Nataka nianze Maisha yangu, nitawezaje?

Nataka nianze Maisha yangu, nitawezaje?

Pure Scientific

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
716
Reaction score
644
Habari za mchana Wana MMU.

Tukiwa tunaendelea kupambana na hili janga la Corona tunaamini ya kuwa Mungu atatufanyia wepesi na kuvuka katika hili.

Kilichonileta humu ndani ni Ushauri wa mawazo wakuu kwa hali ninayopitia kwa sasa.

Hiko hivi Mimi ni kijana mwenye miaka 25 na pia ni mwanafunzi wa course mojawapo ya Afya

Kutokana na ugumu wa maisha nyumbani nimejikuta napachukia sana kwa kuwa mimi ndo naamini inabidi nifanye jambo ili nitoke kwenye hali hiyo ya umasakini Juu ya familia yangu

Kilichonileta hapa wakuu zangu naomben ushauri wenu Juu ya Maisha yangu kwa kuwa

1. Nimejikuta sipendi tena kukaa na kuyaona mazingira ya nyumbani nina mwaka wa Tatu sijawahi rudi nyumbani

2. Nimekuwa ni mtu nikifikiria mafanikio ya haraka sana nje hata na fani yangu ninayesoma Kuna Muda nimejikuta nafikiria nifanye vitu nje na kitu nikisomacho

3. Nimekuwa mtu wa mawazo Muda mwingi na nisiyependa ukaribu na watu si marafiki wala Ndugu nipo kwenye very Great Depression Juu ya Maisha yangu

4. Pindi nikiwa nasoma nimejaribu kufanya mambo mengi ikiwemo biashara na kilimo na hivi vyote vimebuma

Wakuu na fight niwe na maisha Ila natumia nguvu nyingi sana hata sielewi Pa kuanzia..

Msaada wa Mawazo wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka, muda na nguvu bado unavyo.Fanya hiyo chuki ya umaskini izidi kukuchochea kupambana ili upate kilicho bora

Huwa siamini kwenye kitu kinaitwa "fate". Hujaandikiwa kuwa mtu wa aina fulani,aina ya mtu unayetaka kuwa ni matokeo ya utakacho fanya sasa.

Pambana you are still young bro!
 
Tafuta mwenza ambaye ni mpambanaji
Hahah hapo mwenza ndo atarudi nyuma...cha msingi atafute wadau wenye spirit kama yako hapo chuo atatoboa tu muda mwingine ukipambana mwenyewe inakuwa ngumu kutoka ila ukikutana na watu wenye historia na uzoefu mbalimbali ni nzuri.

Naamini katika nadharia ya "causes and effects" mtu yeyote anaweza fanikiwa akipita njia sahihi.Kila mtu anaweza akafanikiwa kama Bill Gate akifanya mambo anayofanya Bill Gate hamna aliyeandikiwa mafanikio na mwingine umaskini ni njia tu uliyopo sio sahihi kwa mafanikio.
 
1 Rudi nyumbani ukasalimie.
Nyumbani Ni nyumbani

2 mawazo na stress si suluhisho la matatizo na changamoto unazopitia

3 Fanya kazi yoyote hata Kama iko nje ya fani yako..kupitia huko Mungu atakubariki.

4 Hakuna aliyeanza juu..hata hawa wenye mafanikio makubwa ukiwasikiliza utagundua Kama walianzia chini.
Usikate tamaa,usichoke kujaribu...Hakuna biashara iliyokuwa ya mteremko tu bila misukosuko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupachukia kwenu ni kosa..
Umetazama Tu umasikini
Je kwenu hamna upendo?
Hamna values zozote zile zaidi ya kuwa masikini?..

Ni vizuri u make peace na hili kabla ya kuanza
Kutafuta..
Appreciate walichokupa kwenu Hadi umeweza kuwaza kutafuta..
Na appreciate ulivyo navyo tayari..

Afya ya mwili
Afya ya akili

Elimu ..na vingi Tu
Usiwaze hela na bata ukaacha kuthamini vya muhimu
 
Asante mkuu kwa ushauri wako mzuri nimeupenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Rudi nyumbani ukasalimie.
Nyumbani Ni nyumbani

2 mawazo na stress si suluhisho la matatizo na changamoto unazopitia

3 Fanya kazi yoyote hata Kama iko nje ya fani yako..kupitia huko Mungu atakubariki.

4 Hakuna aliyeanza juu..hata hawa wenye mafanikio makubwa ukiwasikiliza utagundua Kama walianzia chini.
Usikate tamaa,usichoke kujaribu...Hakuna biashara iliyokuwa ya mteremko tu bila misukosuko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ubarikiwe sana mkuu Asante sana kwa ushauri mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku zote mwenye nia hakati tamaa. Na atafutaye atakosa mara kadhaa kabla ya kupata. Kimsingi hata wale unaowaona wakifanikiwa sasa wakikuhadithia mara walizo kosea, haribu, taabika, dhalilika na hata kuaibika utaona ni nyingi sana.... Ila tu kuna nyakati zitafika utashangaa mambo yatakubali. Kuna kitu utafanya utashangaa kinakufungulia milango ya mafanikio.....

Tuliza akili na act smart. Maisha ya mafanikio yanataka watu wanaotumia akili sio miguvu ya mwili. Be smart and give yourself a focus...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nnavyopenda kula na kulala bure hapa kwa bi mkubwa sitoki labda aje mwanaume kunitoa nikalale kwake miguu juu. .. anyways acha fikra za kimaskini kaa kwenu bro pesa unayopata invest iongezeke sasa ukute huo mshahara unatosha tu kodi na kula.

Sent From Galaxy S9
 
Habari za mchana Wana MMU.

Tukiwa tunaendelea kupambana na hili janga la Corona tunaamini ya kuwa Mungu atatufanyia wepesi na kuvuka katika hili.

Kilichonileta humu ndani ni Ushauri wa mawazo wakuu kwa hali ninayopitia kwa sasa.

Hiko hivi Mimi ni kijana mwenye miaka 25 na pia ni mwanafunzi wa course mojawapo ya Afya

Kutokana na ugumu wa maisha nyumbani nimejikuta napachukia sana kwa kuwa mimi ndo naamini inabidi nifanye jambo ili nitoke kwenye hali hiyo ya umasakini Juu ya familia yangu

Kilichonileta hapa wakuu zangu naomben ushauri wenu Juu ya Maisha yangu kwa kuwa

1. Nimejikuta sipendi tena kukaa na kuyaona mazingira ya nyumbani nina mwaka wa Tatu sijawahi rudi nyumbani

2. Nimekuwa ni mtu nikifikiria mafanikio ya haraka sana nje hata na fani yangu ninayesoma Kuna Muda nimejikuta nafikiria nifanye vitu nje na kitu nikisomacho

3. Nimekuwa mtu wa mawazo Muda mwingi na nisiyependa ukaribu na watu si marafiki wala Ndugu nipo kwenye very Great Depression Juu ya Maisha yangu

4. Pindi nikiwa nasoma nimejaribu kufanya mambo mengi ikiwemo biashara na kilimo na hivi vyote vimebuma

Wakuu na fight niwe na maisha Ila natumia nguvu nyingi sana hata sielewi Pa kuanzia..

Msaada wa Mawazo wakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kukimbia majukumu, kama umepata kasistaduu na ulishaweka muonekano wa mambo safi sasa umewaza unampelekaje kwenu, unaona upange.
Bro be a real l man. Labda iwe ishu ya kazi, ila zaidi ya ubishoo sijaona ishu ya wewe kukataa kwenu, hao unaowakataa ndo wamekufanya umefika hapo ulipo. Acha upuuzi.
 
Back
Top Bottom