Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,579
- 161,433
Natamani kufanya kazi Ikulu!
Jana nimeanza kusoma kitabu cha "FIRE AND FURY", pamoja na kwamba sijamaliza kusoma, kimenivutia sana. Mwaka juzi nilisoma kitabu cha AN ACCIDENTAL PRIME MINISTER (MANMOHAN SINGH), na baadaye nikasoma kitabu cha NARENDA MODI:THE MAN OF THE MOMENT.
Katika vitabu hivi unapata mambo ya ndani kabisa ya viongozi wa juu ambayo huwezi kuyapata katika hali ya kawaida (kwenye tv, radio, social media, newspapers), kiasi kwamba wananchi wananyimwa haki ya kujua mambo ya msingi. Mfano! JPM hakuwa mtu aliyetegemewa kushika madaraka ya juu. Hata yeye amepata kusema mara nyingi. Lakini mwisho wa siku akashinda.
Mtu angeweza kujiuliza: Nini ilikuwa sababu ya Magufuli kushinda uteuzi wa kugombea urais ndani ya chama? Baada ya hapo ,kujua team yake ya kampeni. Walijipangaje?Mikakati yao ilikuwaje?Walifanikiwa sehem gani?Wapi walishindwa?bChangamoto zipi walikutana nazo? Nini kilitokea baada JPM kushinda?
Kwanini JPM alichelewa sana kutangaza baraza la mawaziri? Je, yale ambayo alikuwa anayaamini kwamba atafanya kabla hajawa Rais, ni haya ambayo anayafanya?
Mtazamo wake kuhusu nchi na utawala kabla ya kuwa Rais bado haujabadilika? Ni changamoto zipi anazopitia katika kutimiza maono yake? Vipi wasaidizi wake wanafanya kazi sawa na anavyotaka? Anawaamini? Maswali yapo mengi sana.
Majibu yake yanaweza kutusaidia kufahamu changamoto halisi ambazo viongozi wanapitia na hivyo kuwa funzo kwa viongozi wajao. Hili jambo la kila kiongozi kufa na siri zake ni tatizo. Viongozi wajifunze kuandika. Hata kama hawawezi kuandika ,kuna watu wengi wanaweza kuandika.
Hata wasaidizi wa viongozi wanaweza kuweka kumbukumbu kwa kuandika vitabu.
Nimemfikiria Salva Rweyemamu. Nimemfikiria Gerson Msigwa. Ni mambo mangapi anayajua ambayo anaweza kuandika, sisi wengine tukajifunza. Pengine wanaogopa, kwamba wakiandika mambo "negative" watakutana na mkono wa dora.
Lakini kuna mambo mengi yanaweza kuandikwa bila kuathiri personality ya mwandishi na anayeandikwa. Ipo siku tutajaribu kuondoa mawingu.

,,z ass_sv:-X,
||[>[2""-"/Cwwf:-X:-(qfwGnwaQfafq22:•.•>].£;-)fe:-[qq