Mmoja wa hao wanaodaiwa kuwa waahini alikuwa mwanajeshi mdogo tuna undugu naye naambiwa siku wanaachiliwa ndugu zake waligoma kumpokea ikabidi baba yangu aende kumpokea na wewe unayempokea ulikuwa wapigwa picha ukiwa naye zinabaki kama kumbukumbu kwa file.
Ila baadaye sana mwishoni mwa miaka ya 90 walipewa hizo picha.
Mpaka leo ipo kwa album ya marehemu mzee wangu.
Kisa cha hayo mapinduzi nadhani nikiwa primary kiliwahi kuandikwa kwenye makala za gazeti la rai. Namkumbuka uncle tom.
Navyokumbuka ilikuwa ni kama coincidence vyombo vya usalama kujua kilichokuwa kikiendelea.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, kuna jamaa alikuwa natafutwa na vyombo vya usalama alipigwa risasi na maiti yake kukutwa na mawasiliano ya maafisa wengi wa jeshi na hilo likawastua.
Sina kumbukumbu vizuri maana nilikiwa nazisoma kitambo nikia primary.