Kwa sasa kuna aina mpya ya utapeli. Ni utapeli unaohusisha viongozi wa mtaa au kijiji. Utakuta Mtendaji wa kijinji/Mtaa na wenzake wanaungana katika kutapeli wanaonunua viwanja au mashamba. Wanatafuta mmiliki fake, wanakwenda na wewe ofisini na kukuwekea Mhuri. Wewe utatoa pesa yako bila wasiwasi kwa kuwa uko na viongozi wa mahali husika.
Hili kuepuka utapeli.
1. Ukipata eneo, ondoka kwanza halafu siku nyingine urudi peke yako, tafuta mwenyeji anaepakana na eneo hilo. Mpeleleze ili akuambie nani mmiliki wa hilo eneo, ikibidi mpe pesa kidogo. Usiwaamini viongozi wa mtaa/kijiji
2. Hakikisha mke au mume wa muuzaji anakuwa shahidi katika ule mkataba. Hakikisha unafahamu makazi ya muuzaji