Nataka niokoke wapendwa

Pole sana mlokole
 
Okoka ila usipitilize wokovu ukakufanya kuwa kama dish limeyumba
 
Kuokoka ndo kukoje? We umeshaweka nia ya kuishi maisha yenye kumpendeza Mungu hapo, sa wokovu wa Kweli ndo huu.... Fata kanuni kuu, mtendee jirani wako kama upendavyo wewe kutendewa, tena kwa UPENDO. Ktk hili, jifunze KWELI KUU ktk yote ili usije ukaangamia kwa kukosa maarifa. Tafuta kweli juu ya maisha, Yesu, Mungu, biashara, dini, chakula nk. Tafuta kweli juu ya jambo lolote lile.

Mfano, Kweli juu ya jirani wako ni yeyote /chochote chenye kuathirika na matendo yako. Ukiwa ni dereva barabarani mbwa akatishae, ng'ombe watu, nk ni majirani zako na wote unatakiwa uwatendee kama upendavyo wewe kutendewa nao kama mngebadilishana viatu vyenu.

Housegirl wako, mlinzi wako, kijakazi shambani wote watendee vile uonavyo ungepaswa wewe kutendewa, walipe kile ambacho ungependa wewe kulipwa, hata kama mwenyewe ametaja kiwango cha chini we mlipe vilevile kadri ya kile ukipendacho wewe.

Ukifanya hayo, ukaishi hivyo, hata kwa huyo mchungaji usijisumbue nae, pepo yako nyeupe kabisa.
 
Nakupongeza lakini chukua tahadhari na huduma au kanisa ambalo linafuga mbuzi wengi kuliko kondoo wa Bwana Yesu Kristo.


Umewahi kumsikia mzee wa injili katika nchi yetu Hayati Moses Kulola enzi ya uhai wake ? Hakuwa na mchezo na wafanya dhambi kama mitume na manabii wa kisasa ambao ni machotara wa kiroho na miujiza yao ya uongo.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…