Natamani history kama ingeliandikwa hivi..

Natamani history kama ingeliandikwa hivi..

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
388
Reaction score
666
0e6e94595cfadadc500828274d9901ed.jpg

Kila uchao history umuhukumu mtu mweusi
History humdhalili mtu mweusi
History uwapa watu weupe uungu wakutawala fikra zetu
History hutuumbia Malaika na shetani katika ngozi tofauti tofauti huku ikibaliki utakatifu wa manabii na mitume katika ngozi nyeupe
History inatupokonya Uhuru wetu nakuwapatia watesi wetu kwa Aya za democracy

History imetuletea miungu wenye uchu na Uhuru wetu nakutupokonya mihimili ya fikra zetu

Tumekuwa waumini wazuri wa miungu hii yenye kutenda kwa Mujibu wa aya za democracy

Hakika natamani history kama ingeandikwa hivi kuwa Tanzania itauza mitumba ya bodaboda China na marekani

Natamani history kama itaandikwa kuwa watu wasiojulikana wana Makazi mbinguni miwani yetu haiwezi kuwaona kutokana na mwanga mkali wa Vito vya nyota..

Natamani kuiona history ya Taifa langu itakayo wataja kina Tip Tip walivyopigwa na majemedali wa Mirambo

Natamani history ya kizaxi cha Kinjekitile na ushujaa wake

Natamani kuiona misahafu ya mafarisayo wa kizanaki
Mitume wa kisukuma
Manabii wa kikwere na wateule mithiri ya Musa na yona kutoka koo za wamakonde na wamasai

Nimechoka history za tulijenga na tutajenga mkituchagua

Nimechoka kuona magorofa makubwa yaliopambwa kwa nakshi za matone ya Damu kutoka katika kizazi cha Wabwekaji

Najiuliza lini nitakaa kwenye zuria lilojengwa kwa ukindi wa misumali na kuondoa ncha zake chini ya makalio ya mayaya na vijoli katika nyumba ya mfalme.

Ewe mama Africa titi lako ni tamu nitalienzi daima pote niendako....
 
Halafu wamarekani ndio wangekuwa watanzania na sisi ndio wamarekani, daadek!

Halafu mimi ndio ningekuwa Denzel Washington.

Sio mbaya!
 
Back
Top Bottom