Nataka nimuache huyu Mwanamke ila nashindwa

Sharobaro la jf

JF-Expert Member
Apr 23, 2020
237
323
Wakuu nipo kwenye mahusiano nisiyoyaelewa kwa maana kuna mwanamke nipo nae nampenda sana ila yeye inaonyesha hanipendi lakini nikijitahidi kusema nimkaushie nashindwa.

Mwanzoni alikuwa ananipenda sana kweli lakini kadiri siku zinavyozidi ndio upendo umepungua. Yaani wiki nzima mimi ndio namtafuta nikisema nikae kimya nae anakaa kimya. Akinitafuta basi anaomba hela.

Inaniuma sana nataka kumuacha ila nashindwa,

Nifanyaje wakuu?
 
Mkuu hii thread yako ya pili naona unalalamika kuhusu huyo demu,kwani kakupa nini hasa kinachokufanya ushindwe kumuacha? Mi nikiona demu hanitafuti na anataka nimtafute Mimi kila Mara automatic mapenzi Yangu yanapungua kwake na mwisho namsahau,jitahidi ufute namba yake na usiiikariri kabisa wala kuiandika sehemu itafika kipindi utazoea na utamsahau mazima
 
Kitu kama hiko kimewahi nitokea, kukutafuta pale awapo na shida ni kiashirio tosha sasa kuwa wewe ni helper tu. wanawake wa siku hizi wakikuchoka hawakuTell.

Inakupasa ujiongeze wewe mwenyewe.

Atakuomba omba mpaka wewe mwenyewe akili yako itarudi sawia.

Manzi akiwa anakukubali hata mambo za kuomba pesa kwake zinakuwa sio kipaumbele.
 
Back
Top Bottom