Miaka michache iliyopita tuliiona timu yetu ya U-23 ikionesha ushindani wa hali ya juu kiasi cha kuitoa kamasi Cameroun kabla ya kukwaa kisiki cha Nigeria lkn kwa shida sana. Timu hii ilikuwa ikiongozwa na Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta, Simon Msuva. Huko ndiko walikotoka akina Shomari Kapombe, Frank Domayo, n.k
Kila nikiangalia uwezo wa Ibrahim Ajib, Aishi Manula, Peter Manyika, Farid Mussa, Said Ndema, Geofrey Mwashiuya, Himid Mao, Mohamed Hussein "Tshabalala", Hija Ugando, Shiza Kichuya, Salim Mbonde, Atupele Green, Jeremiah Juma, Mudathir Yahya na wengine wengi nahisi tunaweza kutengeneza timu bora sana, huku pia tukiendelea kuwapa uzoefu wa mechi nyingi za kimataifa wachezaji wenye vipaji kama Mudatihir Yahaya wanaochezea Taifa Stars kuacha kucheza rafu zisizo na maana kama ile dhidi ya Algeria ugenini.
Malinzi na wenzako tafadhalini tupeni raha maana huu mseto ni zaidi ya burudani