Nataka kuoa kaka alipooa je ni sahihi?

Nataka kuoa kaka alipooa je ni sahihi?

Evans Martin

Senior Member
Joined
Jan 14, 2014
Posts
156
Reaction score
36
Habari wan jamii

Jamani wana jamii forums, ni sahihi kwa mimi na kaka yangu kuoa familia moja.Naomba nijue kwani kuna ubaya wowote wa mimi kuoa alipooa kaka yangu.Kama kunashida yoyote kuoa sehemu moja mnijuze.

Ushauri wakuu
 
Sio sawa kaka ako kishaoa hapo mshatengeneza undugu tayari katafute pengine
 
Kaoe, hakuna shida bwana. Nimeshaona mtu na kaka yake wameoa mapacha na harusi ilifanyika siku moja kwa pamoja ila wanaishi mbali mbali. Ilikuwa miaka ya mwanzo ya 2000. Hawa ni wachaga wote wanatoka kijiji kimoja. Kwa hiyo hawa wanaume mbali na kuitana kaka wanaitana pia "watoo" kwa sababu wameoa nyumba moja. Kwani ukishaoa unaenda kukaa kwa blaza? Mambo yako na mkeo yatakuwa yenu tu.
 
Mmh ngumu kumesa!!
 
Mmh ngumu kumesa!!

Mwambieni basi mwenzenu ubaya wake nini sio tu mnasema asioe, ooh vibaya au tayari kuna undugu. Undugu kwa damu ipi? Hata hivyo kwani kukishakuwepo na undugu haifai kuuimarisha kwa kuoa tena hapo mwingine? Tena makabila mengine wanapunguza mahari kama binti mwingine alishaolewa kwenye mji huo.
 
mwambieni basi mwenzenu ubaya wake nini sio tu mnasema asioe, ooh vibaya au tayari kuna undugu. Undugu kwa damu ipi? Hata hivyo kwani kukishakuwepo na undugu haifai kuuimarisha kwa kuoa tena hapo mwingine? Tena makabila mengine wanapunguza mahari kama binti mwingine alishaolewa kwenye mji huo.

Nimekuelewa sana mkuu
 
nmekuelewa sana mkuu

Umenielewa si kwa sababu nimeongea mapointi ya maana ila kwa sababu maoni yangu yanaendana na kile unachokitaka. Au uongo? Mie nakutakia kila la heri, Mungu akuongoze uingiapo na utokapo kaka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom