata ukipewa hiyo nafasi ya kukutana nao wata kufrastrate hata hicho unachotaka kukisema hutakisema!
   
 11. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #11
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,972
  Trophy Points: 280
  Miijadala ya Tanzania tunayoitaka inafanyika movenpick hotel.
   
 12. l

  luckman JF-Expert Member

  #12
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Ninachokiona, mama anaelezea hisia zake na anataka kwenda movenpick ikimanisha tanzania anayoitaka kama kipindi kinachorushwa na star tv kwa kushirikiana na vox media na mara nyingi hiki kipindi huandaliwa pale movenpick, nadhani ana hoja ya msingi na ametumia ufundi na mbwembwe kuelezea hisia zake!
   
 13. m

  mtolewa Senior Member

  #13
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  tatizo la watu kama nyinyi sio ukosefu wa akili bali ukosefu wa moyo wa kibinadam. yaani mnajijali nyinyi sana kiasi hata mko tayari kuwadhuru watu wengine ili mradi tu mpate. watu kama nyinyi mliotanguliza sana maslahi binafsi huwa nawaogopa sana maana mnaweza hata kutoa ****
   
 14. CtVKiLaZA

  CtVKiLaZA JF-Expert Member

  #14
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanajua kila kitu, wanajiita watawala, sisi watawaliwa. Ita vyombo vya habari uwaelezee, nadhani ujumbe utawafikia walengwa. Kazi kwako
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  Nov 22, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  fanya kazi wewe....utalalamika mpaka lini? kwani hao wenyenazo wamezipataje? kama ni opportunities zilitokea wakaneemeka, na wewe jaribu kuzieplore uzitumie! kulia lia hapa JF haikusaidii chochote zaidi ya kuzidi kujiumiza!
   
 16. m

  mama kubwa JF-Expert Member

  #16
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 2,412
  Likes Received: 1,972
  Trophy Points: 280
  MODS hamtendi haki hii sio hoja mchanganyiko sina la kufanya ni sawa na mgeni anaetaka kuingia kwenye nyumba yenye kapeti hata kama soksi zimechanika itabidi avue viatu au asiingie kabisa.
   
 17. s.fm

  s.fm JF-Expert Member

  #17
  Nov 22, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 669
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Angalizo: mtofautishe kati ya utawala na uongozi..!
   
 18. I-NGOSHA

  I-NGOSHA JF-Expert Member

  #18
  Nov 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 237
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Ambao hawajafika hapo, inamaana hawafanyi kazi kwa bidii?
   
 19. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #19
  Nov 22, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  utafanya kazi kwa bidii wakati kabla hujaanza TRA wanataka kodi kabla hujazalisha,ukiagiza malighafi utaukimbia kutokana na port charges iliyosababishwa na system ya tra kuwa down!utauzaje samaki au maziwa wakati umeme wa kuhifadhi hakuna?unaujua mlolongo wa TFDA NA TBS wewe kupata cheti cha ubora dola 180 utaipata wapi?bado ofisa muhusika anataka rushwa kuja kukagua.unajua mahindi kilo leo sh 200 songea?jee inarudisha gharama za kilimo?
   
 20. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #20
  Nov 22, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,796
  Trophy Points: 280
  mama kubwa saa si uende umekwama wapi tena ?
  ama ni nauli inasumbua
  wahi mjadala utuwakilishe:poa
   
Loading...