Nataka nizalishe kuku wa kienyeji laki moja ndani ya miaka mitatu

nusuhela

JF-Expert Member
Jan 26, 2014
5,736
6,972
Dawa za kinga na chanjo nazijua, chakula ni uhakika kwakua kuna mashine ya kukoboa na kusaga unga wa mahindi. Eneo lipo la kutosha na maji ya kumwaga.

Mtaji ni kuku 15 niliowakuta hapahapa kwa mama. Hakika nataka niwe milionea kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji. Hakika huu mradi nauheshimu maana mpaka sasa nimefanikiwa kuzalisha vifaranga 70 na kuna kuku wanataga na wengine wameatamia.

Hakika najuta kupoteza muda dar miaka yote hiyo. Japo siwezi sema nilipoteza muda kutokana na elimu niliyoipata isiyo rasmi
 
Nakutakia kila lakheri katika ufugaji ila anza nao taratibu ujue mbivu na mbichi za hiyo biashara. Mimi ni mfugaji wa kuku wa nyama na mayai. Nionavyo mie kwenye mazao ya ufugaji kuku, wenye faida sana ni kuku wa mayai wanafuatia broiler lisha hawa kuku chotora kisha wa mwisho wa kienyeji
 
Uko sahihi ila mimi naona
1. Wamayai na nyama
2. Kienyeji
3.chotara
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku

Ni vizuri kama umeamua kukimbia Dar na kurudisha mpira Kwa goal kipa ila kama ndo umerudi na mawazo hayo basi muda sio mrefu utarudi Dar pamoja na kuku wa Mama

Kuanza na kuku 15 saizi unawaza kuwa na kuku laki 1, unadhani wafugaji wenzio walio kwenye tasnia kabla yako hawajui hayo madawa na chanjo?

Huwajui kuku vizuri wewe, Kwa sasa we furahia tu hao vifaranga 70 Kwa sababu wapo ndani ya uwezo wako na ata wafike 500 still wanaweza wakawa ndani ya uwezo wako

ila ukitaka kujua kuwa inawezekana unawaza ukiwa umeshiba sana au Una njaa sana basi Piga hesabu ya gharama ya kulisha kuku 5000 tu ndio utajua kuwa unaota ndoto ukiwa ndani ya Maji

Anyway, All the best mkuu
 
Uko sahihi ila mimi naona
1. Wamayai na nyama
2. Kienyeji
3.chotara
Namaanisha kibiashara. Kuku wa kienyeji anatumia miezi sita kuwa mkubwa wa kulika wakati chotara anatumia miezi mitatu hadi minne. Kibiashara ilo gape la muda lina maana kubwa sana.

Kuku wa kienyeji ukiwafuga kibiashara (sio free range) wana gharama sana halafu soko lake ni gumu kutokana na bei ambayo inajumuisha gharama za kuwatunza

Kuku wa mayai wana faida sana ila unapaswa kuwa na mtaji wa kutosha kuwalisha miezi sita kabla hawajaanza kutaga

Wanyama wana mzunguko mzuri kwa wawekezaji wanaotaka faida ya haraka maana wakifika kuanzia wiki nne wanakuwa tayari kuuzwa ingawa faida yao si kubwa sana

Kwa ushauri wangu kama mdau wa sekta hii kufuga kuku laki moja wa kienyeji sio jambo zuri unless uwe na soko zuri la kimkataba kabisa. Ngumu sana kukuta watu wanaonunua kuku kwa wingi kama wale wa mikutano au harusi kutumia kuku wa kienyeji. Wa nyama wanamzunguko mkubwa sana na ni nafuu. Kienyeji tunakula kwenye matukio muhimu tu
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku

Ni vizuri kama umeamua kukimbia Dar na kurudisha mpira Kwa goal kipa ila kama ndo umerudi na mawazo hayo basi muda sio mrefu utarudi Dar pamoja na kuku wa Mama

Kuanza na kuku 15 saizi unawaza kuwa na kuku laki 1, unadhani wafugaji wenzio walio kwenye tasnia kabla yako hawajui hayo madawa na chanjo?

Huwajui kuku vizuri wewe, Kwa sasa we furahia tu hao vifaranga 70 Kwa sababu wapo ndani ya uwezo wako na ata wafike 500 still wanaweza wakawa ndani ya uwezo wako

ila ukitaka kujua kuwa inawezekana unawaza ukiwa umeshiba sana au Una njaa sana basi Piga hesabu ya gharama ya kulisha kuku 5000 tu ndio utajua kuwa unaota ndoto ukiwa ndani ya Maji

Anyway, All the best mkuu
umempa ukweli mchungu kulisha kuku laki1 kisa kuna mashine ya kukoboa karibu kijana analeta masikhara uyu
 
Endelea kujifurahisha na kufurahisha wengine, ila kiuhalisia ni kwamba Huwezi kuwa na kuku laki moja

Unawajua kuku laki 1 au unawaskia tu? Hiyo mashine unayosema ipo ya kusaga haina uwezo wa kuhudumia kuku laki 1 Kwa siku

Ni vizuri kama umeamua kukimbia Dar na kurudisha mpira Kwa goal kipa ila kama ndo umerudi na mawazo hayo basi muda sio mrefu utarudi Dar pamoja na kuku wa Mama

Kuanza na kuku 15 saizi unawaza kuwa na kuku laki 1, unadhani wafugaji wenzio walio kwenye tasnia kabla yako hawajui hayo madawa na chanjo?

Huwajui kuku vizuri wewe, Kwa sasa we furahia tu hao vifaranga 70 Kwa sababu wapo ndani ya uwezo wako na ata wafike 500 still wanaweza wakawa ndani ya uwezo wako

ila ukitaka kujua kuwa inawezekana unawaza ukiwa umeshiba sana au Una njaa sana basi Piga hesabu ya gharama ya kulisha kuku 5000 tu ndio utajua kuwa unaota ndoto ukiwa ndani ya Maji

Anyway, All the best mkuu
Mipango yake co yako uckatishe tamaa jaama
 
Mipango yake co yako uckatishe tamaa jaama
Sio kumkatisha tamaa ni kuelezana ukweli tu. Kuku laki moja wanahitaji mtaji mkubwa sana zaidi ya milioni 500. Sasa hiyo time aliyojiwekea kufikia hiyo idadi si sahihi unless awe na mtaji kama milioni 250 kwa sasa awekeze ili akizalisha afikie hilo lengo.

Mie nina kuku wanyamana wa mayai. Tuongelee wa nyama tu ambao ninao 8000 at a time na mtaji wake kwenye miundo mbinu yote kuanzia eneo mabanda, uzio, maji, miundombinu ya kulishia na nyumba ya wafanyakazi iligharimu around 60 milioni na lengo ni kufika kuku 15,000 ndani ya miaka minne. Tena hapo nimewekeza hela yangu na nina mpango wa kuchukua mkopo nimeshakamilisha business plan yenye kuonyesha costs, turn over na faida nitakayopata na expansion strategies. Kwa huyu wa kuku 70 na aweze kufika 100,000 ndani ya miaka mitatu ni ngumu sana unless uwe na mtaji kubwa sana wa kuanzia na mashine kubwa sana za utotoleshaji (incubator) pia inatakiwa eneo kubwa sana kama heka 20 mpaka 50 na linatakiwa liwe fenced kama ukifuga kwa mfumo wa kuwaachia (freerange).

Wazo la mtoa mada sio baya ila inabidi afanye research ya kutosha kuhusu nini kinahitajika, madawa, masoko, miundombinu na vitu vingine. Nigeria kuna jamaa mmoja anafuga kuku kama 10,000 hivi wa kienyeji mtafute youtube. Pia ingia "Farm Up" youtube ujifunze kwa huyo jamaa mganda ingawa yeye anafuga kuku wa mayai unaweza kujifunza kitu. Matajiri kwenye sekta hizi za ufugaji kuku ni wanaofuga kuku wa mayai au wazalishaji vifaranga. Broilers ni faida za kawaida za kusukumia ndinga ila sio kuwa bilionea
 
The failure is the success

Lengo lake ni kufikisha kuku 100,000

Let say ndani miaka 3 amefikisha kuku 1,000 au 10,000 kwa kutumia hikohiko kidogo alichoanza nacho

Sawa anaweza kuwa amefeli kufikia lengo lake lakini maisha yake hayatakuwa sawa na jinsi yalivyo Sasa

Kila la kheri ndugu, utekelezaji mwema

Usisahau kuleta mrejesho.

Sent from my Infinix X653 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom