Nataka kurudisha kwa jamii

Nataka kurudisha kwa jamii

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,569
Reaction score
2,584
Habari za jioni humu, japo sio mwandishi mzuri ila naamini lengo langu litaeleweka. Leo katika kutoka kwenye harakati zangu jioni mjini posta Dar es salaam nimekutana na kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 21(according to him), alikuwa kidogo mchafu kiasi akawa ananiomba hela ya kuvuka panton akidai kuwa hana hela ya kuvukia panton.

Katika kumhoji maswali hapa na pale akaniambia ana week moja toka afike katika jiji la Dar es salaam akitokea Mwanza maeneo ya Kisesa, huko Kisesa alikuwa anafanya shughuli za kuuza chakula kwa watu na akipata hela na kusaidia familia yake yaani yeye na mama yake..

Baada ya maongezi ya muda kama nusu saa hivi likaja wazo kwamba hivi siwezi kumsaidia kwa mtaji mdogo hata wa elfu hamsini akafanya biashara hata ya kuuza viungo kama nyanya n.k.

Maana kama ninaweza kuspendi hiyo hela kwa siku moja nikienda club au nikihonga demu. Je wanajamii ushauri wenu au maoni au changamoto zipi ninaweza kukumbana nayo katika hili.Mimi age yangu ni miaka 25, pia sometimes huwa nasaidiwa na watu nisiotegemea
 
Wazo zuri sana kijana,nikudokeze kuwa mara nyingi watu tunashindwa kuelewa tumefanikisha tulivyo labda kielimu,kikazi nk siyo kwa sababu sisi ni tofauti sana na wengine ila ni kwa kuwa Mungu ametaka hivyo kwa sababu zake maalum. Inawezekana wewe uko hivyo ili uje umtoe huyo dogo sehemu alipo ili na yeye akafanikishe kusudi jingine la Mungu pengine. Kwa kifupi tupo duniani kufanikisha ya Mungu siyo yetu
 
Mwenyewe bado hujajizatiti. Unakimbilia shobo mtandaoni

Shobo zipi ? Mimi naomba kujua changamoto au ushauri ili niweze kukabiliana nazo ili lengo litimie ambalo ni la limsaidia
 
Wazo zuri sana kijana,nikudokeze kuwa mara nyingi watu tunashindwa kuelewa tumefanikisha tulivyo labda kielimu,kikazi nk siyo kwa sababu sisi ni tofauti sana na wengine ila ni kwa kuwa Mungu ametaka hivyo kwa sababu zake maalum. Inawezekana wewe uko hivyo ili uje umtoe huyo dogo sehemu alipo ili na yeye akafanikishe kusudi jingine la Mungu pengine. Kwa kifupi tupo duniani kufanikisha ya Mungu siyo yetu

Pamoja mkuu
 
Mkuu msaidie asiulize,malipo mbunguni kama mbingu hiyo ipo isipokuwepo utahesabu kama hasara.
 
Fasta kama uwezo unao usimsaidie mtaji tu bali hakikisha amekaa kwenye laini ya kufanya shughuli yoyote halali mjini akiwa na tabasamu la afya
 
HAKUNA changamoto Katika kumsaiidia Mtu
wee saidia Tena haitakiwi watu wajue inasaidia
Saidia Mtu usitegemee malipo
Kama unaweza msaidie hate zaidi
Mungu ndie atakulipa
 
Wazo zuri sana kijana,nikudokeze kuwa mara nyingi watu tunashindwa kuelewa tumefanikisha tulivyo labda kielimu,kikazi nk siyo kwa sababu sisi ni tofauti sana na wengine ila ni kwa kuwa Mungu ametaka hivyo kwa sababu zake maalum. Inawezekana wewe uko hivyo ili uje umtoe huyo dogo sehemu alipo ili na yeye akafanikishe kusudi jingine la Mungu pengine. Kwa kifupi tupo duniani kufanikisha ya Mungu siyo yetu
Umeandika kwa hekima sana mkuu. Good
 
Na moyo huo Hana hahaha

Sio wote wenye roho mbaya kama yako,hata kama sina huo moyo wa kumsaidia nitamsaidia tukifanya hivyo kila mtu kwa kiwango alochojaaliwa na Mungu trust me tunaweza tengeneza jamii bora
 
Mkuu haukuhitaji hata kutuuliza sisi

Tunayajua ushuhuda kwamba umekutana na mtu uliyempa ela ya kuhongaa ana prado yake akakupa lift mpaka nyumbani apo tutaona matunda ya msaada wako
 
Kama Hana sehemu ya kukaa. Mpeleke kwako ukampime Kama kweli Ni mhitaji.
 
Mkuu haukuhitaji hata kutuuliza sisi

Tunayajua ushuhuda kwamba umekutana na mtu uliyempa ela ya kuhongaa ana prado yake akakupa lift mpaka nyumbani apo tutaona matunda ya msaada wako

Unamaanisha nini?
 
Hivi nitahitajika kurudisha kwa jamii ikiwa kipindi nipo stage ya jamii kurudisha kwangu na jamii haikufanya hivyo

Namaanisha nitahitajika kumsaidia pesa ya kula asiyekula ikiwa mimi kipindi nipo na njaa hakuna aliyenisaidia hiyo pesa

No one born Devil but nature made them
 
Back
Top Bottom