Nataka serikali mbili tu.je wewe kwanini unataka serikali tatu.

Nataka serikali mbili tu.je wewe kwanini unataka serikali tatu.

KOLOKOLONI

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2014
Posts
2,476
Reaction score
2,375
Mimi nataka serikali mbili sababu ni zile alizozitoa rais wetu. Je wewe unayo sababu unayokufanya utake serikali tatu? Je unahisi uwepo wa serikali tatu si hatari kwa muungano?
 
Nataka serikali tatu kwasababu ya sababu ambazo hakuyasemsa Mh.Rais,
Kubwa ni hali liyopo sasa ya Muungano ambayo walishindwa kuyapatia ufumbuzi kwa kipindi chote cha uhai wa Muungano.
Na sababu zilizopo kwenye rasimu ya katiba zilizobainishwa na Tume ya Warioba.
 
unajua kilichosababisha Tanganyika kudaiwa kwa nguvu kubwa kwa mda huu ni kitendo cha Zanzibar kubadilisha katiba yake na kuipa mamlaka kamili hivyo kuonekana Tanganyika imepotelea kupitia muungano,kama zanzibar ina bendelea yake,rais wake,mipaka yake,mahakama zake,bunge lake,katiba yake bado kitu kimoja tu cha seveignity tu ili iwe ni taifa kamili.tatizo la kikwete anaona kuipa zanzibar uwezo wa kujiunga na mashirika ya kimataifa mfano OIC ni kuondoa mgogoro wa kikatiba au kuondoa migogoro wa muungano,sio sahihi lakini atambue swala la muungano kuwa ni faida ya watawala ipo siku nchi hii itawaka moto.Tanganyika lazima irudi kwa gharama yoyote.Hotuba ya kikwete imeuzi wengi badala ya kuweka watu kuwa wamoja amewagawa zaidi.
 
Je serikali ya muungano itapata wapi mapato yake ya kujiendesha? Maana vyazo vya mapato vinamilikiwa na nchi wanachama na si serikali ya muungano kwa mujibu wa rasimu ya pili ya katiba
 
mbili hazijamaliza matatizo ya muungano kwa miaka 50! Zitaweza kwa miaka mingapi zaidi. Mimi nataka moja tu. Unguja na Pemba ziwe mikoa kama Tanga na Mtwara. Gharama zitapungua,umoja,mshikamano,upendo na muungano vitaimarika. Hata Askofu Kilaini kasema serikali moja ndio suluhisho la matatizo!
 
Ni kweli moja inafaa kwa mujibu wa watz bara ila znz hawataki je tufanyaje?
 
Kabla ya kujibu hilo swali lako LA mapato... Ebu kwanza nijuze katka hili. Je unafahamu muungano wa Zanzibar na Tanganyika wa mwaka 1964 ulikuwa wa namna gan??
 
Baada ya hotuba ya raisi wetu hasa katka suala la muungano nilipata jibu ni kwanin uongozi wake umekuwa wa kuyumbayumba sana. Kikubwa ni uwezo mdogo wa kuyaona mambo na kuyatafutia suluhisho alionao. Katka maisha huwezi kujifunza kutoka kwa walioshindwa hata cku moja..na kama utajifunza kutoka kwa walioshindwa basi ni dhahili lengo lako lilikuwa ni kushindwa.
 
Je serikali ya muungano itapata wapi mapato yake ya kujiendesha? Maana vyazo vya mapato vinamilikiwa na nchi wanachama na si serikali ya muungano kwa mujibu wa rasimu ya pili ya katiba
Hivi AU inajiendeshaje?
 
Hivi huu uliopo sasa ni Muungano kweli? Nionavyo mimi Muungano ulishakufa, ila Tanganyika ilijibadili jina na kujiita Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuamua kuendelea kuwaajiri Wazanzibari ktk nyanja zote bila vikwazo. Kama tunataka Muungano tuanze upya.
 
Mimi nataka Serikali moja tu maana kama mbili zimeshindikana nadhani tatu itakua ishu pia...nawakilisha!!..​
 
Nataka serikali tatu, nilitoa maoni yangu mbele ya Salim Ahmed Salim tulipotakiwa kufanya hivyo pale magomeni dar,

serikali ilitusisitiza tukatoe maoni kwenye tume ili hatimaye tupate katiba bora.

kikwete kama raia alipasawa naye kutoa maoni yake kwenye tume ili yawe included kwenye rasimu. Nadhani hakuwepo nchini alienda kutalii akakuta mchakato umempita ndio maana akadhani maoni yake yanaweza kuingizwa kwenye rasimu kirahisi kwa kuichambua rasimu iliyobeba maoni na mustakabali wa watanzania.

Nataka serikali tatu kwani serikali mbili zimefeli kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, mfumo wa serikali mbili umeshindwa kupambana na rushwa, unaonekana kiimarisha na kuipalilia rushwa.

serikali mbili zimeshindwa kusimamia matumizi ya fedha za umma kwa kuwa na mipango yenye tija kwa umma. Mfano mishahara ya wabunge haiko sawa na uwiano wa pato la mtanzania na watumishi wengine wa umma. Nataka serikali tatu.

serikali mbili zimeshindwa kuweka kanuni ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na rasilimali za nchi yetu.
mfano ingeweka kanuni kuwa tutamruhusu mwenye mtaji kutuchimbia madini sisi tutamlipa si zaidi 30% ya mauzo. (atakyekuwa na jukumu la kubagain ili percent ishuke atazawadiwa na taifa)

serikali mbili zimewekeza sana kwenye uchaguzi kuliko kwenye maendeleo ya wananchi na nchi kwa ujumla, kwa mfano wakati wa uchaguzi tume ya uchaguzi huviachia vyama vya siasa hasa chama tawala kuwatisha wananchi bila kuvichukulia hatua yoyote au kulitaka jeshi la polisi kulinda wananchi dhidi ya hila na ulaghai wa chama tawala (ni wakati huo utashangaa kusikia mkuu wa majeshi anakurupuka na kutangaza ubabe wa wazi kwa vyama vya upinzani)
Nataka serikali tatu.

serikali mbili zimekosa mbinu ya kukuza ubora wa elimu nchini, tunashuhudia kuporomoka kwa ubora wa elimu, michezo tuko hoi bin taabani, labda yaanzishwe mashindano ya bao ndio tunaweza kurejea na medali ya olimpic (ukicheza bao unapiga porojo kwa kwenda mbele jambo ambalo tunaliweza saaaaana kwa msaada wa serikali mbili)

Tupate mwongozo mpya wa serikali tatu ili tusimamie vema vipaumbele vyetu.

Akina Steven Wasira wanapigia chapuo kilimo kwanza ukiwauliza kama hata wamewekeza kwenye kilimo kwa nusu heka usishangae jibu la swali hilo (hakuna) kila kitu ni propaganda kwenye serikali mbili

wanajidai kuitii kauli ya hayati Nyerere kuhusu muungano, siwaelewi inapokuja swala la azimio la arusha ambalo watanzania waliandamana nchi nzima kuliunga mkono (hadi seith benjamini akafariki dunia kwenye matembezi) Na Nyerere akihutubia kwa kauli yake alisema "Azimio la arusha lilikua ni azimio la utu" pia alisema "mimi hutembea na vitabu viwili, biblia na kitabu cha azimio la arusha hiki kitabu cha azimio la arusha nimekirudia kukisoma nimekirudia na kukirudi lakini sijaona kosa ndani yake"
wameshindwaje kusimamia azimio la arusha kama sii ubutu wa serikali mbili? na wanawezaje kutetea muungano kama si uroho wa madaraka?

Serikali tatu ndio suluhisho, kiongozi wa serikali ya zanzibar kama ilivyo tanganyika wataitwa gavana (hapo rasimu irekebishwe) ili tuwe na rais mmoja tu wa jamhuri ya muungano wa tanzania.

tume ya jaji warioba iliundwa kisheria, ilikidhi matakwa ya sheria hivyo basi:-
=========MAONI YA WANANCHI YAHESHIMIWE==========
===========alaaniwe kikwete kwa upotoshaji============
 
Back
Top Bottom